SI KWELI BAVICHA yatofautiana na maagizo ya Baraza kuu la chama chao, yaunga mkono tozo zinazokusanywa na Serikali

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Barua inayosemekana ya CHADEMA ikieleza malalamiko ya Baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) kutoridhishwa kwao na maagizo yanayotolewa nje ya vikao rasmi vya katiba ya chama chao.


Bavicha Fake.jpg

Barua inayodaiwa kutolewa na BAVICHA ikipingana na maelekezo ya baraza kuu la chama chao
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na barua inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha msimamo wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) likitoa msimamo wake wa kutokuafikiana na maamuzi ya Baraza kuu la chama hicho.

Sehemu ya maelezo ya barua hiyo yanasema;

"Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) tunatoa taarifa Kwa umma juu Kutoridhishwa kwetu na maagizo yanayotolewa nje ya vikao rasmi vya kikatiba.

Maagizo ambayo yamekuwa ya kilitaka Baraza kuanzisha mashambulizi mitandaoni dhidi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali hasa Tozo za kibenki, maagizo hayo yamekuwa hayafuati utaratibu wa kichama na hayana faida Kwa chama bali ni mradi binafsi wa watu wachache ambao wamejipa umiliki wa chama na kukitumia kujipatia fedha, jambo ambalo halikubaliki kamwe."


JamiiForums imewasiliana na viongozi wa CHADEMA ambapo amekana kuitambua barua hiyo. Viongozi hao wamewaomba watanzania kuipuuza taarifa hiyo kwani sio ya kweli na imetengenezwa na watu wasiokitakia mema chama chao.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom