6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,665
- 5,623
Niaje waungwana
Baada ya wazungu kufanikiwa kuwaweka watu wao pale mashariki ya kati (Palestina + Israel), Plan ya pili ilikuwa ni kuwasaidia watu hao kujitanua kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kidogo kidogo, mpaka pale watapojikuta wamefanikiwa kujenga empire na kuzifikia zile nchi zenye uchumi mkubwa wa mafuta kama vile Saudi Arabia, Iraq, Iran nk.
Baada ya kufanikiwa kuzifikia nchi hizo, hatua ambayo ingefuata ni kutumia ukubwa wa empire yao kuvamia nchi moja moja. Na ingekuwa rahisi kwa sababu empire yao ingekuwa kubwa, plus misaada ya kijeshi kama vile silaha kubwakubwa kutoka Marekani na Ulaya, fedha za kuwasaidia kununua material mbali mbali ya kutengeneza silaha nk. Hivyo wangepiga nchi moja moja na kuchukua eneo lote la Mashariki ya kati lenye utajiri mkubwa wa mafuta, na kuhakikisha kuwa eneo lote linakuwa chini ya nchi hizo za magharibi kupitia mgongo wa Israel.
Waarabu haswa zile nchi zilizokuwa kwenye target kama vile Saudi Arabia, Oman nk wao hawakuwa na habari ya kile kinachoendelea au kinachopangwa kufanywa dhidi yao. Wao kikubwa washibe wali, watafune tende na kulaghaiwa kwa maneno matamu na serikali za Marekani, UK na nchi nyingine za magharibi.
Shida kubwa kwa viongozi wa nchi za magharibi ilikuwa ni namna gani wataweza kuidhibiti Iran ambayo haionekani kudhibitika. Wakitega mtego wa wali na tende kama walivyowategea waarab muajemi hakamatiki, wakitengeneza propaganda za kumdhoofisha muajemi hadhoofiki, wakimuwekea vikwazo ili kuuwa uchumi wake moja kwa moja, jamaa wanatumia njia nyingine kukwepa vikwazo na kuiingizia nchi yao hela za kufanya mambo yao kama kawaida. Kifupi jamaa waliwatia jasho viongozi wa magharibi awamu kwa awamu.
Kila raisi wa Marekani alipoingia alikuja na mbinu zake, mwisho wa siku muda wake unaisha bila mbinu zake kufanikiwa, anakuja raisi mungine, hivyo mpaka anatoka bila mabadiliko yoyote ya mafanikio. Hii ni toka miaka ya 70 mpaka leo waajemi wameshindikana, na kuwa tishio kubwa kwa mpango wao walioupanga miaka mingi.
Waajemi ambao wao kiasili sio waarab, waliliona hilo mapema kabla hata halijapangwa vizuri mezani. Wakajitaarisha mapema na chochote kitachotokea wadili nacho muda huo huo kabla ya kujitanua na kusabanisha madhara makubwa kwa nchi yao na majirani zao.
Na hapo ulitumika uzoefu walio nao miaka na miaka. Historia tena ya wazungu wenyewe inakubali kwamba Uajemi kabla ya kuzaliwa Yesu (BC), na kabla ya utawala wa waroma, waliwahi kuwa na empire (himaya) ambayo ilitawala sehemu kubwa huko Asia ikiwemo Israel ya leo. Hivyo hawa ni watu wenye nguvu, akili na uwezo mkubwa wa kujilinda toka maelfu ya miaka iliyopita. Leo hii ukitaja nchi ambazo ziliwahi kuwa na empire kubwa na zenye nguvu duniani basi yao pia himo.
Sasa basi, baada ya waajemi kugundua mipango hiyo, wakaanza kutafuta mbinu za kumdhibiti adui na wasaidizi wake.
Before Israel na Marekani hawajajiandaa kufanya mpango wa kuzivamia kwanza Lebanon, Syria nk, yeye muajemi akawawahi kwa kuwaweka vijana wenye silaha, mbinu za kijehi na misimamo ya kupigania ardhi zao pale pale karibu na mipaka ya Israel. Hivyo kuhakikisha kwamba kabla maadui hawajasogea huku kukamata nchi hizo za Syria, Lebanon na nchi yote ya Palestina, wadhibitiwe kwanza na vijana hao ambao wengi wao wameshatoboka roho, kufa kwao ni sehemu ya maisha tu (kama vile kula, kuoga, kuvaa au kwenda chooni) tofauti na askari wa Israel ambao wao wanaenda vitani, huku wakiwafikiria wake zao na watoto wao.
Na kweli mpango huo wa waajemi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuzima ndoto za mataifa ya magharibi kuziteka na kuzikalia nchi hizo kama walivyopanga. Leo hii waarab wa Saudi Arabia ndo kama vile akili kwa mbaali zinaaza kuwaingia na kuanza kushirikiana na muajemi kidgo kidogo baada ya kupewa mchoro mzima wa kile kilichokuwa kinapangwa na wakorofi hao wa dunia.
Lakini pia pamoja na kuandaa vijana wa kuidhibiti Israel isijitanue kama ilivyopangwa, vilevile hawakutaka kuipa nafasi nchi yoyote adui asogelee anga lao, ndomaana kila Mmarekani alipojaribu kusogeza ndege zake na meli zake za kijeshi karibu na anga la waajemi zilishambuliwa zote na kuachwa majivu matupu.
Kwa namna hiyo ikabidi mmarekani na yeye aje na mbinu kama ya waajemi kwa kuweka watu wake mashariki ya kati ambao na wao watapambana kwa lengo la kulinda masilahi yao, na pengine kuangalia njia za kuwadhibiti vijana waliowekwa na waajemi.
Kundi hilo la kulinda masilahi ya Marekani likapewa jina la Alkaida, wakakusanywa kina Osama, wafuga ndevu mbali mbali na wale wafia dini ambao hawakuwa wanajua kinachoendelea katika mpango ule. Yani unakuta mfia dini na yeye anajiunga na alkaida kumuunga mkono Osama bila kujua kwamba Osama mwemyewe yupo kwenye mission zake.
Baada ya miongo kadhaa ya Osama na genge lake kuleta sintofahamu mashariki ya kati, na Osama kuonekana kuwa ameshachoka kuendelea na mission ile kutokana na umri, pia kupoteza mvuto kwa alkaida mashariki ya kati, ikabidi waamue kumrudisha Osama Marekani akaendelee na maisha yake ya kula bata na wajukuu zake kutokana na kazi kubwa aliyoifanya. Ila ili arudishwe Marekani na kuacha kuzungumziwa alipoendea ikabidi ipangwe ambush ya kutengeneza kifo chake ili asije akafuatiliwa tena waandishi habari ambao wengi wangetaka kujua alipo na operation ya mchongo ya Marekani kumtafuta imeshia wapi.
Osama akapangiwa kifo cha kutengenezwa waandishi wa habari walipotaka kuoneshwa maiti walizungushwa zungushwa na kukwepwa, walipotaka pia kuonesha angalau kaburi wakaambia amezikiwa baharini na picha likaishia hapo. Mpaka leo hakuna aliona maiti ya Osama wala kaburi lake. Lakini wale waliouwawa ki ukweli kama kina Ghadafi, Sadam Hussein na wengine wengi wa aina hiyo maiti zao zilionekana na makaburi yao yanajulikana yalipo.
Baadae likatengenezwa kundi lingine na kupewa jina la Islamic state ila makundi yote yanapoanzishwa yanapewa onyo kwamba yafanye uharibifu kote mashariki ya kati ili kutimiza lengo la kusogelea mipaka ya adui (Uajemi), ila wasijisahau wakaingia mpaka Israel kutengeneza maafa kwa ndugu wa wale waliowatuma. Hivyo hauwezi kukuta makundi hayo yana mpango wala wazo la kuvamia Israel kama wafanyavyo Hizbulla, Hamas na wengine ambao hawana deal na magharibi.
Muajemi sio sawa na Iraq au Libya kwamba utaenda kuivamia muda wowote. Ile haivamiliki kishamba, ndomaana Marekani na washirika wake waliweza kuzivamia Iraq, Libya, Vietnam, Syria, Cuba nk ambazo kimsingi hazijawahi kufanya uharibifu wowote kwa Marekani, lakini Muajemi ambae hufanya uharibifu mkubwa na sometimes mauaji kwa askari wa Marekani hawajawahi kuthubutu kuigusa, cause wanajua wakithubutu kuigusa nchi hizo zitakumbana na vita ambayo itasababisha hasara kubwa kwao, lakini muda huo wanajua Israel haitokuwepo tena katika ramani ya mashariki ya kati anymore, hivyo CIA na Mosad wanawaambia kabisa viongozi wao kuwa jamaa hawaingiliki hovyo hovyo, maana ni hatari na nusu. Ndomaana miaka yote wamekuwa wakifanya ambush tu za hapa na pale, lakini muajemi na yeye anajibu kwa kishindo na kwa madhara makubwa mno kwao.
Hilo ndio swala linalomfanya sasa hivi raisi wa Marekani akubali yaishe kwa kutaka kuundwa taifa lingine la Palestina, waisrael wabaki na sehemu yao waliobahatika kuiteka miaka hiyo. Maana amegundua kwamba ile mbinu waliokuwa wamepanga kamwe haitowezekana as long as Iran still Super Power katika eneo lao la Mashariki ya kati. Bila yenyewe sasa hivi nchi zote zingekuwa mikoa ya Israel na Marekani angetengeneza bomba la mafuta kutoka katika Saudia Arabia, Iran, Iraq, Syria liende hadi kwake. Halafu UK na wamagharibi wengine nao wajipendelee nchi zingine zilizobaki.
But ndo hivyo mission is impossible. Waarab wawashukuru sana waajemi kwa kuwalinda.