Biashara - faida pande zote kwako na kwangu ndani ya miezi mitatu

DOKEZO

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
322
496
Habari,

Iko hivi: Nina gari yangu Toyota Wish ambayo nimekuwa nikiitumia katika biashara ya Taxi mtandao( Uber,Bolt,Ping,Tantaxi,Little ride).

Nilipata changamoto ya ghafla ya kifamilia na sikuwa na akiba ya pesa ikabidi niweke bondi hiyo gari.Gari inadaiwa Tsh 1,600,000/=.Nimepambana kuigomboa ili iendelee na kazi mpaka sasa nimekwama.

Biashara itakavyokuwa:
Kwa yeyote atakayekuwa na hiyo pesa kuigomboa hiyo gari

(1)Kwanza katika kuweka uaminifu,makubaliano yote tutakayokubaliana tutaandikishiana katika mamlaka husika za kisheria mf. Polisi,kwa mwanasheria,mahakamani.Popote pale muhusika atakapotaka.

(2)Pili kwa kutoa kiasi hicho cha pesa 1.6m utapata faida ya Tsh 560,000 ndani ya miezi mitatu.
*Faida hiyo utaipata kwa kila siku utalipwa hesabu ya Tsh30,000/= siku 6 za wiki ndani ya miezi mitatu (wiki 12).

(3)Baada ya miezi mitatu mkataba au makubaliano hayo yanamalizika. Na hapo ndipo nafaidika kwa kumaliza mkataba au makubaliano hayo.

Muhimu:
*Masharti yoyote utakayoyataka wewe kwa asilimia kubwa yatazingatiwa.

Nakaribisha maswali lakini kubwa zaidi YEYOTE MWENYE UTAYARI NAMKARIBISHA NA NITAMSHUKURU SANA

MREJESHO
Habari za leo wakuu. Naomba nitoe mrejesho kuhusu hili jambo langu kuwa tayari nimeshafanikiwa kumpata mtu ambae tumekamilisha zoezi lote. Ahsanteni wote ambao mmenipa ushirikiano wenu.
 
Nilichogundua ni kwamba watu wengi tunaokopesha kwa bondi, tukiona mteja kaleta bondi yenye thamani mfano gari, nyumba ama kiwanja, huwa tunaroga ili mteja asifanikiwe kulipa deni tubebe bondi🥵🥵🥵

Japo mimi sifanyi hivyo🙏🙏
 
Nilichogundua ni kwamba watu wengi tunaokopesha kwa bondi, tukiona mteja kaleta bondi yenye thamani mfano gari, nyumba ama kiwanja, huwa tunaroga ili mteja asifanikiwe kulipa deni tubebe bondi🥵🥵🥵

Japo mimi sifanyi hivyo🙏🙏
Kama una namna ya kunisaidia nikaokoa gari yangu nakukaribisha kwa mikono miwili mkuu. Nicheki PM
 
Kwa nini usiuze tu gari ujipange tena, naona kama unajipeleka kwenye shida zaidi.
 
Back
Top Bottom