Bila shaka nchi ya Tanzania ina kinga kali sana

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,326
2,453
Kinga iliyonayo nchi ya Tanzania dhidi ya Majanga ni kali sana, hakuna nchi ya kulinganisha nayo hapa Afrika mashariki. Haijalishi janga liwe limetokea kiasili au limesababishwa na mwanadamu, nchi yetu kwa kutumia kingo za mipaka yake imetukinga sisi watoto wake.

Ukipitia twakimu kwa miaka mitano nyuma kwa nchi majirani; Mozambique, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya utanielewa kipi namanisha naposema Kinga ya nchi hii sio ya mchezo.

Kabda ya yote ngoja niwapatie tu majanga ya rejareja ambayo majirani zetu wanaishi nayo.

Mozambique - cyclone freddy 2023, cholera 2022, cyclone gombe 2022, cyclone kenneth 2019.
Malawi - cyclone freddy 2023, cholera 2022, polio 2022, ukame 2018-22, kimbunga combe.

images (1) (17).jpeg
Zambia - mafuriko, ukame 2018-2022, kipindupindu 2023.
DRC - mafuriko 2022, volcano 2021, ebola 2022, kipindupindu 2022, polio 2018, vita wenyewe kwa wenyewe. Hii nchi wakazi wake wanajua kila aina ya janga.
Burundi - mafuriko 2021, maporomoko 2020, kipindupindu 2019.
Rwanda - mafuriko 2021, upepo mkali 2021, viwavi 2017, HINI 2009
Uganda - mafuriko 2022, nzige 2019, kipindupindu 2018, ebola 2022
Kenya - mafuriko 2021, ukame 2014-23, nzige 2019, viwavi 2017, kipindupindu 2022, yelow fever 2022, dengue 2021, polio 2018. Inashangaza sana Wakenya na kingereza chote lakini bado wanahaha na kipindupindu.

images (1) (25).jpeg

Tofauti na majirani zetu enyi watanzania shuhudieni jinsi mama yetu Tanzania alivyotulinda na haya majanga.

Tanzania - alitaka kuja Jobo mwaka 2021 akapulizwa, Kenneth naye mwk 2019 alifanywa hivyo hivyo, naye jiwe akapambana na ebola na zika. Hii nchii haina mfano dunia nzima, watanzania sisi japo hatujui sisi sio wa kubezwa hata kidogo, bila shaka tuna sehemu yetu kwenye ufalme wa Mungu.

Lakini, ndugu zangu mda mwingine napatwa na mashaka kuhusiana na usalama mkubwa uliopo kwenye amani ya nchi yetu. Ukitazama kenya, Mozambique, uganda, rwanda, congo, burundi hali ni tafrani wao kwa wao wanafanyiana unyama. Na siku zote ndugu wakigombana kuna adui anayewachonganisha kwa kutumia sababu za siasa, malighafi au dini ili apate maslahi yake. Sasa mbona huyo adui hajatugombanisha mpaka leo watanzania ana mpango gani na sisi, au akishawamaliza anakuja kuishi hapa nchini kwetu.

Labda usalama huu kutoka majanga makubwa makubwa ni kutokana kuwa na nafuu ya uongozi wenye kufuata haki za kibinadamu. Hivyo kinga ni kama baraka, tumekuwa na nyerere, mwinyi, mkapa, Kikwete, Samia. Kama alivyobarikiwa Ibrahim wa Israel basi nasi huko nyuma kuna mwamba tunatembea na baraka zake. Inashangaza sana kasikazini hatari kusin hatari mangaribi hatari na mashariki wapo ndugu zetu na marafiki zetu wazanzibari na sisi tupo salama katikati. Tuwapende sana wazanzibari, ukiangalia kipindi hiki tunapata mvua ya kipimo chetu, tunafurahi , watoto wetu wanatoka nje wanaruka ruka kwenye matonye ya mvua yasio na hila yoyote ile.

Ewe mama yetu Tanzania tunakushukuru sana sisi watoto wako, ingawa tunakukwangua udongo wako na kuwapa wengine tunaomba utusamee.

Picha la kutisha kutoka shambani

images (1) (26).jpeg
 
huyo uliyemuacha pengine ndo anamchango mkubwa kwenye mshikamano kwa asilimia kubwa ya wananchi wa sasa, alileta elimu
Hata waisraeli walipata wafalme chenga, unaposema juu ya elimu nakushangaa bwana yule pasipo AIBU alifukuza wanafunzi wa kike waliopata mimba mashuleni.
Hapo sasa hao mabinti watoto wao watakuwa na elimu gani, anaunda kizazi gani.
 
Hata waisraeli walipata wafalme chenga, unaposema juu ya elimu nakushangaa bwana yule pasipo AIBU alifukuza wanafunzi wa kike waliopata mimba mashuleni.
Hapo sasa hao mabinti watoto wao watakuwa na elimu gani, anaunda kizazi gani.
Tafadhali, nimeishajua unayemuongelea hapa. ACHA habari hizi Ndugu yangu.

Nakuhakikishia leo hupati hata buku siku nzima!!!
 
Back
Top Bottom