- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Nimeona taarifa inayoeleza kuwa bei elekezi ya ARVs ni shilingi elfu sabini na sita kwa mujibu wa wizara ya afya. je, ni kweli?
View attachment 3225724
Nimeona taarifa inayoeleza kuwa bei elekezi ya ARVs ni shilingi elfu sabini na sita kwa mujibu wa wizara ya afya. je, ni kweli?
- Tunachokijua
- ARV inasimama kwa niaba ya antriretroviral hizi ni dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) kwa waathirika. Dawa hizi zimekuwa zikitolewa kwa waathirika wa ugongwa kulingana na amelekezo ya wataalamu wa afya.
Taaarifa iliyotolewa na waziri wa afya kwa wakati huo (2023) ilieleza kuwa Kiwango cha Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na wanatumia dawa za Kufubaza VVU (ARV) ni asilimia 97.9 kulinganisha na asilimia 93.6 mwaka 2016/17. Aidha, kiwango cha wanaotumia dawa na wamefubaza VVU ni asilimia 94.3 mwaka 2022/23 kulinganisha na asilimia 87 mwaka 2016/17.
Waziri alieleza pia kuwa anashakuru mashirika ya kimataifa kwa kuunga mkono juhudi hizo za kupambana na UKIMWI likiwemo shirika la USAID. USAID ni shirika la Marekani kwa ajili ya maendeleo ya kimataifa, shirika hili linakadiriwa kuwa na budget ya dola Billion 40 za Kimarekani sawa na Shilingi zaidi ya Trilioni 100 za Kitanzania (101,151,160,000,000 Tsh).
Baada ya utawala mpya wa Donald Trump kuanza kazi January, 2025 nchini Marekani kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika nyanya mbalimbali ikiwemo kusitishwa kwa muda huduma za USAID, jambo ambalo limekuwa na athari kubwa ikiwemo kwenye kada ya afya kwani walikuwa awafadhili pia wa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI.
Madai
Kupitia mtandao wa Facebook mtu mmoja alichapisha taarifa akieleza kuwa Wizara ya Afya Tanzania imetoa na kutangaza bei ya dawa za ARV baada ya USAID kusitisha huduma zake;
“WIZARA YA AFYA TANZANIA IMETOA NA KUTANGAZA BEI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWI (ARV) KUWA NI SHILINGI ELFU SABINI NA SITA IMETOLEA UFAFANUZI KUWA DAWA IZO AWALI ZILITOLEWA BURE NA WAISANI AMBAO NI (US AIDS) AMBAO KWASASA WAMEJIONDOA RASIMI IVYO DAWA IZO KWA SASA ZINAZALISHWA LAKINI ZITAUZWA NA KUTOLEWA USHURU KAMA BIDHAA NYINGINE KUTOKANA NA KUSHUKA NA KUPANDA KWA THAMANI YA DOLA YA MAREKANI”
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia Taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na ina lengo la kupotosha Umma. Ufuatiliaji umebaini kuwa grafiki iliyotumika imehaririwa na siyo halisi kutoka kwa Millard ayo updates aidha ITV live Tanzania inayoonekana siyo ukurasa rasmi wa ITV Tanzania.
Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu katika uandishi wa taarifa hiyo mathalani neno izo badala ya hizo, ivyo badala ya hivyo, waisani badala ya wahisani, US AIDS badala ya USAID, matumizi ya herufi kubwa tupu.
Vilevile kiungo (link) iliyoambatanishwa na Taarifa hiyo inaelekeza kwenye kundi la ITV YETU. NA MATUKIO la Facebook, ilhali kituo cha ITV Tanzania kinatumia ukurasa (Page) na siyo kundi (Facebook group) na ukurasa rasmi wa ITV ni ITV Tanzania.
Wizara ya Afya kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii walikanusha kuhusu taarifa hiyo. Tazama hapa
Februari 8, 2025, Wizara ya Afya ilitoa taarifa kueleza kuwa inawahakikishia wananchi kuwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI haizuzwi na zipo za kutosha. Tazama hapa