BAVICHA na chapwa wa fikra

mabuba

Senior Member
Dec 5, 2006
133
90
Mara nyingu nina amini katika vijana, huwa napatwa na mstuko pale vijana wanapokuja na uchapwa wa mawazo. Jana Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) limetoa tamko dhidi ya hotuba ya MH. Rais JPM aliyoitoa pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tamko lao lenye kubananga weredi wa hotuba ya Mh. Rais katika limejikita katika Nyanja zifuatazo:


1. Wanafunzi waache kutumiwa na wanasiasa. Bavicha wanashangaa hili, wanajifanya vipofu kuwa halipo. Suala la wanafunzi kutumiwa na wanasiasa lipo sana, hii ili ilazimu serikali kupiga marukufu siasa vyuoni, BAVICHA wanaona uwepo wa shirikisho la vyuo vikuu ni kutumiwa na wanasiasa. Wameshindwa kuelewa kuwa hizi ni dhana mbili tofauti, utumiwaji kisiasa na ushiriki katika siasa za chama chao, hii ni kama ilivyo CHASO. Utumiwaji wa vijana kisiasa ni dhana pana sana. Hata ndani ya CCM vijana wanaweza kutumiwa kisiasa ndani ya makundi ya watu, vivyo hivyo ndani ya CDM. Hapa BAVICHA wamepotoka ama wanapotosha kwa kujua ili kuleta msisimko katika jamii.


2. Pia tamko lao limeelezea juu ya KUFUTA KWA MASOMO YA SIASA. Hili nimeshindwa kuwaelewa vijana hawa wameshindwa kabisa kutofautisha taaluma na siasa za majukwaani. Eti kama Rais anasema wanafunzi wasitumike kisiasa, wafute masomo ya “Political Science”. Naomba wakubwa wao hawa vijana, akina John Mrema , wanafunzi wa sayansi ya siasa waweza kuwafafanulia hili. Hata hivyo BAVICHA wanapaswa kuelewa kuwa si kila mtanzania anayesoma “political science” lazima awe mwanasiasa, hii ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine.

.

3. Pamoja na hayo, BAVICHA wamesema Mh. Rais amewaita vyuo vingine vilaza. Nasikitika kusema kuwa wamejitoa ufahamu wa kutosikia, JPM hakusema hicho, kuwa vyuo vingine ni vilaza, bali alisema kuna vilaza walikuwa kwenye kundi lililodahiliwa Katika vyuo, ambalo halina sifa. Kundi hilo amelitanabaisha kwa umakinifu kabisa kuwa ni wale wenye daraja 4, lakini wamedahiliwa katika kiwango cha Shadada (St. Joseph) na wengine stashahada (UDOM) hawa ndio walioitwa vilaza. Pamoja na hayo, Rais amekwenda mbele nakuwaonesha namna ya kufika huko kwa kwenda kusoma vyuo vya kiwango chao cha elimu.


4. Tamko la Bavicha linasema kwa kunukuu sheria namba 4 ya mwaka 2014, kwamba wanafunzi hao wapo pale kisheria. Rais katika hotuba yake hakuna sehemu alisema kuwa wanafunzi wale hawapo kisheria. Bavicha naomba muwe mnasikiliza vizuri ili mtoke na matamko yenye mashiko na weredi. Mh. JPM alisema katika kundi lenye wanafunzi 7802 wapo wenye sifa na akataja, wapo wenye daraja 1, 2 na 3. Hawa ndio wenye sifa walitakiwa kuwepo pale. Wale wenye daraja la nne hawakupaswa kuwepo pale , ndio maana Rais alisema kuwa, sasa hivi Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako yupo kwenye uchambuzi wa kuchambua wale wenye sifa. Naomba muwe wasikivu katika hotuba zinapotolewa hata na viongozi wenu.


5. Bavicha katika tamko lenu mmemalizia suala ambalo mnalo jibu. Suala la barabara hewa, eti mnauliza barabara hewa zimeletwa na nani? Jibu ni rahisi ni serikali ya CCM. Lakini Rais anapohoji, ina maanisha wamegundua makosa na sasa wanataka kurekebisha. Na hili sio kosa hata kidogo, kosa ni pale unapofanya makosa halafu unjifanya huyaoni. Hapa mimi nasema Rais na Chama chake wameonesha ukomavu.


Mwisho niwasihi kwamba, uzandiki wa kifikra ni uladhini wa mawazo uliojaa utomaslahi ya utaifa. Vijana jikiteni katika ukosoaji wenye tija wa ujenzi wa Taifa letu, na si kukurupuka na hoja ambazo inaonesha kuwa ni umbumbumbu na ubanangaji wa hoja.

Mwanamtaa

Mabuba FKM
 
Tamko lenyewe Bavicha chama chenyewe hata office hakina sasa hao Bavicha ni nani watoe tamko kwa Mh rais ?

Watoe na tamko lowasa akachunge kama alivyoahidi
 
Mkapa alipowaita baadhi ya watu kuwa ni wapumbavu na malofa alikuwa sahihi japokuwa wastaarabu waliona kama vile mzee amepitiliza mipaka. Leo hii ushahidi wa upumbavu na ulofa Tanzania ni mwingi na upo dhahiri kabisa.
 
BAVICHA walikuwa wadhihirisha walivyo vilaza, wanataka kujipendekeza kwamba wao ni watetezi, kile ambacho serikali inapinga UKAWA wanakisapoti, vilaza kweli kweli .mtu mwenye akili huwezi kutetea ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…