Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,567
- 158,296
Wasafi Media imemtafuta Beno Kakolanya na kutaka kujua undani wa taarifa hizo na ameeleza kuwa hajatoroka kambini bali alitoa taarifa kwa meneja wa timu na kuruhusiwa.
“Nilimpa taarifa Meneja kuwa nimepata tatizo na ilikuwa ni siku ya Alhamisi na ilitakiwa niondoke usiku huo huo nikaondoka usiku huo.
“Aliyewapa maelekezo anajua ana maana gani waseme hivyo pia niliyempa taarifa naye kafikishaje ujumbe swali lipo hapo.
“Ila kwakuwa wamenichafua Sana ngoja wanipe ushahidi nimehujumu wapi timu,” amesema Kakolanya.