Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Kinachotutesa sisi sana ni kuwekeza juhudi zetu na matumaini yetu kwenye hisia zetu, bila kujua kwamba hisia zetu huwa hazidumu. Siongelei mapenzi abadani, naongelea whole life process. Maisha yetu kwa ujumla na kila kitu kilichotuzunguka.
Najua hujanielewa, basi endelea kusoma.
Sisi binadamu huwa haturidhiki milele na haturidhiki kwa kuwa hisia zetu ni za mpito. Kile kinachotupa furaha leo si kile kitakachotupa furaha kesho sababu baiolojia yetu inatusukuma kupata kitu kipya kila siku.
Wanasaikolojia wameeiita hii hali kama "Hedonic Treadmill". Mara zote huwa tunapambana kutafuta vitu ambavyo huwa tunahisi tukishavipata basi tutatosheka. Ila baada ya kuvipata tunafurahi navyo kwa muda mfupi kisha tunaviona vya kawaida na kuvipuuza hiyo hali sasa ndio Hedonic Treadmill Theory.
Unapambana kutafuta gari jipya na zuri ukihisi baada ya kulipata utafurahi zaidi. Lakini ukishalipata na likawa karibu yako, basi utaliona la kawaida na kuanza kupata shauku ya kutafuta lingine. (Binadamu hatosheki na hisia zake) mfano huu una apply kwa kila mwanadamu juu ya kila kitu iwe mpenzi, nyumba, fedha au chochote kile shauku ya kukipata ndio hutusukuma kukiona ni cha maana sana ila baada ya kukipata tunapuuza.
Josh Kaufman alipoelezea kuhusu Hedonic Treadmill, alianza kusema "Happiness is a problem". Halafu akaendelea kusema "huwa haturidhiki na kile tulichonacho kwa muda mrefu. Baada ya kukizoea tu na kukiona cha kawaida huwa tunapata hamasa mpya ya kutafuta kingine.
Na ndio maana furaha za wanadamu huwa hazidumu, na ndio maana matatizo ya wanadamu huwa hayaishi sababu kila siku tunapata tamaa ya kitu kingine na tunajitoa sadaka kukipambania. Mark Manson mwandishi wa kitabu cha The Subtle art of not giving a https://jamii.app/JFUserGuide anasema kwamba (our problem is recursive and unavoidable due to our emotions)
Huwa tunajidanganya kuwa tuna uwezo wa kutosheka endapo tutakipata kitu fulani. HUO NI UONGO.
Huwa tunajidanganya kuwa tuna uwezo wa kutatua matatizo yetu yote. HUO NI UONGO.
Ukielewa Hedonic Treadmill, basi utaelewa mzunguko mzima wa maisha yako. You will understand that, we adopt to our success in a very short period of time and our success no longer gives us pleasure.
Kwa msaada mkubwa wa kitabu cha The Subtle Art Of Not Giving A https://jamii.app/JFUserGuide, by Mark Manson. (chapter 2)
Wenu katika kalamu Amani Dimile
#thesubtleartofnotgivingafuck #amanidimile #tusomevitabu