Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,620
- 1,201
Bilioni 1.7 Kulipa Posho za Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa
Serikali imeendelea kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa posho wenyeviti wa vitongoji na vijiji na kuongeza posho ya Madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
“Katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.7 ambapo kufikia Februari, 2024 shilingi Bilioni 1.15 zimetolewa kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa.” amesema Dkt. Dugange
Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetenga shilingi Bilioni 20.8 kwa ajili ya kulipa posho za Madiwani katika halmashauri 168 ambapo kufikia Februari, 2024 kiasi cha shilingi Bilioni 13.5 kimetolewa.