Bima ya afya iache ubaguzi

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
4,433
9,427
Mnogage,

Wakuu kuna kitu mm sikielewi kuhusu bima ya Afya ya Taifa, NHIF, bima hii ni yetu sote lakini m naona imekaa kuwapendelea watumishi wa serikali na kututesa watu tulipjiajiri ambao ndio wengi,
Kwanin nasema hivyo ?

Tazama, mtu anaelipwa 1,040,000/- anakatwa 31,000/- kwa mwezi kama mchango wa bima sawa na 373,000/- kwa mwaka, na hapo anatibiwa yeye, mwenzi wake na wategemezi wanne, na hata kama serikali ikimatch mchango itakuwa ni sawa na 746,000/- kwa mwaka kwa mtu na wategemezi wa nne, na hapo mtu anaenda kutibiwa hospital yeyote bila uhitaji wa rufaa wala nini,

Sasa watu wa pvt ukitaka kupata huduma hio itabidi ulipie 2,200,000/- , utofauti wa 1.5M 💔💔 na hapo bado utakutana na mashart kibao kama vile ili utibiwe inabidi uanzie hospital za chini, wakati mwenzako anaelipa 370,000/- anaweza enda moja kwa moja Muhimbili,


Huu ni ubaguzi wa hali ya juu na unafanya watu wengi washindwe kujiunga kwa sababu bei zenu mnaweka ionekane bima ya Afya ni anasa sana kumbe sio anasa,

M nawashauri, bas wekeni kiwango sawa, na sisi wa pvt tulipie hio 746,000/- kama watu wa serikalini

Salary slip ikionyesha makato ya bima
IMG-20230628-WA0006(1).jpg

Vifurushi vya kitapeli vya bima ya Afya kwetu watu wa pvt
IMG_20231120_113701.jpg
 
Hatuhitaji pole, tunahitaji NHIF watupe huduma kwa bei sawa kwa watanzania wote, bila kujali unafanya kazi serikalini au lah
wewe tafuta unafuu wako tu, ukitafuta kujilingamisha na watumishi wa serikali utakuwa unaingia chaka. Unajuaje kama hiyo si moja ya motivation kwao kutoka kwa mwajiri, au hujasikia watumishi wa serikali wakilalamikia mishahara haitoshi? Halafu usichojua mtumishi yeye anakatwa asilimia ya mshahara tu bila kujali ana mke au mtoto, bora nyinyi private unachagua kifurushi kuendana na mahitaji uliyo nayo.​
 
Naunga mkono hoja.
Mfuko huu hauna budi kujitafakari kama unatenda kwa usawa kwa wanachama wake hususan kipengele cha Rufaa.
Kwamba, niliyeko chini ya Timiza Afya natakiwa kupata rufaa kutoka hospitali moja kwenda nyingine ilihali anayechangia kidogo ( ndani ya mfuko) akipewa uhuru wa kwenda anakotaka kupata matibabu!

Najiuliza huu ubaguzi unasababishwa na nini?
Nina ndugu aliyefanyiwa upasuaji Bugando kurudi clinic anaombwa rufaa! Kwamba anapaswa kuanzia hospitali ya chini kabla ya Bugando ambako tayari alifanyiwa upasuaji.

Kufika hospitali ya mkoa Sekou Toure daktari anasema tatizo hilo linatibiwa Muhimbili. Jitihada za kumshawishi atuandikie rufaa kwenda Bugando zilifanikiwa baada ya juhudi kubwa za ushawishi ndani na nje ya hospitali.

Kufika Bugando, daktari akashauri tumwone daktari mwingine, watu wa Bima wanakataa wakitaka turejee sekou toure tupate rufaa nyingine kwani ile ya awali haijueleza hilo tatizo la pili.
Baadaye ikabainika kuwa magonjwa yote yako kwenye rufaa husika lakini watu wa bima hawakuweza kuelewa maana yake!
Nashauri waajiri watu wenye uelewa wa taaluma ya utabibu kupunguza adha zisizokuwa na ulazima.
Pia, inawezekana kuna "Bifu" kati ya BMC na Sekou Toure ambao wanatafutiwa wateja kwa " nguvu" kwa kisingizio cha tuna madaktari Bingwa ilihali anayeonekana ni mmoja au wawili.

Kadhalika inawezekana baadhi ya hospitali zinahusika na hujuma kwa mfuko lakiki dawa yake haiwezi kuwa ni kuwakomoa wanachama.

Mwisho na muhimu zaidi, Bima iache ubaguzi wa kuwaona watumishi wa umma ndio wanaostahili kutibiwa hospitali yoyote ilihali wengine wakizuiwa
 
Back
Top Bottom