Kuelekea 2025 Bila Uwepo wa CCM Madarakani Nchi ingekuwa Imesambaratika na Kugawanyika vipande vipande

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
25,401
18,826
Ndugu zangu Watanzania,

Nikitizama na kufuatilia namna vyama vya upinzani vinavyoendeshwa ,vinavyofanya maamuzi yake,mfumo wa uongozi na namna ya kupokezana madaraka, uvumilivu na demokrasia katika vyama hivyo nafikia hitimisho kuwa kama siyo uwepo wa CCM Madarakani basi Taifa hili lingekuwa limesambaratika na kugawanyika vipande vipande.

Angalia tu namna viongozi wa upinzani wanavyong'ang'ania madarakani kwenye vyama vyao hususani kwenye nafasi ya Uwenyekiti. Jiulize Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba Na Mh Mbowe ni wenyeviti wa vyama vyao tangia lini? Wameongoza kwa miaka mingapi? Kipi walichobakisha kinachowashinda kuacha mawazo mapya yachukue nafasi ndani ya vyama vyao? Angalia tu Mh Mbatia mpaka alitoka kwenye Uwenyekiti baada ya migogoro na kufurushwa na wenzake.

Vipi kama hawa wapinzani kama CHADEMA ndio wangekuwa wanaongoza nchi? Si wangebadili hadi katiba kwa kutaka mtu mmoja tu aendelee kuongoza yeye peke yake? Angalia tu namna ya kusuluhisha na kutatua migogoro ndani ya vyama hivi vya upinzani. Mara nyingi migogoro yao imeishia kufukuzana na kutupiana maneno hadharani.kwa kuwa havina ukomavu wala stamini ya kumaliza migogoro yao kwa amani na utulivu na kuendelea kuwa pamoja ndani ya chama.

Mfano vyama hivi vingekuwa na uwezo wa kusuluhisha migogoro yao basi tusingeshuhudia akina Mheshimiwa Zitto Kabwe, Profesa Kitila Mkumbo,Samsoni Mwigamba, Dkt Slaa, Juliana Daniel Shonza, Mtela Mwampamba, Julius Mtatirilo, David Kafulila, na wengine wengi wakidhalilishwa na vyama hivyo hasa CHADEMA kwa kuwa tu walikuwa na mawazo tofauti na ya Mwenyekiti wake wa Muda wote. Hapo bado sijazungumzia habari za akina profesa Lipumba na hayati Maalim Seif au hayati Agustino Lyatonga Mrema na wenzake.

Kwa hiyo unachokuja kuona ni kuwa vyama hivi bado ni vichanga sana ,ambapo haviwezi kamwe na katu kufikiriwa wala kuwaziwa kupewa ridhaa ya kuongoza Taifa letu.kwa kuwa bado havijakomaa kimfumo na hata namna ya kuendesha mambo yake.havina uwezo wa kuishi na kuwaunganisha watu wote hata wale wenye mitizamo tofauti ndani ya chama.ndio maana kwa kukosa ustahimilivu huko wa hoja mpya au mawazo kinzani huishia kufukuzana na kuwa maadui kama paka na panya.

Lakini ukija CCM Ni Chama ambacho kina uwezo wa kuishi na kukaa na watu wa aina zote na wenye mitizamo tofauti tofauti na kutoa nafasi ya kila mmoja kusikilizwa mawazo yake na kupingwa kwa hoja au kuelimishwa pasipo kuitwa adui wa chama au msaliti na hatimaye kufukuzwa. Ndio maana CCM imekuwa kimbilio la wanasiasa wote wanaoonewa kutoka upinzani.ni chama chenye utaratibu mzuri wa kutatua migogoro yake baina ya wanachama wake,mfumo imara wa kiuongozi na namna ya kuheshimu maamuzi ya chama.

Sasa leo kwa vyama vya upinzani unakuta wamefanya maamuzi kwa pamoja halafu anatokea kiongozi mwingine anasema sijuwi jambo hili la kumualika Rais kwenye chama chetu lilifayikaje? Cha ajabu ni kuwa huyo anayeuliza hayo hadharani ni kiongozi mwandamizi na aliyeshiriki katika vikao vyote halali mpaka mwisho wa vikao. hii yote ni kukosa uelewa wa maana ya uongozi na vikao halali vya chama na maamuzi yake. Je umewahi kuona ni nani ndani ya CCM anaweza kutoka hadharani kupinga maamuzi ya vikao halali ambavyo hata yeye mwenyewe alishiriki?

Kwa uchanga wa vyama vya upinzani pamoja na uchu na uroho wao wa madaraka ndio maana vinashindwa hata tu kuungana na kuunganisha nguvu zao na mikakati yao kwaajili ya kushinda uchaguzi fulani. kwa sababu vyenyewe kwa vyenyewe tu vinadharauliana na kushambuliana muda wote.haviaminiani wala kuamini katika umoja. Ni vyama vipo vipo tu na vilivyokosa muelekeo na Dira ya kueleweka ya kuweza kuviongoza.

Kama siyo uwepo wa CCM Madarakani kwa hakika kwa sasa tungekuwa tunashuhudia Taifa likiwa limejaa na kutamalaki ukabila uliokithiri, ubaguzi, Udini, ujinsi, ukanda, kudharauliana na mpasuko wa kila aina. Maneno ya kibaguzi mnayoyasikia kutoka kwenye vinywa vya viongozi kama Lissu za kwamba huyu ni wa upande ule na sisi ni wa upande huu yangekuwa yameshamiri na kukita mizizi ardhini. Kusingekuwa na habari za upendo, ushirikiano,umoja wa kitaifa, mshikamano na Taifa moja.

Habari na sera zao za majimbo zingeendelea kuligawa na kulipasua Taifa kila uchwao kwa misingi ya ukabila na ukanda. Vita vingetokea vya wenyewe kwa wenyewe na tungekuwa tukichaguana kwa kuangalia makabila yetu,Dini zetu na kanda tunazotokea. Kwa ufupi kusingekuwa na Taifa tena zaidi ya kuwa na vipande vipande vinavyojitegemea na vinavyohitaji uhuru na utambulisho wake.

Naweka kalamu yangu chini maana naona andiko linakuwa refu sana.nitaendelea wakati mwingine tena.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Kwa mfano raisi angekuwa nani shekhe ubwabwa au baharia!
 
Back
Top Bottom