BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA.
Kabla ya yote napenda kukupongeza kwa majukumu mazito ya kuongoza taifa katika misingi thabiti, angalau nidhamu kama taifa inaonekana wazi,
. umekemea ufisadi
.umeimarisha ulipaji modi
.nidhamu kwa watumishi wa umma
.utendaji thabiti kwa watumishi na mengine mengi sana, na hasa yale ambayo hayahitaji fedha, ambayo yalihiraji usimamizi tu.MUNGU AKUBARIKI NA AKUTIE NGUVU ZAIDI
Baada ya hayo mheshimiwa ninaomba ninene neno moja maana nchi yetu inaruhusu watu kuelezea hisia zao.
Mheshimiwa sisi kama taifa ni kama mtoto aliyedumaa, ambaye amejifunza kutembea akiwa na miaka 20 ,hivyo anatamani kila kitu afanye hasa vitu ambavyo vinafanywa na watu wa rika lake.
Ni kweli ni haki kufanya hivo lakini sio busara maana atapata tabu na pengine anaweza kushindwa vyotee .
sasa sisi kama taifa
NI KWELI Tanzania ni taifa kubwa na sio changa
NI KWELI tunahitaji maendeleo ya haraka
NI KWELI tuna rasili Mali nyingi sana na tukizitumia vizuri, baada ya miaka kadhaa tutaku tunaongea hadithi zingine
NI KWELI viwanda vinaharakisha maendeleo ya nchi
NI KWELI tunahitaji ndege za kisasa, treni za kisasa nk
NI KWELI tunahitaji umeme wa uhakika
LAKINI
SI KWELI kua tutaweza kufikia malengo yote hayo kama hatutakua na mpango endelevu na thabiti katika
.ELIMU
.AFYA
.CHAKULA
Mheshimiwa kwanini tusianze kwa kutambaa hivo hivo, kwakua tumekua wakubwa basi tutatumia muda mfupi.
(1. TUWEKE AKIBA YA CHAKULA HASA NAFAKA
2.KUWEKA BEI NAFUU YA VYAKULA
3.UJENZI WA MAGHALA YA NAFAKA KILA WILAYA
4.KUPUNGUZA KODI ZISIZO ZA LAZIMA KWENYE NAFAKA
5.BEI ZA UHAKIKA ZA KUNUNUA MAZAO KWA WAKULIMA
6.KUHAKIKISHA PEMBEJEO ZINAPATIKANA KWA UHAKIKA)