Barua yangu kwa Rais wa Zanzibar

hatedthemost

JF-Expert Member
Oct 20, 2021
454
315
Habari wana JF.

Eid Mubarak kwa wanaosheherekea!

Mie ninalo la moyoni na samahani kwa yeyote nitakayemkwaza!
1.Zanzibar ni kisiwa cha kuvutia lakini jamani uchafu umezidi!!! Juzi TU stori za kipindupindu lakini hakuna anaetilia maanani inaumiza.

Watu watupa taka kila mahali hebu mwenye mamlaka aangalie namna ya kufanya kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira

2. Barabara mpya zinajengwa katika maeneo mbali mbali lakini hakuna mitaro,njia za watembea Kwa miguu,bumps wala alama za barabarani

Inatandikwa lami mengine mtajijua wenyewe.

Madereva wanaachia tu spidi hakuna anaejali uhai wa anaepita barabarani.

3. Ujenzi wa bara bara hauzingatii taratibu za afya kama kumwagilia maji kupunguza vumbi,mnaumiza wananchi wenu.

Mpaka bara bara ziishe wameshaugua sana. Yapo mengi lakini natumaini wahusika wataona
 
Back
Top Bottom