FisadiMkuu
Member
- Mar 1, 2023
- 8
- 4
Barua ya wazi kwa:
Naibu Waziri,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Tanzania.
Ndugu;
Tafadhali husisha kichwa cha barua hapo juu. Mimi ni mtumishi katika chuo kikuu kimoja hapa Tanzania ambaye kwa sasa nipo masomoni katika chuo kingine cha hapahapa Tanzania kama mnufaika mmoja wapo wa mradi wa HEET.
Kwa masikitiko makubwa, naomba niseme wazi kwamba nimekwazika na kitendo cha wasimamizi wa mradi tajwa kutubadilishia utaratibu wa malipo kwa ajili ya tafiti bila muongozo mpya wowote.
Muongozo wa mradi kwa sisi wanufaika uliweka wazi kwamba kwa tafiti za “Masters” tungepata US dollars 10,000 na kwa tafiti za “PhD” tungepata US dollars 20,000 na kwa hivyo wengi wetu nikiwemo mimi tukachagua tafiti bila kuogopa sana gharama zake bali tuliangalia zaidi manufaa ya kielimu na manufaa kwa taifa letu.
Tumemaliza mwaka mmoja wa masomo tukijiandaa kisaikolojia na tukiendelea kuandaa mapendekezo ya tafiti bila shida yoyote. Lakini ghafla tunaambiwa “maagizo toka juu” yamebadilisha kiwango cha malipo ya tafiti na hivyo zaidi ya nusu ya pesa tuliyotegemea haiji.
Je, ndivyo tunavyotakiwa kuzoea uendeshaji wa mambo yetu katika taifa hili? Hili jambo limetufanya tujihisi wanyonge na hatuheshimiki kabisa. Kwa nini maamuzi yasingekuwa ya taratibu na pia taarifa rasmi itoke ikiwa na orodha ya sababu zilizofanya mabadiliko yatokee?
Sisi sio wajinga na tunajua dhamana ya utumishi na hatusahau maneno ya busara ya Mwalimu Nyerere alipotuasa Watanzania na haswa watumishi kwa ujumla kwa kusema endapo tutadai maslahi sawa na maslahi wanayopata wenzetu katika mataifa yaliyotuzidi kiuchumi basi sisi tutakuwa wasaliti.
Lakini mradi wa HEET kama ulivyokuja na muongozo basi na mabidiliko yake ni vyema yakaja na sababu ili sisi tusijeanza kuhisi kuna rushwa na ufisadi ndani ya zoezi la kuendesha mradi huu.
Mnatuathiri kisaikolojia watumishi wa umma na pia hii dharau sio rahisi kuisahau, ndiyo mambo kama haya yanawajengea watumishi roho mbaya na wao wanalipiza kwa wanaodhani ni wanyonge wao pia! Aibu inakuwa ya taifa na taasisi zake.
Hakuna namna bora ya kueleza jinsi tunavyojisikia lakini tunaomba majibu yatakayoridhisha ili tupate moyo kwamba tunaheshimika pia.
Sote tunakumbuka jinsi gani Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana alionesha furaha na maneno aliyoyasema katika uzinduzi wa mradi huu. Isitoshe alisisitiza kwamba pesa zipo na wakuu wa vyuo na wasimamizi wahimize watumishi kusoma hata vyuo vya nje kuongeza maarifa na "exposure".
Tuwaelewe vipi? Tunaelewa vizuri utofauti wa ahadi ya malipo ya US dollar 20,000 na kulipwa shilingi za kitanzania milioni 20? Utofauti wa ahadi ya US dollar 10,000 na kulipwa shilingi za kitanzania milioni 10? Alafu ghafla tu bila maelezo yoyote zaidi ya "maagizo kutoka juu"?
Kwa niaba yangu na wenzangu naojadili nao sikitiko letu, naomba kuwasilisha na tunaomba utusaidie kutupatia majibu ya mabadiliko muhimu kama haya.
Kwa muda huu tupo njia panda kama tuendelee na tafiti zetu bali tupunguze malengo au tuanze kupendekeza tafiti mpya ambazo gharama zake ni ndogo hata kama hazina “impacts” moja kwa moja kwa jamii yetu ya watanzania na katika elimu kwa ujumla wake. Madhara ya hatua za namna hii ni mengi na sitaweza kuorodhesha yote kwa sasa.
Natanguliza shukrani zangu kama nitaeleweka na natoa pole kwa usumbufu wowote utakaopata kutokana na barua hii.
Wako katika ujenzi wa taifa;
Mnufaika wa mradi wa HEET.
CC:
Wasimamizi wa Mradi
Naibu Waziri,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Tanzania.
Ndugu;
YAH: KUKOSA IMANI NA WASIMAMIZI WA MRADI WA HEET (HIGHER EDUCATION FOR ECONOMIC TRANSFORMATION PROJECT)