Binadamu hawaishi kusema

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
Binaadamu wanaweza kusema lolote pale unapochukua maamuzi fulani kwenye maisha yako.

Lakini kama unahisi hiko ndio UNACHOKITAKA na uko sahihi USIYUMBE, hata siku moja usifate mtu kasema nini katika MAAMUZI MAKUBWA ya maisha yako, sababu hayo ni YA KWAKO!! MATOKEO YOYOTE ya maamuzi utakayochukua ni yako wewe.. wengine ni WATAZAMAJI TU.

Na ukiwafuatisha usitegemee kuwa baadae watakuwa na msaada wowote katika kurudisha kile kilichopotea ama kutengeneza palipoharibika kutokana na KELELE ZAO.

Kama ni FURAHA ama UCHUNGU ni wewe ndio utakaekuwa unapitia tena kwa kiwango kilekile cha maamuzi uliyochukua bila kujali ulishauriwa ama uliamua mwenyewe, Wakati huo waliokushauri ama kuongea hawatakuwepo hivyo kama ni kulia ama kucheka ni peke yako.

Si kila mtu ANAJUA moyoni mwako kabisa kitu gani UNACHOTAKA usifanye kupendezesha watu.. watu wapo na wana maisha yao, HAYO NI MAISHA YAKO na wewe ndio mwenye MAAMUZI!.
 
Binadamu wamezaliwa wanasema huwezi kuwazuia cha muhimu ni kuishi na kufanya unavyofikiria cha muhimu usivunje sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…