Ngufumu
Member
- Dec 29, 2016
- 24
- 42
TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL (TNMC)
Kwanza Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwakumbusha wauguzi na wakunga wajibu wao, nadhani ni vizuri na nyie kama chombo kinachosimamia taaluma mkakumbushwa wajibu wenu
1. (a). Nyie mpo kwaajili ya kuhakikisha umma unapata huduma zilizo bora kutoka kwa wauguzi na wakunga hivyo nyie ni chombo cha umma kwa asilimia kubwa na kwa mantiki iyo mnapaswa kuendeshwa/kulipwa na umma
inakuwaje sasa mnawakandamiza haohao Wauguzi Wakunga kuendesha Baraza lenu kwa kuwatoza fedha Kila wanapohuwisha leseni zao na hii mmeweka mda mfupi(Kila baada ya miaka mitatu) mbali na hilo mnachukua fedha za mitihani wawapo vyuoni kwaajili ya kugharamia Mtihani wa leseni kwanini haya yasiwe malipo ya leseni miaka yote mtu awapo mwanataaluma?
(b). Kila kukicha mnawaza kumpiga huyu Mwanataaluma/mtarajiwa wa fani hii kwa kumuongezea garama za maisha(mnabuni miradi yenu na target yenu ni kuchukua fedha kidogo aliyonayo huyu Muuguzi na Mkunga) Leo mnakitu mnakiita Indexing number(usajili wa awali)
je mnaweza kutuambia iyo elf30 wanayotakiwa kulipa wanaotoka vyuoni ili wapate namba(indexingnumber) inawasaidia nini katika kuongezea ubora wa kutoa huduma kwa jamii? Mnawapiga na mnawakosesha Imani juu yenu
(c) Wizi mwingine upo kwenye kutoa leseni huu ni uhuni wa waziwazi kwa wale wanaojiendeleza kutoka ngazi Moja kwenda ngazi nyingine mfano EN anayejiendeleza Ile awe ANO anakuwa na leseni ya EN ambayo inaisha mda wake pengine mwaka ule ambao ndo anahitimu ili apande daraja kwa kupata leseni nyingine ya ANO chaajabu Ile leseni ya ANO ambayo ametoka kusoma inakuja na muda uleule(unaokaribia kuisha/ulioshaisha) uliokuwa kwenye leseni ya EN,
yaani mtu ana elimu mpya lkn Leseni yake inatoka imepitwa na wakati anatakiwa Kurenew, yaani haingii akilini mtu ametoka kulipia Mtihani wa leseni 150k(2021) amefanya Mtihani huo 2021 amefaulu leseni inatoka 2022 na inaonyesha inaExipire 2022 hivyo anatakiwa kuRenew leseni 60k mwaka huohuo huku ni kuwaibia wanataaluma wenu huu ni ukandamizaji tena hata huruma hamna badilikeni!
2. (a). Moja ya jukumu mlilo nalo ni kumshauri Waziri wa afya kuhusu maswala muhimu yanayohusu Uuguzi na Ukunga bila shaka mnajua mzigo ambao hawa watu wamebeba kwani takwimu zinaonyesha 60%-70% ya kazi zote Hospitali hufanywa na wao na Tanzania Kuna uhaba mkubwa karibu Kila ngazi ya vituo vya kutolewa huduma za afya kwamaana nyingine ni kwamba hawa watu wenu wanafanya kazi nyingi na ngumu pia katika mazingira magumu na mara nyingi kazi zisizo zao ili kufidia upungufu uliopo(Hawa tuwaite zoazoa maana Kila kazi ikikosa muhusika watafanya iwe usafi, udaktari, maabara, ufamasia, na uuguzi + Ukunga wenyewe kama huamini nenda zahanati za vijijini huko)
Lakini ujira wanaopata ni mdogo sana na hii inawapelekea wengi wao kuishi maisha yasiyo na furaha kutokana na ukali wa maisha unachaongiwa na kipato duni na stress za kazi, hali inayopunguza mostisha ya kufanya kazi kwa weledi, je huwa mnatetea maslahi yao kwa Waziri na Mamlaka zinazohusika? Kama jibu ni ndiyo mnaweza kuthibitishaje hili? Na ni hatua ipi hasa imefikiwa ya maboresho ya maslahi yao so far?
(b) Kuna kitu binafsi nakiamini japo sijafanya utafiti wa kitaalam kabisa kuthibitisha lakini naamini ukifanyika utafiti Leo juu ya matatizo mengi wanayoyasabisha Wauguzi na Wakunga katika kutekeleza majukumu yao yawe ni ya kinidhamu au umahiri katika kazi chanzo cha hayo matatizo ni malipo duni/hafifu na yasiyokidhi haja za hawa watu, usipomlipa mtu vizuri usitegemee afanye kazi vizuri, anapata wapi huo moyo kwamfano?
Wangelipwa vizuri ni hakika kabisa 60%-90% ya malalamiko juu yao ingepungua kusingekuwa na taswira mbaya juu ya taaluma hii kama ilivyo sasa, kuendelea kuwalipa chini ya kiwango ni kuzalisha tatizo la rushwa na huduma zisizozingatia utu na ubora, japo hata wanaotoa huduma hizo mara nyingine hawajijui kama wanakosea ila mazingira ambayo mnawaweka yanachochea kufika huko, Fanyeni tafiti namna malipo duni yanavyoweza kuharibu ubora wa taaluma na taswira yake katika jamii.
(c). Kuna kauli mnapenda kuzitumia sana mnapokuwa mnaongea na watu wenu, mnawaasa kufanya kazi vizuri kwani watalipwa na Mungu kwa wakati wake/ Uuguzi na Ukunga ni kazi ya wito, ni kweli ni vizuri kukumbushana kwamba Mungu ndiye mlipaji wa matendo mema,
lakini na sisi tunaomba tuwakumbushe tu mnapokaa kwenye viyoyozi hapo ofisini, mnapoenda kwenye vikao, na mnapozunguka kuendesha mafunzo huwa hamlipwi na Mungu mnalipwa fedha tena na Serikali na kwa wakati, kwaiyo na Watu wenu wanastahili kulipwa Ujira mzuri kwa fedha halali za malipo kutoka benki kuu ya Tanzania tena kwa wakati. Mungu atalipa Yale ya sirini
(d) Kuna Mkurugenzi mmoja wa Tnmc(maadili...) hupendelea kusema ametembea wizara na taasisi nyingi na kwakweli watu wengi wakubwa wanaofanya kazi mule wengi wao ni watoto wa Wauguzi na Wakunga akadai haya ni malipo ya Mungu kwa watu wake kwa kazi nzuri walizozifanya ni kweli hatukatai inawezekana kabisa
lakini nafikiri na sisi tumeona watoto wa mafisadi wakikalia nafasi kubwa tu katika taasisi nyeti(tena ni wengi mno mjini tunasema wenyewe Wana Connection) lakini pia tumeona watoto wa Wauguzi na Wakunga wakikosa ada na kuyumba kimaisha na Bado Mungu anabaki kuwa Mungu,
wakianza kudai maslahi yao msianze kusema “hakuna mtu anayeweza wakuwalipa kwa kazi nzuri mnayofanya kwa jamii mtalipwa na Mungu tu” Mungu awatumie nyie(serikali na Wadau Binafsi) basi kuwalipa kwa kiwango chenye staha na heshima kwa utu,
wakati Wabunge wanaye anayewalipa mshahara mzuri tu na Kila kikao wakikakaa posho 360,000 na miaka mitano tu Kiunua mgongo zaidi ya Milioni 250, Wauguzi na Wakunga wanapiga kazi miaka 30+ anatoka hapo na matatizo ya mgongo(wauguzi wengi ndo matatizo yanayowapata) anakuja kukutana na Kikokotoo Cha ⅓ anapewa milioni30 akafie mbele.
3. Mara nyingi mmekuwa mkiwakusanya Wauguzi na Wakunga kwaajili ya Semina na mafunzo mbalimbali bila kuwalipa chochote ilihali ninyi wakufunzi kutoka Tnmc/wawezeshaji nalipwa/mnajilipa je hamuoni nyie ni wabinafsi na watu wakwanza msio na utu maana hamjali mda Wala garama wanazotumia watu wenu kuja kuwasikiliza,
hapa najua mtasema hamna fungu la kuwezesha kuwalipa angalau nauli lakini tuambieni tu hivi pesa mnazo kusanya kutoka kwao mnapeleka wapi? Wahisani nao hamuwezi kuwafikia na kuwatumia kugharamia haya?
4. Msione ukmya wa Wauguzi na Wakunga mkadhani utadumu ipo siku watachafua hali ya hewa Nchi hii na hapatakalika, fikiria tu wakiamua kugoma kushinikiza maslahi bora kwao nani atabaki salama ikiwa 60%+ ya kazi za mahospitali hufanywa na wao? Maana yake 60%+ ya wagonjwa watakosa huduma ni heri muwasikilize mapema na kuboresha maslahi yao kabla joto la hasira linalofukuta mioyoni mwao halijapanda zaidi,
Wauguzi wanafanya kazi 24/7 hawana sikukuu, weekend wala usiku wao ni muda wote wapo kazini lakini hawapewi allowance zozote za maana, watu wanaofanya kazi Tamisemi kwenye Zahanati, vituo vya afya na hospitali wanaingia Night shift na hawapewi night shift allowance, wanafanya kazi hatari hatari lakini hawapewi risk allowance, wanaingia zamu weekend na siku za sikukuu tena wanafanya masaa hata 12 au zaidi sababu ya uhaba na hawalipwi overtime, ila nyie mmekalia tu kutafuta makosa yao mema yao hamyaoni!
Wauguzi na Wakunga wengi wanaacha au wanahama fani zao kabisa maana hawaoni mtetezi kila mtu akisimama ni kuwaponda tu hakuna wakuwafuta machozi mtakuja kushtuka kwenye database yenu mmebaki na Wauguzi wachache sana kwani wengi wanapenda kujiendeleza nje ya uuguzi na ukunga hasa wale wenye elimu za Diploma ili kujiepusha na kazi hii ya lawama tu kila kukicha,
mjitafakari maana mnapoteza watu ambao wameandaliwa tena kwa gharama kubwa ili kusaidia jamii kwasababu ya kutokuwajali na kuwathamini kazi yenu kuwaponda tu kila siku kuonyesha ubaya wao bila jema lao.
Kaulimbiu zenu zilizoboreshwa kuakisi uhalisia hizi hapa
“Watu Maalumu, kazi Maalumu kwa malipo duni”
“Muuguzi na Mkunga Tarajio la Huduma Bora kwa jamii bila Maslahi Bora Haiwezekani”