Barua kwa Kikwete: Madai ya kuteswa na kudhalilishwa mahabusu

albuluushiy

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
1,404
686
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dar es salaam.

KUHUSU: MADAI YA KUTESWA MAHABUSU WANAOTUHUMIWA KWA MAKOSA YA UGAIDI​

Ndugu Rais,

Nisamehe sana nakuandikia barua ya wazi, lakini mimi raia wako sijui njia nyepesi ya kuwezakukufikishia waraka huu, maana sizijui taratibu
zi lizotandikwa na za wazi za kufanya hivyo. Mheshimiwa Rais, waraka huu unahusu madai ambayo wiki mbili hizi yamekuwa yakiandikwa katika vyombo vya habari kuhusiana na watu kadhaa ambao wako mahabusu kukabili makosa ya ugaidi. Mimi ni katika raia wako wanaopenda mfumo wa sheria ufanye kazi, na ndio maana barua hii si kulalamikia kushtakiwa kwa watu kadhaa kwa wakiwemo wengi kutoka Zanzibar kwa makosa ya
kigaidi. Vitendo vya kigaidi havikubaliki na kwa hakika havichagui wala havibagui na yeyote mwenye kuvifanya, kuviendeleza au kusaidia ni lazima akabili sheria.

Mheshimiwa Rais, najua una wajibu wa kulinda usalama wa nchi ikiwa ni pamoja na raia na mali zao na kwa hivyo wewe ndie muangalizi mkuu wa
sheria za nchi na kuona haki inapatikana kwa kila raia.

Lakini katika kusimamia huko kila mtu atashtakiwa na kukabili kesi yake kwa kiwango cha juu cha heshima na pia kupewa haki ya kuyajua na kujitetea kwa mashtaka ambayo atakuwa anakabiliana nayo. Nchi yetu ina vyombo kadhaa vya usimamizi wa haki kama ambavyo kuna vyombo kadhaa vya ulinzi wa haki zetu na vyote kwa mujibu wa Katiba yetu viko chini yako wewe.

Mheshimiwa Rais, naamini sina haja ya kunukuu vifungu vya haki za binaadamu ambavyo vinampa mfungwa haki hizo na hata kama itathibitika kosa
lake bado chini ya Katiba yetu mfungwa hapaswi kufanyishwa kazi za kutwezwa na za kitumwa. Naamini kabisa unajua kuwa kumekuwa kuna madai ambayo yametoka kwenye vyombo vya habari yanayowahusu washtakiwa katika kesi ya ugaidi ambayo ipo Mahakamani mjini Dar es salaam hivi
sasa.

Washtakiwa hao wamesema Mahakamani kuwa wanateswa kwa njia ya kupigwa, wanafanyiwa vitendo vya kinyama kama vile kutiwa chupa na
majiti sehemu zao za siri. Pia wamedai kuwa hawapati matibabu.

Kwa kuwa madai hayo yametolewa Mahakamani, niruhusu Mheshimiwa niseme kwamba hayawezi kabisa kupuuzwa na itakuwa ni kosa kubwa kwako kuyapuuza.

Ingekuwa vitendo hivyo ni sehemu ya mfumo wa upatikanaji haki, nisingekuwa na sababu ya kuandika barua hii, lakini kwa sababu vitendo hivyo ni
uvunjaji wa haki ya watu waliozuliwa na pia ni uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu, ndio imenilazimu kukuandikia.

Wananchi wako na dunia nzima wanafuatilia juu ya kesi hii. Na habari tunazopata ni hizo za maafisa wetu wa kutulinda kujihusisha na matendo kama
hayo kwa watu ambao wana heshima kubwa katika jamii. Haya tumekuwa tukiyasikia kwengine lakini sasa yapo kwetu.

Leo wapo Mahakamani wanakabili shitaka na kesho wanaweza kuwa wapo nje kwa kutoonekana hawana kosa, jee heshima yao kwa kudaiwa kufanyiwa vitendo kama hivyo itakuwa wapi mbele ya macho ya umma?

Lakini mfumo wetu wa sheria Mheshimiwa Rais unaelekea kufikia kiasi cha kuzama kama hivyo? Hivi inastahili kufanyiana kama hivyo?

Nchi yako Mheshimiwa Rais ni mwananachama wa jumuia zote za kusimamia haki za binaadamu baada ya kutia saini na kuridhia mikataba yote katika eneo hilo, jee huku ndio kutimiza wajibu wetu? Huku ndio kujenga imani kuwa haki za binaadamu na haki za wafungwa zinalindwa?

Kwa fikra zangu Mheshimiwa Rais hili si neno la kupuuzwa. Haya yamelalamikiwa hadharani na washtakiwa lakini wasaidizi wako wote hayajatoa kauli yoyote ile. Si Mkuu wa Polisi, si Mkuu wa Idara ya Usalama, si Mkuu wa Idara ya Magereza. Pia wasaidizi wako Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheri Mkuu, Muendesha Mashtaka walipaswa kutoa kauli juu ya kinachoendelea katika magereza dhidi ya washtakiwa hao kwa kuwa kimelalamikiwa Mahakamani na kwa hivyo kipo hadharani na mbele ya macho ya umma.

Kwa kuwa madai ya kuteswa na kudhalilishwa ni makubwa ni ushauri wangu Mheshimiwa Rais kuona kuwa unachukua hatua ya kuchunguzwa matendo hayo halan, yaani kwa Kiswahili cha kwetu ni kwa haraka inavyowezekana.

Naamini utakuwa na njia zako za kuchukua kwa kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa hatua, ila, la kwangu lilikuwa ni kukuarifu kama ulikuwa hujui,
kukuzindua kama ilikuwa umeghafilika na kubwa zaidi ni kulisema ili kesho na kesho kutwa iwe angagalau sauti moja ilinyanyuka kueleza juu ya
madhila hayo.

Khofu yangu jambo hili lisipochukuliwa hatua kwa kuchunguzwa na wahusika kuadhibiwa ina maana itakuwa tunalilea, na mbali ya kukosa heshima kwa macho ya kimataifa, basi pia itakuwa ni dua kubwa kwa Serikali.

Naomba tena unisamehe Rais wangu lakini roho yangu haingeweza kabisa kulistahamilia hili. Kama ilivyotokea huko Urusi ya Kikomunisti kulikozuka
msemo kuwa usipolisema la mwenzio hakutakuwa na wa kukusema likufikapo wewe.
 
Kama ni kweli yamefanyika hayo, ni mbaya sana ndg. inatakiwa kulaaniwa na jamii yote.
 
Nami nalaani kabisa kwa nguvu zote!kama wamedhalilishwa! Rais aunde tume ndogo tu awape hata week wachunguze! Haki za binadamu kwa wote!
 
Taanzania Tanzania...ilipotokea mauaji ya mwembe chai,, I will never forget 13.2.1998.. pale mwembe chai...waislam walipigwa risasi pasi na hatia, wengine wamepata ulemavu wa kudumu..ilipotakiwa kuundwa tume ya uchunguzi serikali ilisema haina pesa..haikupita siku nyingi serikali ikaunda tume kuchunguza mauaji ya mbwa....
inauma sana..
inauma sana
.machozi ya huzuni kamwe hayatakauka kila nikumbukapo...
hii ya Leo imeniongezea huzuni...aaahh! ! ..nothing to say...mana hakuna wakujali kilio hiki....
 
Taanzania Tanzania...ilipotokea mauaji ya mwembe chai,, I will never forget 13.2.1998.. pale mwembe chai...waislam walipigwa risasi pasi na hatia, wengine wamepata ulemavu wa kudumu..ilipotakiwa kuundwa tume ya uchunguzi serikali ilisema haina pesa..haikupita siku nyingi serikali ikaunda tume kuchunguza mauaji ya mbwa....
inauma sana..
inauma sana
.machozi ya huzuni kamwe hayatakauka kila nikumbukapo...
hii ya Leo imeniongezea huzuni...aaahh! ! ..nothing to say...mana hakuna wakujali kilio hiki....

inauma wallah
 
Unyama umefanyika na makubwa tutayasikia. Kitakachokuja tutaambiwa madai hayo ni ya uongo na blah blah nyingi tu! Ila kwa mfumokristo muislam hana haki!
Mfumokristo Kikwete mwenyewe umembana vilivyo hata hapumui, unadhani mashekhe wetu watapewa haki? Zaidi tutasikia wamepelekwa Marekani kwa uchunguzi zaidi! Bado hatujamsahau Ghailan! Mengi na makubwa yatafuata baada ya awamu hii ya Kikwete.
 
Kama ni kweli wamefanyiwa hivo haki inahitaji kutendeka na ionekane imetendeka, na pia kesi yao ya ugaidi iendelee kama kawaida kitu hiki isiwe kigezo cha kukimbia tuhuma za ugaidi!

hawana lolote hao, wanapoua na kutesa mapadri kwao ni sawa,ila kwao wanaandika hadi barua hekoo polisi,magaidi hawana nafasi. wamechoma kanisa la temeke wamesababisha hasara kiasi gani?wameua padri mushi huko zanzibar wanadhani tumeyasahau?wamemumwagia tindikali padri huko zanzibar wamesahau?hapo mto wa mbu arusha walimchoma kwa misumari mchungaji aliyekuwa anahubiri wanadhani tunafuraha nao? wamelipua kanisa la olasit arusha na kuuwa waumini na kusababisha majeraha na yatima wengi leo wakamatwe wanaodaiwa kuwa ni wahusika halafu we raia mwema uwe na huruma nao?mi nasema wapigwe na wabanwe hadi huo mtandao wao wautaje wote.wanajisingizia kuteswa ili waonewe huruma nasema hakuna.mchuma majanga hula na wa kwao.wakae kimya.
 
Gaidi huwa hana haki kama mfungwa wa kawaida. Jifunze kuhusu wale magaidi wa kule Guantanamo Bay Detention na ile kitu wanapewa ya Waterboarding.
 
Unyama umefanyika na makubwa tutayasikia. Kitakachokuja tutaambiwa madai hayo ni ya uongo na blah blah nyingi tu! Ila kwa mfumokristo muislam hana haki!
Mfumokristo Kikwete mwenyewe umembana vilivyo hata hapumui, unadhani mashekhe wetu watapewa haki? Zaidi tutasikia wamepelekwa Marekani kwa uchunguzi zaidi! Bado hatujamsahau Ghailan! Mengi na makubwa yatafuata baada ya awamu hii ya Kikwete.
Unyama kwa Gaidi, you must be kidding me. In fact, TZ needs to be like China and wipe those people out of the surface of earth.
 
An eye for an eye will make the whole world blind. Vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa watuhumiwa havikubaliki na mtu yeyote wa imani yoyote. Rais kama unasikia haya, hatutakushangaa usipoyafanyia kazi. Nilishangaa sana kuwa hata hakimu riwa hakuongelea hili.
 
wasilamu wafanywee tu wanatakakutuharibia nchii,raisi musilamu mwenzao ila hawahurumii wala kuwavumilia wavunjifu amani
 
“Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe”
“Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya”
Asaalaam Alaykum, mpenzi msomaji. Nadhani nilichokiweka si matusi na wala sikupaswa kupunguza ukali wa neno hata moja nami sijafanya hivyo, kwani kufanya hivyo kungepoteza maana ya kile ambacho binaadamu wanatendewa.
Ikiwa umelipitia gazeti la Mtanzania la Ijumaa, Aug 22nd, 2014, basi utakutana na habari yenye anuani; Watuhumiwa wa Ugaidi wachafua hali ya hewa kortini.Ndani ya habari hiyo ndio utakuta mengi ya kuhuzunisha na kuumiza na baadhi yao ndio hayo niliyoyanukuu katika aya ya mwanzo na ya pili.
Ni malalamiko ya mshitakiwa wa 12 Salim Ali Salim, akiwa naye ni mtuhumiwa wa ugaidi akilalamika katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa juu ya kutendewa uovu na Jeshi La Polisi.
Kuna mambo ya msingi tuwe tunayasema ikiwa ni njia moja wapo ya kulainisha nyoyo za hawa wanowatendea uovu wanaume wenziwao.Napenda sana kusema kuwa,ukitaka kumfanyia mtu uovu hebu jiulize mimi nikifanyiwa nitaridhika? Ama Mama yangu na Dada yangu na Baba yangu akifanyiwa kama hivi, jee mimi nitakuwa radhi?
Baba wa mtu,Kaka wa mtu, unamfanyia unyama. Sababu una uwezo wa kufanya hayo, sitaki kuamini kuwa sheria inawaruhusu kuyatenda hayo wayatendayo. Ila wanajiona na nguvu kwa viumbe wenziwao ndio wanaamua kufanya.
Si suali dogo endapo mwenye akili ataliweka kichwani kisha akalizingatia pia ni kipimo kizuri cha kumtendea wema au uovu binaadamu mwenzako.Nikifanyiwa mimi? Mama,Kama,Dada inaumizaje? Ikiwa ni wenye kufikiri!
Nilipokuwa naisoma habari hii, ukweli nimeumia sana sana. Munaingizana chupa na majiti sehemu za siri? Kwa lipi hata umfanyie binaadamu mwenzako yote hayo? Ukweli inasikitisha lakini kuna siku kila mchunga ataulizwa juu ya alichokichunga.
Wakongwe wa hii tasnia ya habari, walishawahi kuuliza;Wako wapi watesa na wateswaji? Jeuri ya binaadamu ni hii Oxygen kutoka kwenye miti, ambayo Mungu kaiweka huru kwa wababe na wanyonge, ila siku Oxygen ikikatishwa kwako,hapo ndio utaelewa. Ubora na ubaya wa uliyoyatenda.
Unapomsikia mtu mzima anaomba daktari wa kungalia afya yake, au akakubali kuangaliwa jinsi alivyoharibiwa na mwanaume mwenzake. Hii inatoa tafsiri ya kuwa huyu mtu kafikwa na yaliyomfika si madogo, ni makubwa mno.
Wakati napitia maoni ya wasomaji wa taarifa hii kupitia mitandao ya kijamiii, wengi wao walionekana kukata tamaa na kushindwa hata kutoa maoni nini kifanyike. Ila walichokuwa wakikisema zaidi ni kumuachia Mungu, yaani wanaonekana dhaahiri wamekosa lakufanya, ila mmoja wao aliandika hivi:
“Haya ni makosa ya wanaojiita viongozi wa Zanzibar ambao wao wamezowea kudhalilishwa nao wanawadhalilisha watu wasio na hatia yoyote, kama kweli Zanzibar ni nchi ina Rais ina Mwanasheria Mkuu ina Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahkama zake inakuaje aje kuchukuliwa mwananchi kupelekwa nchi ya pili na huku kuna amri ya Mahkama kuwa asitoke nje ya Zanzibar bila ruhusa ya Mahakama, leo anachukuliwa kwa kisingizio cha Muungano, ipo wapi hadhi ya Mahkama Kuu ya Zanzibar?
Nirudie kusema kuwa kila mtu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga. Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Shein umejitwika majukumu ya kuwa mchunga wa Wazanzibari wooote, hili halipingiki na hata ukikataa ndio litabaki hivyo.
Watu wako umeruhusu waondoshwe nchini mwako na wende kuigiliwa na wanaume wenziwao? Jibu Mheshimiwa. Wewe ni Muislam na kama uliishi Chokocho au mahali pengine popote ila tu ulipitia Chuoni (Madrasa). Hii ni kama desturi ya watoto wa Kizanizbar. Sasa utakuwa tu unakumbuka baadhi ya aliyokusomesha Mwalimu wako wa Chuoni huku mkono wa kulia kakushikia mbungo au mpo nzuuri, ni miaka hiyo mingi iliyopita.
Quraan na Hadithi nyingi husomeshwa, ila mimi nataka nikukumbushe haya maneno kuwa “Kiila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga” Huenda umeshasomeshwa umesahau tu, ila ulikula fimbo nyingi kuyaelewa mambo kama hayo.
Sijui historia yako vizuri utanisamehe ila cha msingi ni kuzidi kukukumbusha haya maneno, kuwa wewe ni mchunga na tambua kuwa utaulizwa juu ya Wazanzibar wote, kama huji hilo basi kuanzia leo kaa ukitambua kuwa mbele ya Mungu utakwenda kuulizwa kwa kila Mzanzibar ulimchunga vipi.
Upo umuhimu wa kutii uwongozi wako, lakini pia nasi tunalojukumu la kukukumbusha moja ukiwa kama Kiongozi wetu na kubwa zaidi na la kwanza kuwa ni Muislam mwenzetu.
Nimeumia sana kuyasikia haya na nina masual megi kichwani .Jamani haya ndio matunda ya Muungano. Mashekhe zetu wanafanywa mashoga kule Tanganyika.Dokta, atakaye kukumbusha majukumu yako juu ya wachunga wako ni sisi.
Kuntusikia hewallah, laa twaporoja tunshiba sheli sheli la Mjimbini na pembe pia nsawaa. Masheikh wanaumizwa, wanadhalilishwa, wanazungumza kwa uchungu Rais Jakaya nawe pia ni mchunga na dhulma wanazofanyiwa waja utakwenda kuulizwa, baaada ya hawa wafanyaji kuulizwa itakuwa zamu yako.Hili halipingiki wala kuepukika, ruka ukitoja ukweli utabaki hivyo hivyo hata karene 21 nyengine zijazo.
Mimi nipo kuwakumbusha akhera zaidi kwani kule ndio kuzito na maandalizi mazuri ya kule huwa yapo hapa duniani. Mashekhe wanavuja, wanaumizwa, wananajisiwa.Haki zao zimekiukwa na wewe ndiye Mkuu wa kila kitu kwa hapa kwetu. Wanaongea kwa uchungu sana.
Msikilize Sheikh Faridi kwa huzuni kubwa anasema:“Mheshimiwa wametuomba kwenda kutuhoji tena, mara ya kwanza tulipohojiwa, polisi hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu, ni ushenzi na ukatili, walituhoji uchi wa mnyama na kutupiga.Watu wameumizwa vibaya, mengine hayasemeki, wanajisaidia haja ndogo damu wiki moja hadi mbili, tunaomba tufanyiwe uchunguzi wa afya zetu, ipo siku mahakamani italetwa maiti”
Hata wakiwa na tuhuma za Ugaidi lakini si haki kufanyiwa hayo. Ni kukiuka haki zao na wala mtu hahojiwi kwa njia hizo. Wala ukweli hautafutwi kwa kuvunja haki zao.
Umeshawahi kumuona Ngo’mbe akimuingizia Ng’ombe mwenzake jiti katika sehemu za siri? Watu wanadhalilishwa jamanaiii.Watu wanaingiziwa! Haki zao ziko wapi? Ndio watu wanavyohojiwa hivi? Hizi ndio faida za Muungano ee!!
Watu wanachukuliwa tu kinyemele nyemela, kisha mambo wanayoenda kufanyiwa hata hayasemeki. Serekali yetu ipo, imekaa tu ndio Muungano huo. Muungano wa kutiana majiti na chupa mpaka wakakojoa damu na kuvuja kama Kistula. Duuuh!!
Siku zote sisi tutafanya uwezo wetu na tutakapo shindwa basi tutamuachia mwenyewe Allah (sw). Hata Allah anajuwa kuwa wale ni waja wake watukufu, waliokesha usiku wa Ramadhani kutafuta radhi zake, kisha wakajitahidi kufunga mwezi mzima na sita yake,wengine ni Mashekhe wanaotegemewa hapa nchini katika fani mbali mbali za Uislamu pia ni khamsu swalawati wale.
Yaarabi, wanavyojitahidi vyoote hivyo kukutumikia lakini wapo pia waja wako Majeuri kama Firaun, wanawageuza Kaumu Luut,wanawaweka uchi wa mnyama bila ya ridhaa zao,wanawapiga na kuwanyanyasa. Sikia kilio chao na pia kilio chetu. Wewe ndie mbabe kuliko wababe, tunakuachia kazi hiyo.
Uliwafanyaje Kaumu Lut,ulimfanya nini Firaun aliyewatesa watu wa Mussa. Uwezo wetu umekuwa mdogo juu ya hili,tusaidie kutuondoshea idhalali hii. Wakinge wao na sisi kama ulivyoikinga nyumba yako Al Qaaba wakati inataka kubomolewa kisha ukawaangamiza wote, tunaomba fanya hivyo pia kwa wanowadhalilisha waja wako wema. AAMMIN.
 
Back
Top Bottom