Benki Kuu (BoT): Hatujatoa leseni wala kuruhusu shughuli za LBL

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
790
1,669
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapenda kuutaarifu Umma kuwa haijafanya mazungumzo wala kutoa maelekezo yoyote ya kupewa leseni au kuruhusiwa kwa kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL), tofauti na taarifa mbalimbali zinazozambaa mitandaoni.

Soma Pia: Jeshi la Polisi Morogoro lawakamata maofisa saba wa LBL kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha


Hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa kampuni ya LBL kwa kujihusisha na ulaghai ikiwemo kupokea amana, kutoa riba na kufanya uhaulishaji wa fedha bila leseni ya Benki Kuu ya Tanzania.

Screenshot 2025-02-24 215355.png
 
Mbongo kwa ubunifu wa uharibifu au fursa humuwezi naona Pana platforms kibao wabongo wameanzisha zenye mfumo wa kuperform task za kuangalia video ili ulipwe kama ilivyokuwa lbl huku wakishawishiwa watu wajiunge.

Pigeni pesa at your own risk mwanzoni mwanzoni hela yako ikirudi achana nao na always hizi PONZI PYRAMID SCHEME wa mwanzoni ndo wanawaini wa mwishoni ni kilio.

Sema maisha kila kitu ni risk nashukuru hela yangu LbL lilirudi mapema.

Wabongo wazee wa shortcut,zipo kibao kwa majina tofauti tofauti zimefunguliwa kwa kasi ni wewe tu uchague upigwe ipi zimejaa kama zile za betting.
 
Back
Top Bottom