Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
4,917
15,680
Habari ya mchana wakuu, niko hapa maeneo ya kariakoo kuna ajali imetokea gari ya mwendokasi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke imemgonga mtu na mwili kusagika hapo hapo, inasemekana huyu ni mtu wa tatu anagongwa na kufa hapo hapo na huyu mwanamke.

Mwenye maelezo zaidi kuhusu huyu mwanamke dereva wa mwendokasiatujuze.

====================

UFAFANUZI WA DART
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), William Gatambi:

Bodaboda alikuwa anakatisha Mtaa wa Mafia wakati Taa za Kijani zimeruhusu, akagongwa na Basi akapoteza Maisha palepale, baada ya tukio hilo baadhi ya waendesha Bodaboda wakaanza kuponda basi kwa mbele, wakavunja vioo.

Baada ya hapo wakamvamia Dereva wa Basi na kuanza kumpiga na kumuibia pochi yake. Baadaye Dereva ambaye aliongoza wenzake kushambulia basi na kumjeruhi Dereva amekamatwa na yupo Polisi.

Pia, Dereva naye yupo Polisi muda huu kwa ajili ya kutoa maelezo.
 
Habari ya mchana wakuu, niko hapa maeneo ya kariakoo kuna ajali imetokea gari ya mwendokasi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke imemgonga mtu na mwili kusagika hapo hapo, inasemekana huyu ni mtu wa tatu anagongwa na kufa hapo hapo na huyu mwanamke.

Mwenye maelezo zaidi kuhusu huyu mwanamke dereva wa mwendokasiatujuze
Unavyo rudiarudia neno mwanamke inaonekana una chuki flani naye kwani wanaume madereva wangapi wa mwendo kasi wamegonga watu
USSR
 
Habari ya mchana wakuu, niko hapa maeneo ya kariakoo kuna ajali imetokea gari ya mwendokasi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamke imemgonga mtu na mwili kusagika hapo hapo, inasemekana huyu ni mtu wa tatu anagongwa na kufa hapo hapo na huyu mwanamke.

Mwenye maelezo zaidi kuhusu huyu mwanamke dereva wa mwendokasiatujuze
Mwendokasi ni sawa na treni, kuna katabia cha kijinga kariakoo raia na bodsboda wanacheza sana njis ya mwendo kasi
 
Iwe barabara inapaswa kuwekewa kingo za kuta za chuma.. Inaingiliwa mno na wapita njia na sometimes bila tahadhari.. Na yule dada ni rough driver
Mwendokasi ni sawa na treni, kuna katabia cha kijinga kariakoo raia na bodsboda wanacheza sana njis ya mwendo kasi
Pale taa zilikuwa zimeruhusu mkuu watu wapite, sasa huyu mwanamama katoka huko na mwendokasi mazima kamzoa mshikaji, amembuluza karibia mita mia kasoro mbele.
 
Back
Top Bottom