Biharamulo: Kurudishwa kwa pesa za mishahara zilizoongezeka

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,138
3,324
Katika hali isiyo ya kawaida, watumishi wa idara ya elimu( waalimu) walioajiriwa mwaka jana, wameitwa na mkurugenzi wa halmashauri ili kurudisha pesa zilizoongezeka mwezi wa tatu. Ikumbukwe mwezi huo wa tatu watumishi wengi walilipwa madeni yao hasa ya mishahara.

Kuna watumishi tuliowekewa pesa wakati hatudai yaani mshaara wa mwezi wa tatu ulikuwa doubled. Hii ni kwa nchi nzima. Cha kusikitisha leo tumeitwa na mkurugenzi ili turudishe hizo pesa za mshaara mmoja. Alikuwepo pia afisa wa TAKUKURU ambaye ametwambia ni kosa kisheria kuchukua pesa ambazo zimeongezeka bila kuwa halali.

Sisi hatujagoma kurudisha japo tunaumia sana maana tutakuwa na hali ngumu mwezi ujao lakini tuna wasiwasi kwa namna zitakavyo rejeshwa maana tumeambiwa tunazipeleka kwa mwasibu wa halimashauri.

Hapo si zitapigwa na wajanja wa halmashauri kweli. Kwa nini mkurugenzi asipeleke majina yetu hazina wakatukata hukohuko?

Wajuzi wa haya mambo naomba mtwambie kitu.
 
Mkuu mpaka sasa bado tupo kwenye ukumbi wa halmshauri bado tunapigwa biti kwamba tutafunguliwa mashtaka na kufungwa kama tusipozirudisha.
Mrudishe kama zile za EPA? kama mliingiziwa dabo basi wasiingize tena kwa nini mpewe tena halafu mzitoe muwape tena? Bora mkubali mshtakiwe ili mahakama iiamuru hazina ikate hukohuko.
 
Asiwatishe na huyo takukuru wake, hadi anawaletea takukuru kama ndo mliofanya hyo transaction, nani alimwambia adouble kosa ni lao hela yeyote ikiwa kwenye account yako ni yako, kama anawaomba amueni nyinyi mmpe au mmnyime lakini kama anawatisha msimpe kabisa,
 
Mkuu mpaka sasa bado tupo kwenye ukumbi wa halmshauri bado tunapigwa biti kwamba tutafunguliwa mashtaka na kufungwa kama tusipozirudisha.
Dawa ni kuzirudisha then mnafuatilia kujua kama zimerejeshwa hazina. Lkn kama ni wakweli basi hazina wangekata mishahara ujao juu kwa juu. Uko umoja au biharamulo ps?
 
Dawa ni kuzirudisha then mnafuatilia kujua kama zimerejeshwa hazina. Lkn kama ni wakweli basi hazina wangekata mishahara ujao juu kwa juu. Uko umoja au biharamulo ps?
Hapo pia kuna ukakasi, kwa nini wasikate juu kwa juu. Ngoja waje wataalamu wa haya mambo na wanasheria labda kuna logic kwa hayo madai yao.
 
Mrudishe kama zile za EPA? kama mliingiziwa dabo basi wasiingize tena kwa nini mpewe tena halafu mzitoe muwape tena? Bora mkubali mshtakiwe ili mahakama iiamuru hazina ikate hukohuko.
Afisa wa TAKUKURU anasema ukishashtakiwa na kuhukumiwa maana yake na kazi unaipoteza. Kwani wasizikate huko huko?
 
Rudisheni hizo pesa ni vyema mkakwepa kula msicho kifanyia kazi...kama mnapenda kutenda haki basi nanyi tendeni haki.
 
Rudisheni hizo pesa ni vyema mkakwepa kula msicho kifanyia kazi...kama mnapenda kutenda haki basi nanyi tendeni haki.
Hatujakataa ila namna ya urudishwaji ndo inaleta ukakasi. Tupo tayar tukatwe mshaara wote mwez huu lakini sio sio kumpa mtu eti ataituma hazina
 
Duuuu bora umeimwaga kueupe mkuu
Yeah, nimeileta hapa maana naamini kuna watu wenye mamlaka zaidi yake na wataalamu wa sheria ili waone hiki kitu. Alafu hii ishu tulifanyiwa nchi nzima, kwa nini imuwashe sana yeye tu? Mbona halmashauri nyingine wapo kimya?
 
Walimu Walikula Double Bunder?
Lazima Waje Waseme Kama Ni Tanzania Nzima Mlilamba Double

Mtatumbuliwa Aisee!!!
 
Msikimbilie kurudisha hizo hela , subirini kwanza zirudishwe zile za EPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…