Bashe hataki tujenge reli kwa fedha zetu!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,533
Huu ni mchango wa Bashe mbunge wa nzega.

Hataki serikali itumie fedha za makusanyo kufanyia miradi na mfano alioutoa ni ujenzi wa Reli ya Kati ambayo imekuwa ni kiunganishi kikubwa kati ya mikoa ya mashariki na magharibi .
Badala yake anataka serikali itumie PPP.
 
Gharama za vyakula kweli zipo juu..uongozi uliopo madarakani..angalieni miradi ambayo italenga moja kwa moja maendeleo ya MTU mwenye kipato cha chini..wataalamu wa uchumi mtusaidie..maisha ni magumu sana.wananchi ni waoga kusema ukweli.hali ni ngumu.
 
Nilimsikia Rais Museveni atachangia SGR.
Uturuki wamesaini mkataba kusaidia ujenzi wa SGR.
JMT watachangia pia hivyo PPP itafanya kazi hapo.
Watunga sheria wetu wanayajua vizuri sana, tatizo wanacheza na maneno kuibua hisia kutoka kwa wananchi.
 
Tumenunua zile takataka za kupaa angani na tumeona ilivyotugharimu mpaka sasa.

Kwa sasa bei ya vyakula ipo juu, naona ni vyema hizo pesa ziwekezwe kwa wakulima ili kupunguza ukali wa maisha.
Kwanini unasema ni takataka? Ushawahi kutumia usafiri wa ndege kabla ya hizo bombadier? Fastjet walikuwa wanafanya wanavyotaka....tuache maneno maneno
 
PPP iko wapi mpaka sasa.

Sekta binafsi kwa taifa letu baado sana. Watu wanafikiri Ulaya na Marekani walianza na PPP!! Walianza kama sisi na mwisho sekta binafsi wakaona inawalipa ndo wakaanza kuendesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…