Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,421
Nimestushwa kuona namba +255768078523 ya Ben Saanane aliyepotea tangu mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha, leo namba hii ipo hewani inatumika na inatumika na mtu mwingine, mtu huyu amedai ameinunua namba hii kutoka kampuni ya simu ya Vodacom.
Kilichonishangaza ni kuwa kampuni ya Vodacom huku ikitambua kuwa namba hiyo ipo kwenye uchunguzi baada ya mmiliki wake kupotea kwa zaidi ya miezi kumi na mbili sasa, imeamua kuiuza namba hiyo, kitendo hiki ni nini, kama siyo kuvuruga ushahidi huu ambao ni muhimu kuliko jambo lolote? Izingatiwe wakati tukiwa tunasubiri uchunguzi wa vyombo vya ulinzi juu ya Ben Saanane, amepotea tena mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi.
Dhana ya kiuchungu ipo moja tu ambayo ni ya asili ambayo dhana mpya zote hufuata msingi huu tu, Ninakumbuka mkufunzi wangu Mr Zimmerman akikielezea kitabu kinachoitwa MURDER INVESTIGATION MANUAL (2006): "Produced on behalf of the Association of Chief Police Officers by the National Centre for Policing Excellence". Kitabu hiki kina muongozo mzuri wa kiupelelezi
Ujasusi ni hatua ya juu ya shughuli za kipelelezi... Yani ni sawa na mwanajeshi kufikia ukomandoo (field marshal) ambapo sasa hakutakuwa na mafunzo zaidi ya kuyarejelea yaleyale uliyojifunza kama sehemu ya kujiweka sawa.
Hatua za awali kwa mtu yeyote anayefanya upelelezi/ujasusi wa jambo lolote msingi wake ni mmoja tu, sawa kabisa na polisi au mtu yoyote anayeweza kujifunza miiko na taratibu za upelelezi.... Sheria kuu (principles) za upelelezi wowote ule ni NNE tu,
1. Tukio, (Kupotea Ben na Mwandishu,Kupigwa Lissu na Nasari
2. Hisia (suspect), (Risasi, Line za Simu)
3. Kuhoji hisia, (Watuhumiw ambao kwa sasa hakuna)
4. Advanced (Kusonga mbele kiuchunguzi)
Hayo manne ndio msingi wa shuguli za kipelelezi duniani kote, yaani mtu yeyote anayesema anafanya upelelezi wa jambo lolote lazima azingatie hayo. Hivyo ukienda kuuliza mwenendo wa upelelezi wake lazima ukute mtiririko huo...
Ujasusi hushughulika zaidi na mambo ya juu (Advanced) kama yalivyo katika mtiririko wa misingi na taratibu za upelelezi, Huku kwenye ku advance upelelezi kuna mnyumbuliko mkubwa sana ambako ndiko ulimwengu wa watu na vile vya ulimwengu huu ndiko viliko.
Unapofika ngazi ya shahada ya kwanza hadi uzamivu ya kusoma ujasusi kwa sehemu kubwa utasoma watu na yawazungukayo, utasoma uwezo wa kumtafsiri binadamu kwa kila nyanja na hasa kupitia milango yake mitano ya fahamu, huku ujasusu huongeza mlango mwingine wa sita.
Binadamu utamtafsiri katika mambo muhimu ya kiusalama tu, ili kuzuia madhara yaletwayo na binadamu huyu kwa wengine (crimes). Hapa ninamaana sasa unaweza kujikita kutambua na kung'amua mauaji (mfano jaribio la mauaji ya Lissu), ugaidi, wizi, ufisadi nk. Kwa ujumla hapa ni makosa ya jinai yote. Ujasusi upo katika kubaini viashiria vya tukio (kabla ya tukio), kuzuia tukio, tukio lenyewe, baada ya tukio, na kusaidia kubaini ukweli baada ya tukio.
Sasa ili ufunzwe ujasusi wa aina hiyo, moja ya somo huwa ni kuwatambua binadamu na makundi yao na namna bora ya kuyakabili makundi haya ya binadamu bila kuleta madhara kwako na katika jamiii kwa ujumla.
Nidhahiri, binadamu kama walivyo viumbe wengine, hutofautiana kwa mambo mengi. Kwa kushindwa kutambua tofauti zilizopo baina yao, binadamu wamekuwa ni viumbe wanaoongoza kwa migogoro. Kwa kuzingatia hilo, Wakufunzi katika vyuo bora vya Ujasusi wanalazimika kuwafunza maafisa ujasusi wanaosomea mambo haya kwa weledi wa hali ya juu sana.
Kwenye uchunguzi wamatukio yanayohusisha risasi, kwa sehemu kubwa hatua ya kwanza huwa ni kushughulika na ballistic reports (uchunguzi wa silaha iliyotumika katika tukio), hii inakuhakikishia 80% ya kazi yako ya uchunguzi.... Tukishatambua kiwanda kilichotengeneza moja tu ya viambata vya silaha..... Hatua zingine ni chain.....tu....vivyo hivyo kwenye kesi za jinai katika ulimwengu wa kidigiitali kama hii ya Ben na Mwandishi wa Mwananchi, hatua ya kwanza ni kushughulika na mawasiliano yao ya mwisho kupitia mitandao yao ya simu walizokuwa wanazitumia, leo inashangaza kusikia Voda wameuza line ya mtuhumiwa namba moja ambae ni BEN SAANANE katika tukio lake la kupotea.
Mpaka leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na kupotea kwa Ben, Mpaka leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na shambulio la Lissu, Mpaka leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na kupotea kwa mwandishi wa habari, Mpaka leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kwa kuuawa kwa Mawazo, Mpaka leo hakuna aliyekamatwa kwa kuuawa Ali Zona kule Morogoro, Mpaka leo hakuna aliyekamatwa kwa tuhuma za kushambuliwa Kibanda, Mpaka leo hakuna aliyekamatwa kwa kutekwa Roma na mengine meeeeengi ya kufanana nayo,
Huu ndio msingi wa wanaharakati wa haki za binadamu na wanamageuzi kote nchini kuhitaji uchunguzi huru wa kimataifa, hili limefanyika mwaka majuzi tu kule Zanzibar walipouawa Mapadre, na FBI walifanikiwa kutoa mwangaza kwa wahalifu na kukamatwa. Nadharia za kijasusi karibu zote zinamsimamo unaofanana, japo zinaweza kutofautiana mwelekeo tu kulingana na tukio,
Tukio kama la Ben, Lissu, la mwanahabari ama hili la Nassari kiuchunguzi yanaweza kufanana kwa namna moja ama nyingine, uzito wayo utakuja kama hakuna mtuhumiwa/watuhumiwa waliokamatwa kwakuhusishwa nayo, na jambo hili linaweza kubaki kwenye dhamiri ya wapelelezi wetu tu kuamua kuhitimisha uchunguzi wao, au kusimama kwenye mizani ya kisiasa katika taaluma pana kama hii.
Kwanini mawasiliano ya Ben yameuzwa na kampuni ya Voda? Je hawana taarifa kuwa uchunguzi juu ya Ben unaendelea? Hii ni hoja tata inayohitaji majibu ya kitaalamu na sio siasa. Mifano ya kesi ambazo zilidumu mda mrefu na nawasiliano ya waambata wa kesi hiyo yakalindwa mpaka mwisho ni hizi hapa,
1. Kumbukumbu ya Jarada Na. 76/1994 la FBI linahusu kesi maarufu ulimwenguni ya mauaji ya Ronald Opus. Tar. 23 Machi, mwaka 1994, tabibu mchungzi, aliuchunguza mwili wa marehemu, Ronald Opus na kufikia maamuzi kuwa Ronald Opus alikufa kwa kupigwa risasi kichwani. Hii inatokana na jeraha kubwa la risasi kichwani alilokutwa nalo marehemu Ronald Opus. Hapa ndipo tabibu mchunguzi pamoja na Vyombo vya Usalama walikubaliana kuwa wana muuaji mikononi mwao. Mpaka kufikia hatua hiyo, uchunguzi uliofanyika awali na Vyombo vya Usalama, unabainisha kuwa marehemu Ronald Opus alijirusha kutoka kwenye jengo la ghorofa kumi (kwa lengo la kujiua), akiacha kikaratasi chenye ujumbe mfupi kwenda kwa wazazi wake wapendwa, chenye maneno makali: “Poleni, sitaweza kuwasamehe. Nitakuwa na Mungu.” kesi hii ilidumu miaka sita na mawasiliano ya watuhumiwa yalilindwa mwanzo mwisho, leo mawasiliano ya Ben yameuzwa na Vodacom.
2. Jalada la FBI linalosomeka The Collar Bomb Case linaeleza tukio lililotokea tar. 28 Agosti, mwaka 2003 saa 8:28 za mchana. Tukio hilo lilifanywa na mwanaume wa makamo, Bw. Brian Wells, aliyeingia katika benki ya PNC iliyopo Erie, Pennsylvania, akiwa ameshika fimbo fupi ya kutembelea huku akionekana na uvimbe wa ajabu kwenye kola ya shati yake, akielekea moja kwa moja kwa mhudumu wa benki na kumtolea kikaratasi kidogo chenye maandishi yasomekayo: “kusanya wafanyakazi wenye mamlaka ya kufungua sehemu salama ya fedha, jaza dola 250,000 kwenye begi, una dakika 15 tu.” Mhudumu alimuangalia Brian Wells kwa mshangao tu. Wells akahisi kama hajaeleweka vizuri. Ndipo alinyanyua shati lake juu akionesha kitu kama chuma cha ajabu alichovaa mwilini mwake. Akaachia tabasamu pana huku akisema “Ni Bomu hili, mama.” Kesi hii ilidumu kwa miezi 36 na mawasiliano ya watuhumiw/wahanga yalilindwa mwanzo mpaka mwisho, leo mawasiliano ya Ben yameuzwa na Vodacom.
3. Kesi nyingine muhimu kabisa ni ya COWBY MOWATT,
Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1980s na mwanzoni mwa miaka ya 1990s, katika jiji la Washington, D.C., Marekani, lilikumbwa na wimbi kubwa la biashara ya mihadarati aina ya Cocaine, iliyozalisha makundi makubwa hatari na hasimu ya wauzaji yenye nguvu ya pesa na silaha katikati ya Jiji. Baada ya vijana hasa weusi kugundua kuwa usambazaji na uuzwaji mihadarati ungeweza kuwapatia fedha nyingi, silaha na nguvu, ongezeko la makundi haya yalishika kasi ambapo uhasimu baina yao wa kutumia silaha kali za moto, uvamizi na wizi wa kuvunja majumba, uhalifu na mauaji ukatikisa jiji la Washington D.C. Kesi hii ilichukua miaka kumi mbili mpaka COWBY MOWATT alipokuja kukamatiwa kule Arumeru nchini Tanzania akiwa kajichumbia analima bangi. Wakati wote mawasiliano yake yalilindwa, lakini leo Vodacom wameuza mawasiliano ya Ben ilihali Ben hajapatikana.
Hii ni mifano midogo tu ya nadharia za kiupelelezi inavyopasa kuyalinda mawasiliano ya wahusika ili kutovuruga ushahidi kwa namna yoyote ile.
Naomba nijikite kuelezea ushahidi usio na shaka unaoweza kupatikana toka kwa watuhumiwa hata kama wangekuwa mia moja au milioni ikiwa kutakuwa na dhamiri ya kuujua ukweli wa matukio hayo... Sehemu kubwa ya kiuchunguzi huwa katika kubaini ukweli toka kwa watuhumiwa (suspects), hapa ndipo kazi ya ujasusi wa kisaikolojia huhitajika (Forensic Psychology).
Nadharia hii tunaweza kuiangazia kwa mwanasaikolojia Edward Geiselman ambaye ni miongoni mwa waliofanya tafiti nyingi sana kuhusiana na Cognitive interview ( mahojiano ya utambuzi ) katika chuo kikuu cha California. Njia hizi ndizo zinazotumika na wapelelezi duniani kote hadi leo, ingawa kuna maboresho ya kiteknolojia.
Kwa wale waliobahatika kusoma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, watakumbuka, kuna kitu kwenye ujasusi wanaita " cognitive load", unapomuuliza maswali mtuhumiwa, yaani unamuuliza swali anakakaa kwa muda kulitafuta kichwani jibu lake,. Wakati huo huo anajiandaa, unaongeza mzigo mwingine wa swali , kijasusi wanasema unampa " Mental Energy". wakimaanisha ili aweze kufunguka zaidi, watoto wa mjini wanasema kutiririka.
Yote haya katika ujasusi nikutaka kumbaini muhusika na kumpelekea kukiri, huku ukimhoji kama rafiki na kwa upole na kama anataka chochote wakati wa mahojiano unaweza kumpa mfano sigara, kinywaji chakula nk. Mbinu hii inaitwa (Confession Oriented Method with Distinctly Parent Tone).
Kuna mbinu nyingi inatumiwa ili mradi kumtia hatiani mtuhumiwa ama kumuachilia kwakujiridhisha hahusiki. Njia hii ni ya kawaida sana ya kijasusi ya kumhoji mtu ukimuangalia mwili wake hasa macho. Katika macho tunatafuta kumbukumbu yako na ubunifu wako, maana kuna watu wajanja duniani lakini kwa falsafa hii wengi wanafeli.
Mtu yeyote akitaka kukumbuka kitu au jambo lolote wakati ukimuhoji kwakumuangalia machoni, Macho yake huenda kulia, wataalamu wa "Cognitive Interviews" wanaelewa ubongo wake wa kumbukumbu unaanza kufanya kazi. Anapoanza kufikiri (thinking), macho yake yanaenda juu kushoto hapo, yakiashiria utambuzi wa jambo katika ubongo wa kati, na ndipo uongo na ukweli unaupatia hapo kwa mtuhumiwa, huku usiache kumuongeza maswali ya kumchanganya mtuhumiwa, dhumuni lako wewe liwe kuusoma mwili wa mtuhumiwa, huku yeye anapaparika na maneno. Hii inaitwa (Mental note of the suspect's eye activity).
Kuna mbinu nyingine ambayo hata watu wote huwa wanaitumia, inaitwa ya kiuandishi habari ( journalistic approach) na wapo waandishi wa habari makanjanja wa mjini Daslam kama akina Jerry Muro, kwakuijua tu hiyo dhana, basi hujiita Usalama wa Taifa, wakati ni vibaka wa lumumba tu, Kwa wale waliosoma uandishi habari utakumbuka dhana hii, ili uandike habari na iitwe habari lazima kuwepo na kitu kiitwacho 5W ( Five w). 5W ni maneno 5 kwa kizungu ambayo ni (where, when what , who, why) , wataalam wa journalism waliokwenda shule kama vile kamanda Malisa GJ, waliongeza lingine ambalo ni "How" .
Hivi ndivyo civil intelligence tunavyoweza kuutafuta ukweli katika matukio mnasaba kama haya ambayo mamlaka zinaathuriwa na siasa uchwara katika kuutafuta ukweli wake....
Kitaalamu inaamiwa kwamba mtu mkweli huwa anatiririka na anatoa maelezo ya ziada katika mtiririko, ila Mtu muongo au ambaye ni mtuhumiwa kweli na anataka kukwepa tuhuma zinazomkabili, anasimamia jibu lake la msingi .
Sasa kuna wakati nasikiliza haya majibu ya watu makini katika jamii hususani Bungeni, wanasema katika
"jibu langu la msingi ". Je Majibu haya yanatusogeza katika ukweli....
Nani amemteka Ben? Nani alimshambulia Lissu? Nani amemvamia Nassari? Nani amemteka mwandishi wa mwananchi? Nani anafuata? Nini dhamiri? Dhamana ya usalama wa raia na mali zao upoje katika utawala huu?
Nini hatima ya mambo haya? Jibu ni rahisi tu, jukumu la kwanza na lamsingi la serikali yoyote duniani ni usalama wa raia wake, Serikali inayopuuza usalama wa watu wake ni serikali iliyokosa uhalali wa kuongoza watu hao.....
Ni wakati wa watanzania wote kuitaka serikali iwajibike kumrudisha Ben Saanane, Mwandishi wa Habari na kuhakikisha inatuekeza nani alimpiga Lissu na nani alimshambulia Nasari na hatua za kisheria zinachukuliwa.... Hili ni jukumu la watanzania wote sio vyama, sio dini, sio matabaka, bali watu wote bila kujali itikadi zetu. Tuisaidie serikali kukomesha uovu huu katika nchi.
Na Yericko Nyerere