Biashara ya Kufuga samaki inalipa sana. Ila ni kwanini wengi hupata hasara?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Ningependa kushare nanyi sababu mbalimbali zinazowafanya wafugaji wengi wa samaki kutofanikiwa katika hii biashara yenye Tija na Rahisi kufanya.

Huu ni mwaka wangu wa Tano toka nimeanza kufuga samaki. Hivi sasa ufugaji wa samaki ndyo biashara pekee ninayotegemea kunipa kipato na ninafurahia mafanikio ninayoipata tokana na hii biashara.

Hivi sasa nimeweza kupata utaalamu wa hali ya juu kutokana na experience ya changamoto na mafanikiyo niliyokutana nayo toka nianze kufuga samaki. Nilianza kufuga tu ila sasa naweza zalisha vifaranga vya samaki ( kambale) mpaka laki mbili kwa mwezi. Mabwawa yangu yananipatia si chini ya Tani moja ya samaki wakubwa kila mwezi.

c7cf6e05364ee60268fb1e0be1baec79.jpg

Hii miezi miwili iliyopita nilizunguka maeneo mbalimbali hapa Tanzania na kukutana na wadau wa ufugaji wa samaki. Changamoto kubwa nliyogundua inawakumba wafugaji wengi wa Tz ni KUTOFANIKIWA.

KUTOFANIKIWA kwao kunakuwa either kushindwa kuvuna samaki wenye ukubwa unaotakiwa au wingi aliotegemea. Mfano unakuta mkulima kafuga samaki elfu 3000. Ila anavuna 200 tu. Wengine wanaweza kuwa wadogo au hawapo kabisa. Inaniuma sana kuona biashara yenye fursa kama hii inageuka kuwakatisha wadau tamaa.

Ilinibidi nifanye utafiti na kudadavua sababu mbali mbali zinazowafanya wadau washindwe kufanikiwa katika ufugaji wa samaki.

1. UZEMBE WA MFUGAJI
wafugaji wengi wamekuwa wakifikiri kufuga samaki ni kuweka vifaranga bwawani na kulisha tu baada ya miez 6 aanze kuvuna. Unakuta mfugaji mambo ya msingi kama ulinzi, usafi wa maji, mazingira ya mabwawa hana habari nayo kabisa.

Ufugaji wa samaki unahitaji umakini wa hali ya juu kama ufugaji mwingine. Uzembe kidogo tu waweza kukusababishia hasara kubwa sana.

2. UKOSEKANAJI WA MBEGU BORA
Hili ndilo kosa kubwa sana wafugaji wengi wamekuwa wakifanya. Hii inaweza kuwa bila kujua, kutojali au kudanganywa na waliomuuzia mbegu. Ni kweli wafugaji wengi wanakosea bila kujua au kudanganywa na wataalamu.

Kwa mfano. Wafugaji wengi wamekuwa wakidanganywa na kuuziwa mbegu za kambale kutoka mto ruvu. Kwa sababu wanauziwa wakiwa ni wadogo, basi ni vigumu kwao kugundua kuwa ile mbegu zimechanganyika aina tofauti.

Katika mito kuna aina nyingi sana za kambale. Kwa mfano, Kuna wale "clarias gariepinus" kambale wa mabaka mabaka, hawa ndyo wanafaa kwa ufugaji.kuna wale "Mumi au clarias hetrobruchus "

a1dfd8e49147ff039c45c6614140f69f.jpg

26f4cc360350d6c4120d76c4efb04455.jpg
65f20055ca47a399c540c3b9242ab843.jpg
Hawa ni weusi na wana vichwa vikubwa, si wazuri kwa kufuga sababu wanakulana sana hasa mabwawani. Ila wanakuwa kwa haraka sana na wanapendelea live feeds ndyo maana hulana sana. Wanauwezo wa kufika 15kg ndani ya miez 9 wanapolishwaa vizuri. Tatizo lao ni kulana na wanahitaji space kubwa wanapokuwa bwawani.

"Neke au Clarias batrachus "
0e2498b2a099de97ce796058ebf8e2c7.jpg

Hawa hata umfuge miaka 20 hafikishi hata 200g). Sasa hawa wakiwa wadogo kwa mtu ambye si mtaalamu hawezi watambua. Utawafuga ila mwisho wa siku unakuta unavuna chini ya 30% sababu walikulana na wengine ni wadogo sana.

3. WATAALAMU MATAPELI
Hiki ndicho kilio cha wafugaji wengi hapa Tanzania. Wengi wamekuwa wakilalamikia watu wanaojiita wataalamu waliowatumia kipindi wanaanza ufugaji samaki. Hii hata mimi binafsi ilinicost wakati ninaanza. Mara nyingi nilikuwa nafikiri wale waliosomea uvuvi na ufugaji wa samaki ndyo wataalamu. Ila cha kushangaza unakuta hamiliki hata bwawa lolote la samaki kutwa kuibia watu na kujiita mtaalamu.

Simaanishi wote ni matapeli, wengi wamekuwa wakitumia Utaalamu uchwara kuibia watu. Mfugaji anapewa ushauri wa hovyoo mwisho wa siku wanafail.

Wengine ni kweli wataalamu ila wanatanguliza pesa mbele bila kujari mafanikio ya mfugaji. Kwa mfano;
Unakuta mtaalamu anamshauri mkulima kufanya overstocking ( kuweka samaki wengi katika sehem ndogo) imradi amuuzie tu mbegu nyingi ili apate faida. Kuna sehem nilifika nakushangaa. Bwawa la 50m square, mkulima kaweka kambale 20,000. Maana yake kila mita square kuna kambale 400!! Hapa ndipo mwisho wa siku mkulima anafuga kwa muda mrefu anakuja vuna samaki wasiokuwa na ukubwa wa kutosha na wakati mwingine hata idadi inakuwa ndogo sana.

4. CHAKULA BORA CHA SAMAKI NA GHARAMA ZAKE

Chakula kimekuwa changamoto kubwa kwa wakulima wengi. Kusema ukweli gharama za kulisha samaki zipo juu sana kma mfugaji hatakuwa mbunifu katika kubudget na kuandaa chakula cha samaki.

Unakuta mkulima anashauriwa kununua chakula cha samaki 3000 had 4000 kwa 1kg wakati mwingine anajitengenezea kwa gharama isiyozidi 1000 kwa 1kg. (wiki ijayo ntapost njia ya mkulima kuweza kujitengenezea chakula kwa gharama nafuu)

Hii imewasababisha wakulima wengi kujikuta wametumia gharama nyingi na kukatika mitaji kabla ya kufika muda wa kuvuna.

5. KUKOSA MPANGO KAZI WA BIASHARA NA KUTUNZA TAKWIMU
Ufugaji samaki ni biashara kama biashara nyingine. Kama mfugaji anahitaji kufuga samaki kibiashara, ni lazima awe na Investment Plan. Mara nyingi wengi wakipigiwa hesabu za mezani na kuona faida kubwa, wanakimbilia kujenga mabwawa makubwa au mengi na kununua vifrang wengi bila kuelewa kuwa 70% ya investment katika ufugaji ni chakula.
Ile miezi ya mwanzoni atamudu kuwalisha ila baada ya hapo wengi hushindwa maana gharama za ulishaji huwa kubwa zaidi. Na wengine hujikuta wameshindwa au kuacha kabisa kuwalisha wakifikiri kuwa wataendelea kukuwa sababu tu wapo kwenye maji.
452dfb03a817fd086e905504f1b09a82.jpg

Pia mali bila daftari huisha bira habari. Mfugaji anapofanya uzembe kuweka records za matumizi na mapato katika ufugaji, pia anajitengenezea mazingira ya kufail.

6. Kuto kuwapanga (Sorting) samaki

Hili nalo ni Tatizo kubwa linalowakumba wafugaji. Wengi wanafikiri samaki wakiwa kwenye bwawa na kulishwa ndyo ufugaji wa samaki unaishia hapo.

Sorting ni muhimu sana kwa samaki. Mara nyingi samaki bwawani hawawezi kukuwa kwa kulingana hasa kambale. Ni lazima watatofautiane tu. Na wanapotofautiana kwa ukubwa inamaana, kutakuwa na group la samaki wababe na wanyonge. Hawa wababe ndyo wanaopata chakula na kukuwa haraka, wanyonge ukuhaji wao huwa ni duni na wasipotenganishwa hudumaa. Na wanaodumaa kwa kambale huweza kuliwa na wale walio wakubwa.

be390f925eb02fe000f135d5812446e8.jpg
Mfugaji anashauriwa kuliko kuwa na bwawa kubwa moja, ni bora aligawe mara mbili ili baada ya muda aweze kuwasort samaki katika magroup angalau mawili hadi matatu.

7. SOKO.
Soko la samaki si tatizo hapa Tanzania. Samaki wanademand kubwa na inaongezeka kila siku sababu ya watu kuzidi kupata elimu juu ya faida ya ulaji wa samaki.

Tatizo linakuja pale mkulima anapotafta soko pale muda unapokuwa umefika wa kuvuna. Hapa wengi unakuta wanaacha kulisha samaki na kuangaika na soko bila kujua wale samaki wakiachwa bila kulishwa, hupungua uzito waliokuwa wameshafikia. Ni muhim mfugaji kuplan mapema na kutafta soko mapema kabla ya kufika muda wa kuvuna.

Mambo 10 mfugaji ni lazima ayazingatie

1. Hakikisha unanunua mbegu bora, isiyokuwa na magonjwa na kutoka kituo cha uzalishaji kinachoaminika. Hapa mkulima unahitaji ufanye reseach mwenyewe ujihakikishie.

16a0de7b09110926794ee9fe5f6c2d9d.jpg

2. Usiweke samaki wengi katika bwawa ( Overcrowding)

3. Hakikisha condition za maji ni salama na zinazotakiwa. Vipo vifaa visivyokuwa na gharama unaweza nunua kuweza kupima pH ya maji, oxygen, ammonia, etc

cf8bf3ebe275abf20e6d881d22380aca.jpg

4. Hakikisha mazingira ya bwawa yapo salama na hakuna wanyama, wadudu na ndege wanaokula samaki. Ni vizuri kuzungusha fance na kufunika kwa net ili bwawa liwe salama zaidi.

caeacf6d1510835d5511a9b42ac58227.jpg

5. Hakikisha samaki wanalishwa chakula bora na kwa kiwango kinachotakiwa. Usilishe sana ili kuavoid kuchafua bwawa na usilishe kidogo ili usije wadumaza.

6. Kuwa na Ratiba maalumu ya muda wa kuwalisha. Pamoja na sehem maalumu ya kuwalishia katika bwawa.

7. Chunguza samaki wako tabia zao za kula na jinsi wanavyotembea bwawani. Hii itakusaidia kujua afya yao.

8. Fanya Sorting angalau kila baada ya miez mitatu.

9. Tafta soko mapema kabla ya kukaribia kuvuna.

10. Tunza kumbukumbu.

Itaendelea...



Updated 23/12/2017
SUCCESS IS NOT ABOUT WHAT YOU GET, IT'S ABOUT WHAT YOU GIVE.

Nipo free kwa mtu yeyote kunitafta kama unauhitaji wa elimu zaidi katika ufugaji wa samaki. Sina charges zozote. 0759741303, whatsup or Call.

Unakaribishwa katika Group letu la whatsup ambalo tunatoa mafunzo ya kitaalamu juu ya ufugaji wa samaki, mbegu, chakula na msoko.

UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA
 
Biashara hii n nzur sana ila inahtaj ufanye kaz bega kwa bega na wataalamu wa masail haya ...na hilo wamekuwa wakilisisitiza ....kuhudhuria semina mbalimbali pia mtu utagain knowledge
 
Eneo linatakiwa liwe na ukubwa gani?
Bwawa linauwezo WA kugharimu sh ngapi?
 
Eneo linatakiwa liwe na ukubwa gani?
Bwawa linauwezo WA kugharimu sh ngapi?
Mkuu hii inadepend na kiasi cha samaki unachotaka jufuga, upatikanaji wa maji. Aina ya samaki, na aina ya ufugaji unaotaka kufanya.

Post yangu ijayo itazungumzia maandalizi ya bwawa na aina ya ufugaji.
 
Hongera na ubarikiwe sana ndugu.

Huu ndio uzalendo.

Tumepata elimu nzuri ya ufugaji.
Nasubiri sshemu ya pili yke. Swali langu,je unahitaji mtaji kiasi gani kufuga kambare 2000 mpaka unavuna?
 
Uko vizuri sana mkuu, hongera kwa kuamua kushea uzoefu wako hapa jukwaani. Kila LA heri katika utafutaji wako.
 
Back
Top Bottom