BINADAMU NI MNYAMA?

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
BINADAMU NI MNYAMA?

DR. MUHAMMED SEIF KHATIB

Sayansi ya kibaiolojia inamjumuisha binadamu kuwa katika kundi la manyama. Hata jarida moja liitwalo Time Magazine la March 14 mwaka 1994 limethibisha kuwa “hakuna chembe ya tofauti inayombagua binadamu na mnyama. Binadamu ni mnyama na mnyama ni binadamu. Tunaweza kutoa tafsiri kuwa mnyama ni kiumbe hai ambaye kwa kawaida huwa na miguu minne na binadamu ni mja au mahuluku. Hivi maelezo hayo yanatosha kutafausha? Wengine hujenga hoja kwamba binadamu anao uwezo wa kutengeneza vifaa, anao uwezo kupima mambo, na kutumia moto na anaweza kucheka na kulia. Hivi mambo haya yana mvua yeye hulka au mfanano na mnyama?

Binadamu hadi leo tokea kuja kwake duniani amekuwa akitafuta asili na chimbuko lake. Binadamu mwenyewe katika maisha yake bila ya kushurushwa amekuwa kigezo cha tabia na hulka zake sawa na mnyama. Hujifananisha na ndege, samaki, mdudu na mnyama. Binadamu anajichunguza mwili, umbo na tabia yake na hamaye anafananisha na jamii ya wanyama tofauti. Hali hii inathibisha jewellery kuwa binadamu ni mnyama. Yupo popo mnyama anayeruka kama ndege ingawa si ndege. Kwa maumbile hayo ya kuwa mnyama lakini anaruka, kubeba hulka za ndege na mnyama, sawa na kuwa ndumakuwili yaani mtu muovu lakini ajifanyaye mwema na rafiki.

Huyu ni mzandiki na mnafiki. Yupo kinyonga, mjusi anayetembea tarabu na mwenye tabia ya kujibadilisha rangi ili afanane na pahali alipo. Huyu naye ni kigeugeu. Yupo samaki kitatange. Huyu ni aina ya samaki wa rangi ya njano, umbo la duwara na mwenye pezi lililosambaa miongoni. Ni samaki mwenye tabia uchokozi wa kuwasukumia samaki wengine waingiye ndani ya mtego lakini yeye hangi. Yupo ndege kunguru ndege mkubwa kiasi mweusi wengine wanabaka jeupe shingoni. Nini ila yake? Ni ndege mjanja, mwoga na mwizi. Hulka hii haipo kwa binadamu? Yupo punda, mnyama anayetumiwa kubeba mizigo na mwenye mizigo. Yeye anahusishwa na mambo mawili, kuwa mkaidi na hana shukrani. Hana shukrani kwa wema anaotendewa na mmiliki wake.

Wanyama wote hawa wakiwemo, wadudu, samaki na ndege wanafanana na tabia na hulka za binadamu. Ingawa hawatembei kwa miguu miwili, wala hawacheki na kulia wanafanana na binadamu. Wanyama hawa hawatengenezi vifaa wala kuoka moto lakini nao wanafanana kitabia na binadamu. Hebu zama katika tafakuri wakumbuke watu kadha, visa vyao, viroja vyao na mikasa yao, huwaoni miongoni mwao wenye hulka na tabia ya popo, kunguru, kinyonga, kitatange na punda? Hakuna tofauti kati ya binadamu na mnyama. Wapo katika Tanzania wenye kuamini kuwa vyama vya TANU na ASP vilivyokomboa nchi zetu havistahiki heshima. ASP haikupasa kufanya Mapinduzi ya kumamua Sultan Jamshed ambapo kama si Mapinduzi hadi leo angekuwepo Sultan kwani yupo hai huko UINGEREZA.

Yeye alirithi usultan uliodumu tokea mwaka 1832. TANU ilifanya kosa kumamua Mwingereza?. Heshima ya Mwaafrika katika ardhi yake imeletwa na ASP na TANU. Ukombozi uliletwa na wazee wetu walipokuwa vijana. Walikuwa na maisha duni. Walijitolea kwa kidogo walichonacho kuendeleza mapambano. Juu ya unyonge wao na kujinyima walipambana na hamaye kuukata mayororo wa ukoloni mkongwe na usultan wa el Busaidy. TANU na ASP zikaungana kwa dhamira ya kuleta Umoja na kuendeleza azma yao kuwapata maisha ya ustawi hatua kwa hatua kwa Watanzania. Maendeleo yaliyoletwa na vyama vya ASP, TANU na CCM kwa kipindi hiki ni makubwa ukilinganisha na Utawala wa Usultan huko Zanzibar kati ya mwaka 1832 na 1964.

Hali kadhalika Tanganyika ilitawaliwa na Wajarumani, Waarabu (mwambao) na Waingereza zaidi ya karne mbili. Nchi ilikuwa nyuma na watu wake walikumbwa na ufukara, maradhi na unyonge. Wakati mwakani CCM mrithi wa TANU na ASP inafikisha nchi miaka arubaini, bado wapo binadamu wanabeza ukombozi, mtangamano na maendeleo yaliyofikiwa. Wenye kauli hizo wao wamesomeshwa na fedha za walipa kodi za wakulima na Wafanyakazi. Hivi nani hajui kuwa wao ndiyo wenye maisha mazuri. Watoto wao wanawasomesha katika shule binafsi au wapo nje. Ni wao wenye kupanda magari mazuri na ya kisasa huku mke na watoto kila mmoja na gari lake. Ni wao waliojitenga na wengine na kujijengea “mahekalu” yanayoshindana kwa uzuri na miundo.

Nyumba zao ni pepo ya dunia. Wamefungua makampuni, wanamiliki viwanda, mashamba makubwa na ranchi za ngombe, mbuzi na kondoo. Hawajiulizi bila uhuru na Mapinduzi wangepata wapi fursa hii. Kejeli na dharau hii wanayo ni kwa sababu CCM imewamua watawala wa kikoloni na kisultan na kutoa fursa kwa wazalendo, ndipo wao wakapata fursa ya maisha bora kuliko wengi vijijini. Sina hakika kundi la aina ya watu wa aina hii lisito kuwa na shukrani na TANU, ASP na CCM watakuwa kundi gani la kufanana hulka za wale wanyama popo, kitatange, kunguru, kinyonga au punda. Binadamu ni mnyama.

00000
 
Mohammed Seif Khatib ni mtu mnafik asiye na shukrani. Ni mchumia tumbo tu hana Jipya, atawadanganya hao hao magozi wenziwe.
 
Ilichokifanya can ni 5%tu Kati ya 100 %
Hizi zingine ccm wametumia kunufaisha matumbo na familia zao
 
Eti binadamu ni mnyama na mnyama ni bindamu, binadamu ni mnyama lakini sio wanyama wote ni binadamu, binadamu anajitambua ingawa wapo mapunguani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…