Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa Nipeni Maua yangu wa Roma Mkatoliki.
Je, taarifa hizi zina ukweli ndani yake?
Je, taarifa hizi zina ukweli ndani yake?
- Tunachokijua
- Aprili 19, 2023, Mwanamuziki Roma Mkatoliki alitoa wimbo unaoitwa "Nipeni Maua yangu" unaozungumzia mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Hadi Aprili 24, 2023, kwenye mtandao wa YouTube, wimbo huu ulikuwa umetazamwa na watu zaidi ya 770,000, umepokea maoni zaidi ya 7700 na ndio ulikuwa wimbo unaoshikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya nyimbo zinazovuma zaidi (Trending).
Wimbo huu umezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku taarifa zisizo rasmi zikisema kuwa tayari Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia usichezwe kwenye vituo vyote vya redio runinga nchini.
JamiiForums imezungumza na Isack Bilali, Mkuu wa Kitengo cha Habari BASATA ambaye aliyethibitisha kuwa habari hizo hazina ukweli. Ameweka bayana kuwa kama kungekuwa na taarifa hizo basi baraza lingetoa taarifa rasmi kupitia vyombo sahihi, ikiwemo kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai yanayosambaa mitandaoni yakidai kuwa BASATA imeufungia wimbo wa Nipeni Maua yangu wa Roma Mkatoliki hayana ukweli.