Sheria ya Bodi ya usaili wahandisi inampa madaraka yote Waziri husika na Rais kwenye uteuzi wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini na uwakilishi huo ni batili kwa sababu hautokani na ridhaa ya wahandisi wenyewe.
Matokeo yake matakwa ya wahandisi hayashughulikiwi na ya serikali tu ndiyo hufanyiwa kazi na kuishia shughuli nyingi zinazohitaji utaalamu wa uhandisi hufanywa na wasio na sifa.
Huku tunahimiza watoto wakazanie masomo ya sayansi lakini ikija ajira kazi zao hufanywa na wale walioyakacha na kuacha maswali kuna faida ipi.
Majengo yakiporomoka ndiyo tunagundua kumbe managing director siyo mhandisi ujenzi naye kibosile yule huo hugeuka kuwa ni utetezi wake. Kuna ugumu gani kwenye sheria ya uhandisi ikazuia wasio wahandisi kutofanya kazi za wahandisi na makosa ya kukiuka sheria hii ni makosa ya jinai.
Kudai ni nafasi ya kiutawala huko maamuzi anayoyafanya ni ya kitaalamu ni kuhalalisha kazi chafu kila mahali ambazo hazizingatii utaalamu husika.
USHAURI.
Sheria ya bodi ya wahandisi irekebishwe kwa wahandisi kuchagua wahandisi kuchagua viongozi wao wenyewe wanawaona wanawafaa badala ya uwakilishi haramu kupitia Rais na Waziri husika.
Pili, sheria tajwa itamke kwa uwazi ni makosa ya jinai kwa mtu yoyote kufanya kazi za uhandisi ziwe za nafasi za juu za kiutawala kwenye makampuni binafsi au serikalini. Hii ni pamoja na managing director, bank signatories, ministerial and permanent secretaries na zenye sifa kama hizo.
Kwenye makosa ya jinai tajwa pia itajwe bayana watendaji kwenye mabenki wataguswa kama watapitisha bank signatories ambao hawajasajiliwa kama wahandisi
Bila ya kuwawezesha wahandisi kwa marekebisho ya sheria ya usajili ya wahandisi basi ujenzi wa viwanda ni njozi isiyotekelezeka