Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,038
- 55,915
Mh Rais Samia Suluhu Hassan
Nakusalimia kwa Jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Awali ya yote nianze kwa kukutakia uzima na afya katika kutekeleza majukumu yako.
Baada ya salamu hizo nije katika ujumbe ninaokusudia kukuandikia.
Ni hivi ndugu Rais, WANANCHI HATUNA MAJI YA UHAKIKA na kweli hii hali imetuchosha mno, inatufedhehesha mno na kwa ukwrli kabisa inatukasirisha mno.
Ndugu Rais, Leo miaka 64 ya Uhuru wa nchi hivi kweli Serikali yako na zenu za CCM zomeshindwa kutatua shida ya Maji?. Kitu ambacho ni basic need, kitu ambacho ni muhimu kuliko chochote kile katika maisha ya mwanadamu?.
Ndugu Rais hivi nyinyi vipaumbele gani ni muhimu kwanza kuliko maji?. Mko busy kununua midege ambayo ni secondary need, mko busy na Miuchaguzi feki ambayo huwa mnaivuruga, mko busy na mamisafara mirefumirefu, mko busy kununua magoli ya Simba na Yanga Lakini Suala la MAJI YA UHAKIKA mnafeli, hivi ndugu rais hamuoni aibu hamuoni haya?
Ndugu rais,
Zamani ilikuwa kila robo ya mwisho ya mwaka shida ya maji inaanza, sababu zilizokuwa zinatolewa ni zilezile, ooh ukame, ooh upungufu wa maji kwenye mto fulani. Sasa siku hizi hata kwenye miezi ya mwanzoni mwa mwaka shida ya maji iko palepale. Ndugu rais mnatupeleka wapi?
Ndugu rais
Hivi ninavyokwambia Jijini Dar es salaam, matatizo ya maji mtindo mmoja. Yaani tangu enzi za Nyerere zikaja za mzee Mzee Mwinyi na mpaka leo maji ni ya manati, hivi mnafanya nini ofisini nyie aisee?.
Ndugu Rais
Nyinyi hamna kisingizio cha maana juu ya uhaba wa maji nchini. Sababu kuu ni Incompetence yenu, Kutokujali mambo ambayo ni Primary mnaconcentrate kwenye mambo ambayo ni Secondary. Haiwezekani hii nchi yenye maji mengi kuliko nchi yoyote katika Africa iwe na uhaba wa maji wa kutisha kwa wananchi wake utadhani ni nchi ya jangwa. Yaani haiwezekani, common sense inagoma, inakataa katakata. Hili linaonyesha kuwa serikali zenu za CCM zimekuwa hopeless bin useless. Biblia inasema "IN ABUNDANCE OF WATER, THE FOOL IS THIRSTY"- yaani palipo na maji mengi, mpumbavu yeye bado ana kiu. Sasa inakuwaje tuna vyanzo vya maji mengi nchini namna hii halafu bado tuna shida ya maji kiasi hiki, ina maana sisi ni wapumbavu?.
Ndugu Rais.
Achana na kufanya vitu vya kufikirika. Solve vitu vya msingi kwanza. Solve tstizo la Maji, weka mazingira ya kuhakikisha raia wanakula wanashiba, weka mazingira ya kuhakikisha wanavaa mavazi yenye heshima, weka mazingira mazuri ya usafiri wao, weka mazingira ya elimu nzuri na huduma bora za afya. LAKINI KATIKA YOTE HAYO MAJI NDO TOP PRIORITY
Punguza na bana matumizi ya serikali.
Rasilimali za nchi zitumike wisely, achana na habari za kuingia mikataba mibovu ya miaka mingi ili kupata hela za harakaharaka za kutekeleza miradi ya muda mfupi ya "kuombea kura" (ofcourse natambua kuwa siku hizi hata kura zenyewe haxina thamani anyway.)
Ndugu Rais, liko wapi Bwawa la Kinunda?- Miaka minne iliyopita kulipokuwa na shida ya maji ya kutisha Dar (kama kawaida yake), Ulikuja na kauli ya kisiasa ya ujenzi wa bwawa la Kinunda , hebu tueleze ndugu Rais, hilo bwawa limefikia asilimia ngapi ya ujenzi na limetengewa bajeti sh ngapi?. Ndugu Rais wananchi tunapenda ukweli siyo kupigwa Saundi!
Ndugu Rais
Nawasilisha huku nikiwa na hasira sana kwa sababu ya serikali yako na za wenzako waliopita kushindwa kusolve tatizo la maji wakati tuna vyanzo kibao vya maji nchini.
Missile of the Nation.