Barua kwa viongozi vijana. Badala ya kuiga watangulizi badilisheni mfumo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,429
10,269
Ndugu zangu viongozi na viongozi watarajiwa,

Hii nchi yetu pedwa haitabadilishwa na viongozi wa sasa ambao wamefundishwa kufanya kila wafanyanalo kuhudumia viongozi wenzao badala ya kuhudumia taifa. Viongozi ambao wanafikiria watapata vipi pesa kutokana na kodi na rushwa.

Viongozi ambao wanaona magari binafsi ni bora kuliko huduma kwa jamii. Viongozi ambao wamefanya nchi yetu iwe tegemezi mkubwa kwa misaada ya hata vyakula. Viongozi ambao hawataki demokrasia wakati kama nchi tulisha kubaliana ndiyo mfumo mzuri kwetu.

Viongozi ambao wanatumia pesa za wananchi kuwateka, kuwanyanyasa wananchi. Viongozi ambao wanaona Polisi ni chombo chao na sio cha wananchi. Viongozi ambao wanafikiria kusifiana badala na kubuni mbinu za maendeleo.

Viongozi ambao wanaona vyama vya upinzani kama maadui badala ya wadau wa maendeleo. Viongozi ambao wako tayari kuwauwa watu, kupiga risasi wanasiasa na wengine ambao wanazuia wenyewe na ndugu zao kuendeleza mfumo wa wizi kwa wachache.

Wakati Maraisi wa Marekani waki staafu wanaenda kwa wananchi na kuchangiwa kufungua maktaba ya kumbukumbu za Uraisi hapa kwetu wameona ni vema wajijengee maikulu binafsi tu kwa pesa za umma!. Nchi ambayo wake na wame wa wastaafu wanalipwa kuliko wanajeshi na walimu wastaafu. Nchi ambayo viongozi wanahamishwa wakifanya vibaya na hata wakiiba pesa za umma.

Nchi ambayo wananchi wanapewa maji machafu na viongozi wanataka wananchi wawashukuru kwa maji eti kwasababu ni bahati kupata maji. Viongozi ambao ukienda na suluhisho la kusaidia jamii waziri na viongozi wana angalia kwanza watanufaika vipi. Nchi ambayo viongozi wanajitajirishwa kwa rushwa. Nchi ambayo mikataba ya kimaendeleo na mikubwa kama bandari ni ya siri!. Nchi ambayo misitu inauzwa bila wananchi kujua!. Nchi ambayo bandari na airport zinapata mikataba ya kisiri ili kuchukuwa rushwa.

Ombi letu ni badala ya kuiga mazoea haya mabaya fikirieni tofauti. Inawezekana kabisa Tanzania ikawa nchi yenye demokrasia, ubunifu na isiyo na rushwa kwa kiwango hiki. Tanzania inawezekana ikawa na katiba nzuri ya maendeleo ambayo inajali nchi na sio watu wachache wa chama tawala. Nchi ambayo mikataba iko wazi. Nchi ambayo sio dampo la vitu vya grade ya chini kutoka China. Nchi ambayo Watanzania wote waliopo Dunia nzima wanachangia maendeleo yao bila ubaguzi. Nchi ambayo inaunganisha Watanzania wote bila kujali visiwa, diaspora, kabila wala kanda.

Lazima vijana muelewe hawa wazee wengi waliopo madarakani wanaenda na mazoea ya ubinafsi na hamtaweza kushindana na nchi nyingine kwa katiba hii, mfumu huu wa rushwa na kuiga hawa wazee. Wasameheni bure hawa wazee ambao wamejiaminisha kwamba ni wazalendo wengi wao wanazoea uongo mpaka wameweka imani kwenye uongo na unafiki.

Nchi yetu inahitaji vijana wanao jitambua na sio kudanganywa na bongo flava na michezo wakati wenyewe wanaojua mfumo wanaendela kuiba na kuwaweka kwenye madeni na utegemezi huko mbele. Nawaomba unielewe na kujielewa bila hivyo iko siku mtaamka na kutambua haya yote nayosema hapa. Wengi wenu kwasasa mnatumia na kuendeshwa kama gari bovu jitambueni na amkeni kukomesha mabaya na kusaidia nchi yetu
 
vijana acheni uchawa
 
Back
Top Bottom