KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 72
- 133
Ingawa viongozi wa Mkoa na Wilaya hawataki kutoa taarifa kwa jamii juu ya uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu.
Ni kuwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu imekubwa na visa wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu.
Kata ambayo inatajwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo ni Kata ya Buhnamala, kwenye mitaa ya Majaida na Imalilo.
Kwa mujibu wa viongozi wa mitaa hiyo (hawakutaka kutajwa majina) wameeleza kuwa zaidi ya wananchi 10 mpaka sasa wamepata dalili za ugonjwa huo.
“ Timu ya watalaamu wa Afya Halmashauri wakiongonzwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri imeshinda huku kwenye mtaa wetu, hali kwa kweli ni mbaya sana, wananchi kama wanne leo hivi walihisiwa kupata ugonjwa huu”
“Walikimbizwa Hopsitali na siwezi kusema moja kwa moja kama ni Kipindu Pindu, kwa sababu Madaktari hawajatupatia majibu ya vipimo kwa wale ambao wamehisiwa, lakini kwa jinsi nilivyowaona walikuwa na dalili zote za kipindupindu, na ninaweza kusema ule ni mlipuko wa Kipindu pindu”
Siku chache zilizopita walihisiwa wananchi wengine watano, wakapelekwa Hospitali na wakapatiwa matibabu na sasa hivi wanaendelea vizuri, Lakini ni kipindupindu sema tu viongozi hawataki kusema Lakini ni kweli hata hawa waliotibiwa waliambiwa kuwa ni Kipindupindu.
Kwa sasa wananchi wa mitaa hiyo wameingiwa na hofu kubwa, kwani visa vingi vimetokea mitaa hiyo, huku mtaa wa Imalilo ukidaiwa kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha ugonjwa huo.
“ Imalilo ndiyo hatari zaidi kwa sasa, visa vingi vimetokea huko, wengi ambao wamepata ugonjwa kwa mtaa wa Majaida walitokea Imalilo na kusambaza ugonjwa huo kwa wengine”
“ Kwa sasa tunaishi kwa woga sana, na chanzo cha ugonjwa huu ni maji ambayo wananchi wanatumia, hii mitaa haina maji safi na salama, wananchi wanatumia maji ya kwenye madimbwi.
Hata hivyo Viongozi wa Wilaya na Mkoa, mpaka sasa wajasema lolote wala kutoa taarifa ili kuwajulisha wananchi kuweka tahadhari dhidi ya ugonjwa huo. Jambo hili limelalamikiwa sana na wananchi wa mtaa mitaa hiyo pamoja na Wilaya kwa ujumla.
Soma Madai ya Mlipuko wa Kipindupindu Simiyu, RC asema ‘Ni Ugonjwa wa Matumbo, tumewapiga faini Wananchi wasio na vyoo’