Barua ya ushauri: Freeman Mbowe omba msamaha ukajipange na maisha mengine

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
372
505
KWAKO F.A MBOWE
S.L.P GEREZANI


Nianze kukupa pole na hongera gerezani siyo mahali salama na pazuri kwako.

Nianzi kwa kusema ..

Leo kuna kitu nimejifunza juu ya utatuzi wa migogoro hasa katika kipengele cha CONFLICT MANAGEMENT
Ili uweze kuendelea na maisha ya furaha pasipo karaha muda mwingine hata kama siyo mkosaji kuna hatua unatakiwa ufanye two side reconciliation ambapo utachagua wewe kulingana na uhitaji, mahesabu ya faida na hasara, thamani ya muda. Uamuzi unaohitajika hapa ni WIN WIN SITUATION ( BARGAINING RESOLUTION pata na Mimi nipata

Lakini pia nilisoma hadithi Fulani kama siyo kuhadithiwa kwa kifupi iko hivi:-
Palikuwa na miji miwili Iliyo tenganishwa na MTO mkubwa mahitaji yote ya muhimu hospitali, shule, soko, stand za magari, bar , maduka yalikuwa upande wa pili yaani Mji B,
Hapo penye MTO hapakuwa na daraja hivyo alitokea MTU mmoja mwenye hela , mamlaka akajenga daraja akaweka masharti

Sharti la kwanza akamuweka mbwa pale darajani kila anayepita lazima amsalimie mbwa SHIKAMOO anaruhusiwa kupitia

Sasa Siku moja Msomi mwenzangu akawa hataki na wala hajawai kukubalina mambo ya shikamoo kwa mbwa nikweli ni dharau akijiona ni popular ,msomi wa chuo kikuu Ila Siku moja mke au mtoto aliugua karibu kufa na huduma zote zipo ng'ambo Mji B kikwazo ni mbwa kusalimiwa Shikamoo akaenda atumie nguvu mbwa yule alimjeruhi saana
Watu wakamshauri msalimie tu uvuke akasema siwezi na Kule nyumbani akapoteza Mama mzazi,Mke, Mtoto wake pia akafa kwa kukosa matibabu lakini kizuizi ni mbwa baadaye sikumbuki kama alimsalimia au alika Mji A milele au laa just to make short

Ukirejea stori hapo juu nikuwa funzo kubwa ni
UNAPO TAKA KITU FAIDA, MAISHA, N.K TUNALAZIMIKA KUJI SACRIFICE ILI upate kile unacho kitaka kwa hali na mali

Yesu kristo alikuwa mtakatifu lakini alitukanwa, akadharauliwa, akasulubiwa kwa kuitwa mwenye dhambi mwisho alifikia lengo LA UKOMBOZI WA ULIMWENGU.

KAKA ,BABA, BABU,KIONGOZI ,MVIP, MZAZI WANGU KILA MAZINGIRA YANAONEKANA YESHAKUWA MAGUMU KWAKO KUWA HURU, SASA, FANYA MAAMUZI MAGUMU, TU JITOSE OMBA USAMEHEWE TU BURE NARUDIA BURE UJE URAIANI UFANYE MAMBO MENGINE,

NAOMBA SIKIA USHAURI WA FAMILIA MMOJA MOJA ,najua kuna mgawanyiko katika mawazo ya watoto, chama na viongozi wenzio, POTEZA 30 UPATE 70
MTEGO UMETEGWA NAWE HAUWEZI KUKUNASA ILA UTAKUZUIWA NA KUKUUMIZA KWA MUDA MREFU SAANA,
JIPE MUDA WA KUTAFAKARI KUSHINDA UTASHINDA LAKINI TO THE LAST DROP OF BLOOD UTAKUWA UMECHOKA

NI USHAURI TU JAPO WENGINE WANASEMA UKIOMBA MSAMAHA YATAKUKUTA YA JOB NDUGAI MMMMMM!!!! LABDA WANADAMU SIYE HATUTABIRIKI

Wengine wanahisi ukiomba msamaha ndo utakandamizwa kwa kuwa ni kama umekiri kutenda kosa

Kaa na mawakili wako mjadili kisheria itakaaje ILI uwe safe side.
Nawewe ni political trap wasipo kuachia baada ya Ku compromise mtego utawafyatua wao 2025.

Huo ni ushauri wangu kwako Mwana siasa mkongwe. Amini hutopoteza saana kama mwishoni kwa kesi yako.

Angalizo kama wao jamhuri imetoa room hiyo nafikiri IPO japo siyo direct OMBA YAISHE BABA.
REJEA HOTUBA MH.RAIS SIKU ZITO KABWE AMEKUOMBEA MSAMAHA

AHSANTE
 
Usifikiri “msamaha“ unakuja bure, akisamehemewa maana yake pia apishe Uwenyekiti kwa Makamu na asi- attack Serikali iliyopo, kwa kifupi aache upinzani awe kama wengine akina Act, Mbowe siyo mjinga kama ingekuwa rahisi kihivyo angeshafanya hivyo!
 
Hivi Kwann imekua hivi? Msamaha how? Jambo lipo mahakamani na kesi inaendelea. Inakuaje yanakuja matamko ya watu mbalimbali juu ya kuomba msamaha kwann? Nadhan ni vzr kila mmoja akae kwa kutulia ili mahakama itende haki kisheria. Hii biashara ya kuomba msamaha kuna kitu hapa.. sio bure!

2923053_E8aqzrqWYAMhHTF.jpg
 
Hivi Kwann imekua hivi? Msamaha how? Jambo lipo mahakamani na kesi inaendelea. Inakuaje yanakuja matamko ya watu mbalimbali juu ya kuomba msamaha kwann? Nadhan ni vzr kila mmoja akae kwa kutulia ili mahakama itende haki kisheria. Hii biashara ya kuomba msamaha kuna kitu hapa.. sio bure!


View attachment 2094230
ushahidi wa yule askari wa uchunguzi, na ushahidi wa gudluck leo unaonesha kesi imeisha na serikali imeshindwa!

wanatafuta namna ya kujichomoa
 
Sema aombe msamaha kwa kosa/makosa gani hasa?
Wenzake anaoshtakiwa nao huo msamaha utawahusu pia?
 
Aombe msamaha kwa kosa lipi? Na sheria zetu zinasemaje kama ukishtakiwa mahakamani, unaomba tuu msamaha yanaisha?? Kuna nini apo??
Rejea ya Rugemalila, Tito, singasinga Ndo serikali yetu ndugu mwenyenhuvu mpishe
 
Back
Top Bottom