Mwaka 2019 benki kuu ya Tanzania Ilitengeneza kanuni za kuwalinda walaji wa huduma ndogo za fedha zikiitwa BANK OF TANZANIA FINANCIAL CONSUMER PROTECTION REGULATION,GN 884 2019, lengo la kanuni hizi ni kumlinda mteja wa huduma za fedha kama tigopesa, mpesa . N.k
Kanuni hizi zinamtaka mlaji anapokuwa na malalamiko dhidi ya mtoa huduma basi hatua ya kwanza anatakiwa kuwasilisha malalamiko husika kwa mtoa huduma wake, zikipita siku 14 mtoa huduma hajashughulikia au kujibu basi itambidi kuwasilisha malalamiko dawati la malalamiko benki kuu ya tanzania, ambapo malalamiko hayo yatashughulikiwa ndani ya siku 45. Kama mlaji hataridhishwa na uamuzi wa dawati basi itamlazimu kuomba REVISION kwa gavana wa benki kuu.
Mwezi wa tano mwaka huu tigo pesa walinikata pesa kwenye account yangu kiasi cha shilingi 118,000/= , ambapo baada ya kukata pesa hiyo niliwaandikia tigo kuwalalamikia, lakini tigo hawakujibu. Malalamiko yalijikita kwenye mambo mawili, kurudisha hela yangu, lakini pia kunifidia hasara waliyonisababishia kulingana na ushahidi niliowasilisha kwao. Tigo walirejesha hela baada ya kusumbuana sana ila issue ya fidia hawakutaka kujibu.
Ilinilazimu kuzingatia kanuni na kuwasilisha malalamiko benki kuu, kwa kuwa kanuni zinataka kufanya hivyo na ukienda kinyume kufungua kesi mahakamani moja kwa moja unakutana na mapingamizi. (Preliminary objections) badala benki kuu wasikilize malalamiko na kutoa uamuzi, (determination) wao wanatoa maoni na ushauri kinyume kabisa na kanuni ambazo wao ni regulator.
Kwenye kanuni hakuna mahali ambapo benki kuu wana wajibu wa kutoa ushauri na maoni. Wajibu wao ni kupokea, kusikiliza na kutoa uamuzi wa malalamiko kwa mujibu wa kanuni.
Mh gavana naomba utupie jicho dawati la malalamiko la benki kuu kuna namna wanawalinda watoa huduma kuwajibika kwa walaji kwa matatizo wanayotusababishia.