Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 336
- 696
Basi la Abiria la Nguruka T545 D/W imegonga Treni ya Mizigo Y611 na kusababisha mabehewa matano kati ya 30 ya treni hiyo kuanguka na abiria 14 wa basi hilo kupata majeraha madogo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) imesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Novemba 10, 2024 majira ya saa 4:20 usiku katika makutano ya reli na barabara kati ya Malagarasi na Nguruka, mkoani Kigoma
Taarifa hiyo imedai kuwa chanzo cha ajali hiyo kilitokana na dereva wa basi kulipita basi lingine lililokuwa limesimama ili kupisha treni na kusababisha ajali