KERO Biashara ya lodge Sinza, Manzese na Tandale ni hatari kwa sasa! Wateja na wamiliki wanadhalilishwa na polisi kwa kisingizio Cha madada poa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,377
3,398
Inasikitisha sana kwa wakuu wa wilaya na mapolisi kuvamia guest usiku, na kuwadhalilisha wateja waliolala kama vibaka. Ifahamike kwamba gesti ni biashara kama zilivyo biashara zingine!

Kinachoendelea wilaya ya Ubungo ni udhalilishaji na kuharibiana biashara. Chimbuko la madada poa sio gesti house, ni tabia na malezi yetu wenyewe, ugumu wa maisha, nk. Mnawafukuza waende wakavamie mitaa na kuleta usumbufu kwa jamii!

Mnawapeleka mahakamani, mnaushahidi gani kama wanauza miili yao? Sinza kuna starehe nyingi, kuna ma-bar na night club! Watu wanaogopa sasa kwenda kufanya starehe zao maeneo hayo.

Hata mteja wa kawaida amepanga chumba, ana mtu wake ametoka naye alikotoka, anakamatwa kwanini? Wanafanya ambush kama wanavamia majambazi. Wafanya biashara na wamiliki wa gesti house, toeni tamko biashara zenu ziheshimiwe.
 
Hizo gharama za mafuta wanazotumia kupigia root wangeongezea kwenye ambulance ya wilaya tungeokoa wagonjwa wengi sana
 
Back
Top Bottom