BlackBerry yarudi upya na simu itakayofunika asilimia kubwa ya simu zilizopo sokoni

BigBaba

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,908
9,040
Ng'ombe hazeeki maini. Kampuni ya BlackBerry inatarajia kurudi tena sokoni kwa kuzindua Smartphone yake ya BlackBerry Keyone ambayo itakuwa na vitufe vya QWERTY na itatumia mfumo wezeshi (Operating System) ya Android v 7.1 Nougat, ikiwa na 8MP kamera ya mbele yenye flash, kamera ya nyuma yenye 12MP auto-focus large pixel pamoja na Fingerprint Sensor.



Simu hii pia itakuwa na injini yenye RAM ya 3GB na internal memory ya 32 GB lakini itakuruhusu kuweka memory card yenye ukubwa wa hadi Terabyte 2
 
Sawa blackberry anarudi, swali la kizishi sim milioni je uko kijijini kwa wazee umefanya manuva yoyote, umetoa zile nyasi, vip ule mlango, madogo vip sale za shule, ni mda gani mama au baba hawanaona ile sms ya imethibitishwa

Ebu ukiwa unaipigia bajeti hii blackberry basi piga na hesabu za utatuzi wa changamoto za home
 
wacha tusubiri second hand tu, au kwajamaa zangu wa ubungo mataa
 
Hapo kwenye kutumia OS ya android ndio wamekosea, watengeneze ya kwao kama iPhone ili wabaki kuwa unique. Siku izi unakuta litablet likubwa utazani la maana kumbe ni Android ngapi sjui inabaki kua just another Android with a better handset
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…