mwakani naolewa
Senior Member
- Jul 25, 2024
- 148
- 425
Kaimu mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Sharifa Suleiman amelitaka jeshi la polisi Tanzania kumfukuza kazi aliyekua kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Theopista malya kwa kutoa kauli za dhihaka kwa binti aliyefanyiwa unyanyasaji kwa kubakwa na kulawitiwa. amesema hakustahili kuhamishwa kitengo tu bali kufkuzwa kazi mazima.