Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 10,185
- 29,514
Wakati Diamond Platnumz alikuwa na miaka 17, alifanya kazi ya kuuza nguo za mitumba na kuuza mafuta kujaribu kuweka akiba ya kumwezesha kurekodi studio, lakini haitoshi. Hatimaye mwimbaji huyo mwenye jina la kuzaliwa la Naseeb Abdul Juma Issack, aliuza pete ya dhahabu ya mama yake. "Nilimwambia nimeipoteza bafuni - kwamba imeanguka chini ya choo," anasema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 31, akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam, Tanzania.
Wimbo alioutoa alipoenda studio uliitwa "Toka Mwanzo," ambao ulikuwa na miondoko ya R&B ambayo alikuwa bado hajaimudu vizuri, na haukupata mafanikio makubwa. Lakini kwa kukaa studio kulimfanikisha Diamond kukutana na meneja wake wa kwanza, ambaye alimlipia muda zaidi wa kurekodi studio. Mnamo 2010, aliachia wimbo uliokuja kumpatia mafanikio makubwa na kumtambulisha kama msanii, "Kamwambie," ambao ulisababisha ushindi mkubwa wa tuzo tatu kwenye Tuzo za Muziki Tanzania, na mara tu baadaye, Diamond alitoa albamu yake ya kwanza ya aliyoiita "Kamwambie" kama jina la wimbo wake.
Alivyoingia katika aina ya muziki wa bongo flava - unaojulikana kwa kuchanganya mtindo wa rap ya Marekani na taarab ya Afrika Mashariki - muziki wa Diamond, ambao mara nyingi hugeuza maumivu ya mapenzi kuwa nyimbo za kuinua, ulimpatia msingi wa mashabiki. Wimbo aliotoa mwaka 2013 "Number One" ulifanikisha lengo kubwa zaidi: "Nilitaka kwenda ulimwenguni," anasema, akiongeza kuwa alijifunza Kiingereza, ambapo aliimba kwa lugha hiyo kwenye kiitikio cha wimbo huo, kabla ya kuurekodi.
Mnamo mwaka wa 2020, Diamond alikua msanii wa kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata kutazamwa zaidi ya mara bilioni 1 katika mtandao wa YouTube na mwaka huu aliteuliwa katika kinyang'anyiro cha mwanamziki bora wa kimataifa kwenye Tuzo za BET kwa mara ya tatu. Mnamo Mei, msanii - ambaye ana mpango wa kutoa albamu yake ijayo mwaka 2021 - alisaini mkataba wa 360 na "Warner Music Group" kupitia lebo yake, WCB Wasafi (iliyozinduliwa mnamo 2018 na Lava Lava, Queen Darleen na Mbosso). Chini ya ushirikiano huo, WMG inaisaidia lebo ya Diamond katika lengo la kuunda njia zinazofaa zaidi kwa wasanii wa Afrika Mashariki kufikisha muziki wao Nchini Marekani ambapo wasanii wa bara la Afrika wamekuwa wakianza kutizamwa kwa ukaribu zaidi nchini humo. "Kuna wasanii wengi wa Kiafrika wenye talanta ambao hawawezi kupata muda wa kusikilizwa, hawawezi kupata mikataba ya kurekodi," anasema. "Ninaweza kuona nikibadilisha maisha ya watu wengi."
Source: