Biashara noma sanaa, unataka kujiona hufanyi kitu kwenye biashara? Ingia Instagram cheki biashara za wenzako..!!!

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
6,764
15,888
INTRODUCTION:-
Wananchi salamaa?
Wale wanayanga wenzangu tusijali TUTAVUKA BILA CALUCULATOR zao..!!!

BODY:-
Ukiachana na utumishi wa umma, Mimi bwana ni mfanyabiashara ninaye miliki kampuni inayofanya biashara aina tatu tofauti.

Ashukuriwe Mungu mauzo kwa siku hayawi chini ya Mil 2 kama siku ikiwa mbaya na siku ikinoga yanaenda mpaka mil 7 kwa siku..!!!

SCENARIO:-
Baada ya biashara zangu kuwa kubwa na jina kufahamika, nilishauriwa niingie Social media ili kuitangaza zaidi.

Hivyo nikafungua Page Instagram, Twitter (X) na Facebook.

Kwenye kulipia ads niligoma, hivyo naendesha pages ambazo hazijalipiwa.

Sasa bwana mwenzenu ninapopata nafasi huwa natembelea pages za watu kujifunza vitu mbalimbali, sasa nayokutana nayo huko sometimes yanasononesha moyo na kutia maudhi na kujiona badoooo sanaaa kwenye biashara .....

1. Raia wanaagiza bidhaa kwenye kontena.
Sijawahi agiza bidhaa likajaa kontena, uwezo wangu huwa ni fuso tu.
Hivyo dah nikiwacheki wa insta na makontena yao yaani dah..!!!

2. Raia wana maduka/fremu zimelembwa.
Unakuta duka la mtu lina mataa mataaa hatari mpaka kunoga..!!
Yaani duka ukiliangalia kwenye kioo cha simu linavutia noma.

3. Raia wanatumia wasanii na watu mashuhuri kufanya promo.
Ukiingia insta unakutana na wenzako (hasa wa Dar) wanatumia wasanii wa bongo fleva na watu mashuhuri kwenye matangazo yao.
Kuna siku niliona jamaa anafanya biashara kama yangu mkoani anamtumia Hamed Ally wa Simba kufanya promo..!!!

4. Raia maduka yao yanajaaa wateja.
Ndio hata mimi nauza, ila naonaga insta unakuta duka limevamiwa na wateja kama anagawa bure.
Yaani kama huna moyo halafu akawa ndio mpinzani wako wa "same location" lazima uzimie..!!!

5. Raia wana wafanyakazi kibaoo.
Kuna siku niko na view ad ya jamaa mmoja anafanyabiashara kama yangu, nakuta anawafanyakazi kibao (nilihesababu wakafika 9) wotee wako bizeee na wanasale zao freshh.
Huku kwangu kampuni yangu ina vijana wa 4 tu tunalisongesha.

6 .... N.k utamalizia na wewe.

CONCLUSION:-
Wazee wa Insta mnatutisha wenzenu..!!!

Anyway:-
Business is better than investment.
Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Deal chafu nyingi kwenye biashara , biashara ina mbinu nyingi mno , hayo makontena anayosema wengine washadaka uwakala , wao mizigo hutumwa Tu hawajaweka hata mia yao , wanauza wanabaki na cha juu ndio michezo ya kariakoo,
Nadhani unajua vingi vya k.koo
Tuunganishe basi na wa mikoani na sisi" "tubaki na cha juu iwe michezo yetu mikoani""

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Mkuu kuhusu mienendo ya wenzio isi kupe wasiwasi au morali ya kufanya Kama wanavyo fanya wao.

Kwani Kuna msemo una sema 'jikune uwezavyo", kwani kila mtu ana kimvuli chake, kwa urefu wake na hata upana wake.

Kikubwa tazama biashara yako kwa makini, uone Kama Kuna sehemu ya kuboresha, kurekebisha au hata kuongeza ili uji kuze.
 
Mbona hapa jf hutangazi!?
Anyway kifupi we na wenzako ni matajiri ila jua yote mtayaacha hapa hapa duniani
we Jamaa ume ni chekesha sana, ni sawa wata acha duniani, ila huko unapo kuwazia ume paona??.

angalau tutengeneze Pepo yetu hapa, ili hata tusipo ikuta tusi lalamike.
We huoni soni mwanao ana enda shule na madumu Kama machinga??
 
Naweza nikawa nje ya mada ama sahihi

Kipindi nikiwa kwenye kampuni x kabla haija stop operation zake.....

Ilikuwa ni kampuni ya pharmaceuticals na ilikuwa inaagiza dawa kutoka uchina .......

Maake hapo naona umesema pia una kampuni na una wafanyakazi wanne.....

Basi ile kampuni ukimweka MD, MIMI, WATU WA SALES 3, MLINZI KAAJIRIWA NA KAMPUNI YAKE SO SIMWEKI HAPO...

Tulikuwa watu watano tuu...... Mtaji wake ulikuwa mkubwa kwakweli japo mwanzoni alikuwa mbishi mpaka ajisikie ndo aruhusu oda....

Mimi nikawa naichukulia biznez kama yangu ikitokea odaa hata hajaruhusu namwambia mteja aingize pesa kwenye account ya kampuni then mm ni deal na MD,

Biashara ukiichek Haina matangazo sijui insta wala Facebook.... Ila nilikuwa nikisimamia shoo kwa siku hata mio 20 tunauza nikishirikiana na watu wa sales....

Na mtaji wake unasoma parefu kuleta dawa maake alikuwa anashusha 40ft container

Naamini hata wewe mkuu usife moyo utafika wakati unashusha container tuu ...... na kufanya kile unachotaka kwenye biashara yako mkuu....

Kila la khery
 
Ukweli social media watu wanauza sana

Sasa kuna tiktok huko balaaa, wanafungua mizigo watu wa nanunua live na delivery inaendelea wakiwa hewani

Ndio maisha na rahisi kwa wengi

Ten alive za jioni hadi kama tatu usiku wanawake wapo kazini.

Hapo viewers mara nyingi naonaga nearly 200 ipo lazima na wakati mwingine inazidi.

Jiongeze utafika zaidi, kuwa mwanimifu na delivery men was iwe wa tamaa ya pesa kuchaji usafiri
 
INTRODUCTION:-
Wananchi salamaa?
Wale wanayanga wenzangu tusijali TUTAVUKA BILA CALUCULATOR zao..!!!

BODY:-
Ukiachana na utumishi wa umma, Mimi bwana ni mfanyabiashara ninaye miliki kampuni inayofanya biashara aina tatu tofauti.

Ashukuriwe Mungu mauzo kwa siku hayawi chini ya Mil 2 kama siku ikiwa mbaya na siku ikinoga yanaenda mpaka mil 7 kwa siku..!!!

SCENARIO:-
Baada ya biashara zangu kuwa kubwa na jina kufahamika, nilishauriwa niingie Social media ili kuitangaza zaidi.

Hivyo nikafungua Page Instagram, Twitter (X) na Facebook.

Kwenye kulipia ads niligoma, hivyo naendesha pages ambazo hazijalipiwa.

Sasa bwana mwenzenu ninapopata nafasi huwa natembelea pages za watu kujifunza vitu mbalimbali, sasa nayokutana nayo huko sometimes yanasononesha moyo na kutia maudhi na kujiona badoooo sanaaa kwenye biashara .....

1. Raia wanaagiza bidhaa kwenye kontena.
Sijawahi agiza bidhaa likajaa kontena, uwezo wangu huwa ni fuso tu.
Hivyo dah nikiwacheki wa insta na makontena yao yaani dah..!!!

2. Raia wana maduka/fremu zimelembwa.
Unakuta duka la mtu lina mataa mataaa hatari mpaka kunoga..!!
Yaani duka ukiliangalia kwenye kioo cha simu linavutia noma.

3. Raia wanatumia wasanii na watu mashuhuri kufanya promo.
Ukiingia insta unakutana na wenzako (hasa wa Dar) wanatumia wasanii wa bongo fleva na watu mashuhuri kwenye matangazo yao.
Kuna siku niliona jamaa anafanya biashara kama yangu mkoani anamtumia Hamed Ally wa Simba kufanya promo..!!!

4. Raia maduka yao yanajaaa wateja.
Ndio hata mimi nauza, ila naonaga insta unakuta duka limevamiwa na wateja kama anagawa bure.
Yaani kama huna moyo halafu akawa ndio mpinzani wako wa "same location" lazima uzimie..!!!

5. Raia wana wafanyakazi kibaoo.
Kuna siku niko na view ad ya jamaa mmoja anafanyabiashara kama yangu, nakuta anawafanyakazi kibao (nilihesababu wakafika 9) wotee wako bizeee na wanasale zao freshh.
Huku kwangu kampuni yangu ina vijana wa 4 tu tunalisongesha.

6 .... N.k utamalizia na wewe.

CONCLUSION:-
Wazee wa Insta mnatutisha wenzenu..!!!

Anyway:-
Business is better than investment.
Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Kuna Siri nyingi watu wamebeba tuangalie tu 😜
 
we Jamaa ume ni chekesha sana, ni sawa wata acha duniani, ila huko unapo kuwazia ume paona??.

angalau tutengeneze Pepo yetu hapa, ili hata tusipo ikuta tusi lalamike.
We huoni soni mwanao ana enda shule na madumu Kama machinga??
Ni kuchangamsha mada wote tuko tunapambana ila kupata pepo ukiwa duniani ni ngumu sana mkuu
Sikiliza "holes"ya passenger utanielewa
 
Back
Top Bottom