Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 20,571
- 22,490
Ni wazi chairman na msaidizi wake Taifa hawana tena mawazo mapya wala fikra mbdala kuiongoza chadema ikapiga hatua au kufanikisha chochote kisiasa.
Taasisi imekuwa haina mipango mikakati endelevu, sera mbdala, dira wala uelekeo muafaka unao eleweka na wenye kuleta matumaini au ahueni ya kufika mahali fulani kwa wanachadema au hata wananchi kwa ujumla.
CHADEMA haina ushawishi kabisa wa kisera na wala haina mvuto tena wa kisiasa ukilinganisha na hapo awali. Inasikitisha sana viongozi wake wamefikia ukomo wa fikra mpya na mawazo mbadala kiasi kwamba, hivi sasa Chadema inaongozwa kwa mihemko, hisia na huruma za wananchi tu.Just imagine eti ndio inataka uongozi wa nchi.
Nilio wapendekeza, jipangeni vizuri, fanyeni tafiti nyingi sana za kina, kusanyeni maoni na mitazamo mahususi mbalimbali ya wananchi, zingatieni ushauri wa majopo ya wataalamu na wabobevu wa kiuchumi, kijamii, kisiasa, kitaifa na kimatafa, na kwa hakika mtafanikiwa kuyafikia malengo yenu kwa uhakika zaidi na hakuna haja ya kujakunishukuru 🐒
Mungu Ibariki Tanzania