The August
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,080
- 2,026
Ni jumatatu yenye hangover ya weekend. Basi lets talk about Music. Good Music.. Rhumba & seben Music.
Kutoka miaka ya 1990 jamii ya Tanzania katika anga la Burudani, muziki wa dansi (nikimaanisha Rhumba na Seben) ulishika sana hatam. Iwe ni maharusini, disco na maredioni nyimbo kama Kalay Boeing yao vijana warembo na watanashati (Wenge Musica) hadi Solola Bien miaka ya 2000 mwanzoni zilitamba sana. Miaka ya 2000 huku kwetu bendi kama Tam Tam yake Mwinjuma Muumini, Twanga Pepeta Chini ya choki na banza stone, FM Academia chini ya kina Malou stonch, Marehem ndanda kosovo kichaa, Patcho mwamba na hata stono musica na kisha kuibuka Mashujaa band. Bado nyakati hizi muziki wa dansi ulitamba sana.
Kuibuka kwa band ya Akudo miaka ya 2007 chini ya Christian Bella kuliibadilisha sana sura muziki wa dansi na kuleta ushindani mkubwa kwa Twanga na Fm Academia. Nyimbo kama Yako wapi mapenzi na Safari sio kifo, zilitikisa anga la muziki wa dansi..
Kushamiri na uwekezaji mkubwa uliofanywa na wanamuziki wa Bongo Flava. Kuliipa dhoruba kubwa muziki wa dansi. Muziki huu ukadidimia sana nchini.. Nyimbo hizi zikawa zinapigwa bar tu. Tena bar chache. Nazo bendi zilizokuwa zinapiga muziki huu ikafika mahala wakaanza kupiga kwenye mabar huku kiingilio kikiwa ni chupa ya bia tu. (HAKIKA NI NYAKATI MBAYA KABISA KATIKA MUZIKI WA DANSI).
Kuanzia mwaka jana, kumekuwa na hamasa na kampeni kubwa sana ya kuhamasisha au kuhuisha muziki wa dansi.
Kampeni hii imehusisha maeneo makubwa hasa matatu.
Moja, ni kutoa kwa nyimbo mpya. Katika eneo hili, mwaka juzi baada ya gawanyiko la band ya FM Academia, Rais Patcho mwamba alianzisha band yake. Bamd hii iitwayo Bogoss Musica ilizinduliwa mwaka jana na kutoa wimbo ulio maarufu kabisa na kuleta sura mpya muziki wa dansi.
Band hii ilikuwa na 75 % sura na damu mpya katika muziki wa dansi. Mathalani mwanamuziki Kelly Hustle naye mwaka huu akaachia nyimbo mpya iitwayo Come Back.
Bado mwaka jana na huu umeshuhudia utoaji wa nyimbo mpya kadhaa.
Mkali Jimmy Manzaka baada ya kutoka na Coco Chanel...
..
Siku kadhaa ameachia nyimbo hii iitwayo Chozi langu..
Papii kocha naye akishirikiana na bwana mdogo mwenye sauti ya kipekee, Melody mbasa nao wakatoa nyimbo iitwayo upepo.. Nayo ni rhumba yenye vionjo vilivyopikwa kiufundi haswa.
Ukiwa mkoani Arusha, unaweza pata muziki mzuri wa band kutoka bendi iitwayo Mjengoni classic band.
Hakika muitikio wa kutoa nyimbo mpya umekuwa ni mkubwa.
Hatua ya pili ni uchezwaji wa nyimbo hizi kwenye vyombo vya habari.
Ni hatua ya kupongezwa kuwa muitikio sio mbaya.. Wapo watangazaji wengi wamefanya vyema kuupigania muziki huu.
Mathalani.
Sunday mwakanosya na Ben Kinyaiya katika Channel Ten na Magic fm wanaufanyia haki muziki huu.
Dakota de lavida a.k.a Abdacadabra huwezi acha thamini mchango wake. Kipindi cha Mama land cha Clouds TV na pia weekend bonanza cha Clouds FM. Pia ana program yake ya Buzuki Time ambayo anafanya kipindi kutokea bar fulani. Hii inaweka ufaham mtaani juu ya kipindi na muziki wa dansi.
Irene Gabriel. Mwanadada huyu kupitia radio uhuru hakika anawapa nafasi muziki wa dansi.
Zuhuru mwinyi yuko active na mwepesi kutoa nafasi kwa wanamuziki wa dansi.
Benard James.. Kwa upekee kabisa, Ben james amastahili pongezi na pia somo moja kutoka kwake napenda watangazaji wengine wamuige. Anafanya vipindi viwili maarufu sana. Anaongoza kipindi kiitwacho Afrika kabisa kupitia kituo cha Star Tv na Tanzania Stars cha RFA. Jambo moja la kipekee ni kanuni yake ni kucheza kwa 95% nyimbo mpya tu katika vipindi vyake.
Hii inatoa nafasi kwa nyimbo mpya kucheza, hamasa kwa watu kutoa nyimbo, na muhimu kabisa kuutangaza muziki huu.
Ni ajabu kukuta kipindi cha muziki wa dansi unasikia nyimbo za kina Gato, Tabu Ley, Fally ipupa Associe, Fere Gola Mercure, FM Academia Vuta N kuvute. Hakika njia hii haikuzi muziki kabisa.
Kwa hili ninaomba sana watangazaji wa muziki wa dansi, tuige kanuni hii ya Ben James, hakika itakuza sana muziki wetu huu dansi, kwani ni hakika hujawahi sikia kipindi cha XXL nyimbo zinazopigwa humo ni Wachuja Nafaka, Monduli Mobb, Hard Blasters Crew au Watu Pori.
Asanteni.
Cc rogaroga GENTAMYCINE
Sent using Jamii Forums mobile app