Bei ya Mafuta yashuka mwezi Novemba, EWURA yatahadharisha wauzaji

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,515
4,017
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta ya petroli na dizeli nchini kwa mwezi Novemba 2024, ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba.

Kwa mujibu wa EWURA, bei ya petroli kwa lita moja kwa bandari ya Dar es Salaam imepungua kutoka Shilingi 3,011 mwezi Oktoba hadi Shilingi 2,943 kwa mwezi Novemba. Kwa bandari ya Tanga, bei ya petroli imeshuka kutoka Shilingi 3,016 hadi Shilingi 2,948, huku Mtwara ikishuhudia bei ikishuka kutoka Shilingi 3,016 hadi Shilingi 3,015 kwa lita moja.

Kwa upande wa dizeli, bei ya rejareja kwa lita moja Dar es Salaam imeshuka kutoka Shilingi 2,846 hadi Shilingi 2,844. Tanga, bei imeshuka kutoka Shilingi 2,859 hadi Shilingi 2,855, na Mtwara kutoka Shilingi 2,862 hadi Shilingi 2,916 kwa lita moja. Hata hivyo, mafuta ya taa yameendelea kuwa na bei inayotofautiana kidogo katika maeneo tofauti.
1730876593165.png
Mkurugenzi Mkuu EWURA Dkt. James A. Mwainyekule amesema kushuka kwa bei hizi kunatokana na mabadiliko ya bei za kimataifa za mafuta yaliyosafishwa, pamoja na gharama za uagizaji na viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Amesema bei ya petroli katika soko la dunia iliongezeka kwa asilimia 1.56, na dizeli kwa asilimia 4.99, ikilinganishwa na mwezi Septemba 2024. Gharama za uagizaji wa mafuta (Premiums) kwa mwezi huu zilibadilika kwa kiwango kikubwa kwa bidhaa mbalimbali, ambapo gharama za dizeli zilipanda kwa asilimia 14.48, jambo ambalo linaweza kuathiri bei za ndani za mafuta.

EWURA pia imewataka wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha kuwa bei zinazouzwa kwenye vituo vyao haziendi juu ya bei kikomo iliyotolewa na kwamba mabango yenye bei sahihi ya mafuta yaonekane bayana ili kusaidia ushindani wa kibiashara na kulinda maslahi ya walaji.
1730876718018.png

5861726002592465338.jpg
5861726002592465339.jpg

5861726002592465340.jpg
5861726002592465341.jpg
 
Vituo vya mafuta ambavyo wameshusha bei kwenye hii barabara ya kilwa ni PUMA,BARRE na CAMEL TU hawa ndiyo wanauza Tsh 2943/= lakini vituo vingine vilivyobaki bado wanauza Tsh 3011/=

Hawa wajinga ingekuwa bei ya mafuta imepanda najua mapema Sana wangepandisha.
Wauza mafuta ni wahuni Sana hawa washenzi
 
Back
Top Bottom