Barua ya Wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa CCM Taifa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
7,444
9,902
Kwako, Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Amiri Jeshi Mkuu,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa,
Mpendwa Kiongozi wetu,

Nakupa salamu za heshima na taadhima nikiwa na imani kubwa na uongozi wako imara. Kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kuchukua fursa hii kuonyesha heshima yangu kwako na kuthamini juhudi zako zisizo na kifani katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa nchini. Nikifikiria mbele, ninashukuru kwa utekelezaji wa mipango ya kimkakati ambayo inaleta ustawi wa watu wetu.

Mheshimiwa Rais,

Katika barua hii ya wazi napenda kutoa wazo la kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha mabasi makubwa na daladala hapa nchini. Itakuwa vizuri kama kiwanda hicho kitazalisha mabasi ya aina tatu, ya kutumia gesi, umeme, na mafuta. Sekta ya usafiri nchini imekua kwa kasi kubwa sana, na tunao uwezo wa kuingiza mapato mengi kupitia uwekezaji huu. Kwa kuanzisha kiwanda cha mabasi, tutakuwa na fursa ya kufikia soko kubwa na kuongeza mapato mengi sana kwenye serikali yetu.

Mheshimiwa Rais, naomba pia kama ikiwezekana, wawekezaji wanaoshiriki katika mradi wa mwendokasi, ambao ni mradi mkubwa wa usafiri wa mabasi kuliko yote nchini, tuwavute waweze kuwekeza pia katika uzalishaji wa mabasi makubwa na daladala. Huu ni uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi wetu na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

Naona mapato ya bure tena mengi sana kupitia uwekezaji huu. Hii ni fursa nzuri kwa taifa letu, na ninaamini itaongeza uchumi wa taifa na kuchangia katika ustawi wa jamii nzima.

Nashukuru kwa umakini wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Hii ni hatua muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia kiwango cha juu cha maendeleo katika sekta zote muhimu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
+255687746471
Asante sana

Wasomaji wa Barua hii mnaweza kushangaa kwanini nimeamua kuandika barua hii ya wazi kwa Rais Dr. Samia Suluhu. Kama ulikua hujui mwaka jana Tarehe 9 May 2024 Rais Samia alizindua kiwanda cha Magari hapa Tanzania, kiwanda kipo kigamboni.

SAMIA-9.jpg

SAMIA-6.jpg

GNIokupXIAA3klB.jpg

Kuanzia leo tunaweza kumwita Rais Samia ni mama wa viwanda vya magari kwasababu alifanikisha hilo na hili anaweza kufanikisha.

Naomba kuachia video ya uzinduzi:

View: https://www.youtube.com/live/PqOXrPN6Q1M?si=11KocCkGclgLkjqi
 
Kupanga majiji,miji na vijiji tumeshindwa mambo ya kutengeneza mabus ndo tutaweza ?

Huwezi fanya mambo makubwa ikiwa madogo yamekushinda.
Kiwanda ni mapato, mabasi ni mapato, mabasi ni kodi boss, mabasi ni uwekezaji ukimwita mwekezaji ukamhakikishia usalama wa kiuchumi wa biashara yake anawekeza na return anaiona.
 
Kupanga majiji,miji na vijiji tumeshindwa mambo ya kutengeneza mabus ndo tutaweza ?

Huwezi fanya mambo makubwa ikiwa madogo yamekushinda.
Hii ndio shida ya wasomi wa afrika wanawaza vitu vilivyoandikwa tu bila kujali uhalisia.

Imagine 70% ya Watanzania ni wakulima tena wa jembe la Mkono.

Majembe haya ya mkono yanaagizwa yote china.

Hapa tuna Madini ya Chuma matrilioni kwa matrilioni.

Hana hata kiwanda cha Chuma cha kugongelea lakini anawaza Kiwanda cha Mabasi🤣🤣🤣🤣
 
Kwako, Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Amiri Jeshi Mkuu,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,
Mpendwa Kiongozi wetu,

Nakupa salamu za heshima na taadhima nikiwa na imani kubwa na uongozi wako imara. Kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kuchukua fursa hii kuonyesha heshima yangu kwako na kuthamini juhudi zako zisizo na kifani katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa nchini. Nikifikiria mbele, ninashukuru kwa utekelezaji wa mipango ya kimkakati ambayo inaleta ustawi wa watu wetu.

Mheshimiwa Rais,

Katika barua hii ya wazi napenda kutoa wazo la kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha mabasi makubwa na daladala hapa nchini. Itakuwa vizuri kama kiwanda hicho kitazalisha mabasi ya aina tatu, ya kutumia gesi, umeme, na mafuta. Sekta ya usafiri nchini imekua kwa kasi kubwa sana, na tunao uwezo wa kuingiza mapato mengi kupitia uwekezaji huu. Kwa kuanzisha kiwanda cha mabasi, tutakuwa na fursa ya kufikia soko kubwa na kuongeza mapato mengi sana kwenye serikali yetu.

Mheshimiwa Rais, naomba pia kama ikiwezekana, wawekezaji wanaoshiriki katika mradi wa mwendokasi, ambao ni mradi mkubwa wa usafiri wa mabasi kuliko yote nchini, tuwavute waweze kuwekeza pia katika uzalishaji wa mabasi makubwa na daladala. Huu ni uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi wetu na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

Naona mapato ya bure tena mengi sana kupitia uwekezaji huu. Hii ni fursa nzuri kwa taifa letu, na ninaamini itaongeza uchumi wa taifa na kuchangia katika ustawi wa jamii nzima.

Nashukuru kwa umakini wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Hii ni hatua muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia kiwango cha juu cha maendeleo katika sekta zote muhimu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
+255687746471
Asante sana
Wafanye mipango miji kwanza, miji imekaa kiswahili swahili. Hakuna barabara za kutosha, kubwa na feeder roads kwenye miji yetu yote, Nyumba zimejengwa ovyo ovyo bila utaratibu, unazalisha slums nyingi, miji michafu, hakuna sewage system, miji imekosa vyoo vya public, watu wanajisaidia vichakani, kwenye mito na wamefanya bahari kuwa vyoo vyao, nchi ni chafu mno. Rekebisheni hayo kwanza kabla ya kuunda magari. Bado nchi ipo savage katika level ya chini sana ya maendeleo.
 
Hii ndio shida ya wasomi wa afrika wanawaza vitu vilivyoandikwa tu bila kujali uhalisia.

Imagine 70% ya Watanzania ni wakulima tena wa jembe la Mkono.

Majembe haya ya mkono yanaagizwa yote china.

Hapa tuna Madini ya Chuma matrilioni kwa matrilioni.

Hana hata kiwanda cha Chuma cha kugongelea lakini anawaza Kiwanda cha Mabasi🤣🤣🤣🤣
Mkuu mahitaji ya vitu vyote ni muhimu. Hoja yako pia ina mashiko, nayo aisome.
 
Hii ndio shida ya wasomi wa afrika wanawaza vitu vilivyoandikwa tu bila kujali uhalisia.

Imagine 70% ya Watanzania ni wakulima tena wa jembe la Mkono.

Majembe haya ya mkono yanaagizwa yote china.

Hapa tuna Madini ya Chuma matrilioni kwa matrilioni.

Hana hata kiwanda cha Chuma cha kugongelea lakini anawaza Kiwanda cha Mabasi🤣🤣🤣🤣
Asante kwa andiko zuri boss. Lakini kumbuka tuna Wizara mbalimbali. Kwa hiyo tunatakiwa kwenda na mambo yote kwa pamoja.

Swala la kutengeneza Majembe kwa kutumia Chuma lipo kwenye Wizara ya Kilimo huku likitegemea Wizara ya Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Kutengeneza Mabasi ni Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Viwanda na Biashara. Kwa hiyo mambo yote hayo yanatakiwa kwenda kwa pamoja, Wizara zetu zinaweza kutafuta wawekezaji wenye mitaji na utekelezaji wa uzalishaji ukaanza kwa pamoja. Serikali kupitia wizara zake ina uwezo wa kufanya mambo mengi kwa pamoja wala haina tatizo.
 
Kwako, Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Amiri Jeshi Mkuu,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,
Mpendwa Kiongozi wetu,

Nakupa salamu za heshima na taadhima nikiwa na imani kubwa na uongozi wako imara. Kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kuchukua fursa hii kuonyesha heshima yangu kwako na kuthamini juhudi zako zisizo na kifani katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa nchini. Nikifikiria mbele, ninashukuru kwa utekelezaji wa mipango ya kimkakati ambayo inaleta ustawi wa watu wetu.

Mheshimiwa Rais,

Katika barua hii ya wazi napenda kutoa wazo la kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha mabasi makubwa na daladala hapa nchini. Itakuwa vizuri kama kiwanda hicho kitazalisha mabasi ya aina tatu, ya kutumia gesi, umeme, na mafuta. Sekta ya usafiri nchini imekua kwa kasi kubwa sana, na tunao uwezo wa kuingiza mapato mengi kupitia uwekezaji huu. Kwa kuanzisha kiwanda cha mabasi, tutakuwa na fursa ya kufikia soko kubwa na kuongeza mapato mengi sana kwenye serikali yetu.

Mheshimiwa Rais, naomba pia kama ikiwezekana, wawekezaji wanaoshiriki katika mradi wa mwendokasi, ambao ni mradi mkubwa wa usafiri wa mabasi kuliko yote nchini, tuwavute waweze kuwekeza pia katika uzalishaji wa mabasi makubwa na daladala. Huu ni uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi wetu na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

Naona mapato ya bure tena mengi sana kupitia uwekezaji huu. Hii ni fursa nzuri kwa taifa letu, na ninaamini itaongeza uchumi wa taifa na kuchangia katika ustawi wa jamii nzima.

Nashukuru kwa umakini wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Hii ni hatua muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia kiwango cha juu cha maendeleo katika sekta zote muhimu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
+255687746471
Asante sana
Ila tusitekwe kwenye mabasi!
 
Mimi naona kwanza tungepunguza kodi katika uingizaji wa magari hapa Nchini hususan mapya ili watu wanunue. na sisi kama Nchi tupate kodi kupitia mafuta wanayoweka na kodi zingine mbalimbali.kuliko kuwa na kodi kubwa ambayo wengi wanashindwa wakati mwingine hata kulipia kukomboa gari zikitua bandarini.

Na kama ni suala la kujenga kiwanda cha kuzalisha magari basi serikali ingefanya ushawishi wa kuvutia wawekezaji ili wao ndio wajenge na serikali ibaki inakusanya kodi tu.

Kuliko kusema serikali ndio ijenge kwa kutumia kodi zetu halafu unakuta mwisho wa siku kiwanda kinakufa na kubakia magofu. hivyo kuwa hasara kwa kodi za mtanzania mlipa kodi. Maana watanzania janja janja nyingi sana na upigaji pamoja na kuhujumu miradi ya serikali.

Kwa sasa Kazi ya serikali iwe ni kuvutia wawekezaji na kukukusanya kodi yote inayotakiwa kisheria na siyo kujiingiza moja kwa moja katika biashara kwa kodi zetu.
 
Back
Top Bottom