kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,365
- 13,862
Kuwa na Afya njema ni zaidi ya kukosa maumivu mwilini, jeraha au kuvunjika mifupa. Mpira unachezwa na mwili pamoja na akili. Mchezaji che Malone amepata ajali ya gari usiku pale maeneo ya Mikocheni jirani na shule ya FEZA. Hata kama mchezaji wetu huyu kisiki Che Malone hakupata majeraha ya mwili kwenye ajali ile lakini amepata majeraha makubwa kwenye akili yake yanayohitaji matibabu ya haraka sana.
Kwavyovyote vile ajali ile ilimshangaza sana (imevuruga akili), imesababisha ndugu zake kuumia (kumevuruga akili), imesababisha gari yake kuharibika (imechanganya akili). Bila shaka Che anafikiria imekuwaje, itakuwaje na kwanini nyingi sana (inavuruga akili yake pia). Kwa wachezaji wa Afrika hasa Afrika Magharibi ni rahisi kuhusisha ajali ile na nguvu za giza (inamchanganya akili yake).
Ni makosa makubwa sana kwa Ahmed Ally kusema mchezaji wetu hakuumia na yuko buheri wa afya. Huwezi kuwa na afya kwa kukosa kuvunjika tu kwenye ajali, bali inawezekana mchezaji akashindwa kucheza kwasababu ya kupata maumivu, michubuko na majeraha ya kwenye akili (psychologically, socially, spiritually and emotionally) kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu yake kwa 100%. Hata kama hana jeraha la mwili atakuwa ana jeraha la moyo linalohitaji kutibiwa kwelikweli. Namna ya kulitimu jeraha hili ni kumpatatia muda apunzike atafakari, akutanane na spiritual workers wake, consellors na psychologists wabobezi. Pia apewe kila aina ya support anayodhani itamsaidia ku normalize.