CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 6,999
- 23,395
Huwa nawambiaga watu mimi nikitaka kuanzisha biashara hiyo unayoifanya wewe (unaesoma hii post) hiyo biashara ambayo unaona hailipi haina faida eneo hilo hilo nina uwezo wakupata faida,si kwasababu nina uhakika wa wateja ila nimeshajua kwanini wateja hupati.
Unajua biashara inapoelekea kufa au kufilisika wengi hawataki jiuliza maswali ya msingi ya kwanini biashara yake imekufa wakati miezi ya mwanzo au mwaka wa mwanzo ilikua ikimlipa sana tu,kwann leo ife?
Kwamba unataka kusema hapo ulipo watu hamna tena au barabara imebadilishwa au nyumba za watu zimehamishwa,nk unataka kusemaje labda? si kweli huna la kujitetea ila kuna excuse unajipa ili nafsi yako iridhike kweli biashara hii haifai. Unajipa majibu yale moyo wako unayataka.
Acha niwambie kitu leo,sababu kubwa inayofanya biashara nyingi kufa ni BEI, hiii ndio sababu nambari 1 inayosababisha biashara nyingi kufa, Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini wenye maduka ya nguo,viatu,sijui takataka gani ilimradi ni bidhaa waliopo pale kariakoo vitu vyao vinatoka CHINA?
Umeshawahi jiuliza kwanini kila mfanyabiashara wa hapa Tanzania mtaji ukikua tu anawaza kwenda kufata mzigo wake china? kwanini CHINA? na sio America? kwani marekani au mataifa mengine hayauzi TV au hayauzi Simu au hayauzi Viatu na nguo?
Hapana si kweli kwamba china tu ndio ina kila kitu,ila unajua kwanini CHINA? kwasababu ya BEI,china hawana bidhaa za gharama hata kama zipo ila si bei kulinganisha na mataifa mengine. kwahiyo Tunakubaliana kwamba BEI ndio sababu kubwa ya kufanya biashara/huduma yako kufa.
Umeshawahi jiuliza kwanini maduka ya mikoani yana agiza bidhaa zao za jumla kariakoo? kwamba soko lenye mazaga zaga yote n kariakoo tu au? Hapana si kweli ila jibu ni kwamba Wana opt kariakoo kwasababu BEI ya bidhaa za kariakoo ni simple kuliko akiagiza pale kampala au nairobi,nk
Ukishamjua mchawi wako ni rahisi kumpiga maombi mpaka amrudie Mungu, tushamjua mchawi katika biashara zetu ni BEI je tufanye nini sasa ili tutoboe tuvuke hiki kiunzi kilicho mbele yetu?
SHUSHA BEI
Hapa ndio utakumbuka nilishatoaga somo la kujitangaza,sasa apply ile formula washa spika lako tangaza kuwa bei imeshuka,fanya unavyoweza wajulishe wateja wako bei imeshuka na sio kama ilivyokua mwanzo.
kama ni saloon ulikua unanyoa raia 1500 na walikua hawaji watangazie wambie bei imeshuka watolee 500 wanyoe kwa BUKU,kama n mam ntilie ulikua ukiuza chakula 2500 watolee buku wambie sasa ni 1500, shusha bei ya Vunja Vunja bei kila area,fanya kama unataka kusafisha duka ulete mzigo mpya Piga promo za maana wambie BEI imeshuka sawa na bure.
ACHA TAMAA
Kuna wafanyabiashara wana tamaaa,kwakua wateja wataaanza kurudi kwasababu bei imeshuka ataanza kuleta tamaa kuna wateja watakuja wakidhani bei ni ile ile so atatoa 2500 kwasababu kazoea wali ni 2500,wafanyabiashara wenye tamaa hawarudshi chenchi wanafinya kimya kimya (acha hiyo tabia) umeshasema bei imepungua wakija wateja waliodhani bei n kama mwanzo wakilipa pesa ya mwanzo Rudisha chenchi ya mteja.
Wambie na wafanyakazi wako maana hapa ndio wafanyakazi hujichukulia point za ushindi,wambie ukigundua kuna mfanyakazi analipsha wateja bei ya zamani Hauna ONYO bali ni unamfukuza na Fukuza kweli ''kuwa serious" Simamia kauli zako na asitokee wa kupindisha.
Nakuhakikishia utafanya biashara, tujifunze kupitia makampuni makubwa kina PEPSI na COCACOLA hawa majamaa wa coca zamani walikua wanajiona soda zao ni tamu kuliko wenzao eti wakawa wanauza 600 wenzao pepsi soda 500, coca yalipowafika shingoni wakaanza na wao kuuza 500 matokeo yake sasa hivi mnaona coca inanyweka pepsi inanyweka,ki sh 100 tu kimeondolewa Wateja haoooooo..
nawewe kwenye biashara yako punguza bei kata kutoka bei ya mwanzo wape bei mpya,utaona mvua itayofurika,mimi ni nshahidi nimesha apply hii formula imeokoa biashara zangu nyingi sana zilizokua zinapumulia oxygen.
Hii formula kui apply inahtaji uwe umefatilia lile somo la kujua wapi bidhaa unayouza inapatikana
kama wewe ulikua na urafiki na middle man hii formula kui apply utapata tabu sana maana unashushaje bei wakati middle man anakuuzia kitu bei ya juuu? aseee middle man anakufelisha leo ila kama ulikua unafata vitu vyako direct toka vitokapo apply hii formula utanishukuru siku 1.
BEI BEI BEI achana na bei za marekani achana na BEI za M/City achana na Bei za KFC hapa ni TANZANIA weka bei za kitanzania,tunatembelea magari ila mifukoni tuna buku jero ya lunch,usinione na gari ukafkiri ntaenda kula kfc,tumepanga nyumba za gharama ila tunaendaga kunyoa saloon za buku buku,usifkiri utakaa unikute nanyoa cutting master... kwenye biashara yako siri ni BEI kuwa makini na hilo eneo,acha kukariri eti chapati wanauza 500 na wewe uuze 500, uza chapati 250 kwa jero mtu ale chapati mbili uone kama hutouza.
Kusanya faida ndogo ndogo kila siku uwe na uhakika kuliko kutegemea faida kubwa halafu ukose kabisa,Nasema hiviiii ni Bora 200 ya uhakika kuliko Buku la kubahatisha.
AM OUT.

Ongeza faida kwenye biashara yako kwa kumkwepa middle man
Maisha ya biashara na ujasiriamali kila unapoamka inapaswa upashe akili moto kuongeza ile 500 uliyoipata jana leo upate 1000 na kesho kutwa upate 1500 Hiyo ndio inatwa biashara na ujasiriamali. Leo nataka kuandika kitu kidogo chakufungulia mwaka kuamsha waliolala,na jambo lingine leo nataka...
www.jamiiforums.com