Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema barua ya malalamiko kuhusu uteuzi wa viongozi watendaji wa juu na wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliyowasilishwa katika ofisi hiyo na kada wa chama hicho, imewafikia.
Kanda huyo Lembrus Mchome, mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) mkoani Kilimanjaro anapinga uteuzi wa viongozi hao uliofanwa na Mwenyekiti, Tundu Lissu Januari 22, 2025, akidai umekiuka katiba ya chama hicho.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kabla ya kuipeleka katika ofisi hiyo ya msajili, Mchome alipeleka barua hiyo katika ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika jana Jumanne, Februari 18, 2025 akibainisha uteuzi wa vigogo hao uliidhinishwa bila akidi ya kikao cha Baraza Kuu kutimia.
Soma Pia:
Kwa mujibu wa Mchome vigogo waliopatikana katika utaratibu huo ni pamoja na Katibu Mkuu, John Mnyika, Aman Golugwa (naibu katibu mkuu - Bara) na Ally Ibrahim Juma (naibu katibu mkuu - Zanzibar).
Katika barua hiyo ambayo Mwananchi imeiona, Mchome anadai wajumbe wa kamati kuu walioteuliwa na kuidhinishwa na kikao hicho kuwa ni Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ni batili.