Basi lenye ushawishi na uhakika wa kusafirisha mizigo midogo

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,381
3,826
Nina muda kidogo nimekuwa mteja wa mabasi kwa kusafirisha vifurushi na mizigo midogo kutokea Arusha kwenda Dar na Morogoro, nimebaini mapungufu mengi na ubora wa huduma kati yao, the best nime baini ni kampuni ya BM ni seme kwanini:

1.Wao hawalazi mizigo na vifurushi endapo kuna basi la kuondoka, hata kama ni usiku, dakika za mwisho labda uwasilishe pakiwa hamna basi kwa wakati huo.

2. Unafuu wa bei ya kusafirishia, kiwango cha chini ni elf 5 kwa bahasha na kifurushi saizi flani, wana standard zao yan mpaka mteja anayepokea anafahamishwa kuhusu thamani ya mzigo huo

3. Anayetuma anajulishwa kwa sms kuwa kampuni imepokea mzigo wake , na atakaye upokea anajulishwa kwa sms, hii ni uhakika zaidi na mteja kuwa na uhakika na mzigo wake kuwa upo mikononi mwao.

KAMPUNI YA KILIMANJARO

Hawa wana mabishano sana, unaweza ukafika ukaambiwa huo mzigo haujafika kumbe bahasha ndogo hajaangalia vizuri ulipo, pia nimekutana na wafanya kazi wakibishana kutopokea mzigo kutoka arusha, mara mfanya kazi x hakuupakia na haujapokelewa na mfanya kazi x, hi route ya Dar-Ars. Mara oh alitakiwa atume kwenye bahasha kubwa, sasa unaanza kuulizwa ni kitu gani, unakaa mda mrefu, management ya kutuma na kupokea hawako vizuri.

KAMPUNI YA ESTHER

Hawa vifurushi au baasha wanaanzia sh 10k si chini ya hapo, wanaringa sana hawana customer care, a labda ni kutaka ku wa discourage wateja kuwa usafirishaji wa vifurushi sio miongoni mwa vipaumbele vyao.

KAMPUNI YA ABUDI

Ni wasahaulifu, hawatumi kwa wakati, unaweza ukaambiwa haujafika pamoja na kwamba umetuma toka jana

KAMPUNI YA SHABIBY

Hii kampuni magari yote ya usiku hayasafirishi mizigo/ vifurushi ilinikuta nikawa mpole mara mbili kwa Route ya ARS-Dodoma

Niseme tu kwamba usafirishaji wa vifurushi una hela nyingi na mshindani mzuri ana kipato kikubwa kwenye mizigo unapo safirisha kwa bei nafuu, kumhakikishia mteja mzigo wake upo mikononi mwao hadi unapofikia ofisi x ni kumfanya mteja awaamini zaidi na unafika kwa kumridhisha mteja. Ofisi za BM za kusafirishia mizigo zina msongamano kuliko makampni mengine. Tusibaki kulalama na kugombana na makampuni ya mabasi, kila mtu aende atakapoona anarihika na hakuna usumbufu.
 
Bm iko safi saana kusema ukweli ila kwa mikoa ya mwanza na kanda ya ziwa nilifurahia pia huduma ya happy nation kwa ifakara, mahenge ni
 
Fungua kampuni ya vifurushi!
 
Abood nawakubali Sana.

Ila kûna kijana wao mmoja pale shekilango ñàona anaingiza TAMAA na ataanza kuharibu jina la Kampuni.

Mzigo weñye thamani ya Laki tano kaniambia kusafirisha 70k ikipungua 60k.

Naenda Kampuni ya kiomboi mzigo ukasafirishwa Kwa Tsh 30k
Nendeni posta!
 
Kwenye mabasi pia kuna udalali saana kuna siku nilikuwa na boksi la kama kg moja lilikuwa linaenda kanda ya ziwa musoma kampuni ya kwanza walinambia sh 30 elfu na nyingne 25 elfu na mwishowe nkafika happy nation huwez amini nilisafirisha kwa sh elf 15 mpka nkashangaa
 
BM yuko vizuri sana but kwa sisi Dar- td tunakosa huduma yake tunapita na ABC naye yuko smart sana
 
Kwenye mabasi pia kuna udalali saana kuna siku nilikuwa na boksi la kama kg moja lilikuwa linaenda kanda ya ziwa musoma kampuni ya kwanza walinambia sh 30 elfu na nyingne 25 elfu na mwishowe nkafika happy nation huwez amini nilisafirisha kwa sh elf 15 mpka nkashangaa

Unajua bei hupangwa na aina ya usafiri uliyochagua kuitumia
Huwezi kutegemea kulipa bei sawa kwa mzigo uliosafirisha kwa basi la daraja la kwanza na basi la daraja la tatu. Nina maanisha, basi la daraja la kwanza, la pili na la tatu kila moja litakuwa na bei yake
Kuna uwezekano umetumia basi zuri tu ila la daraja la chini kidogo....
 
Watu wa mabasi katika vitu wanachukia kusafirisha ni hizo Parcel wanasema ni hatari zinaweza kukupeleka hata jela labda ndo maana wanakua wasumbufu.

Kwa njia ya uhakika zaidi tuma kupitia posta kwa EMS
 
Back
Top Bottom