Baraza la vyama vya siasa Nchini, kukutana kuijadili Zanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,859
Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Peter Kuga Mziray amesema wanajipanga kukutana na kuitisha baraza la mashauriano baina ya vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC wakati wowote visiwani Zanzibar kwa ajili ya majadiliano.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Peter Kuga Mziray.

Mziray amesema hayo kupitia kipindi cha HOT MIX kinachoruka EATV, na kuongeza tayari walishatoa muda wa kutosha kwa vyama vya CCM na CUF kutatua tatizo hilo kwa amani na maelewano lakini vimeshindwa kutumia busara kumaliza tatizo hilo.

Aidha Bw. Mziray ameongeza kuwa imewalazimu baraza hilo kuingilia kati suala la utatuzi wa mgogoro huo baada ya kuona mvutano ukizidi bila ya kupatikana suluhu kwa wakati muafaka hivyo watatoa mapendekezo ya kutatua tatizo la mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa baraza hilo la usuluhishi linaundwa na vyama vyote vyenye usajili nchini ambalo litazingatia zaidi maslahi ya taifa kwa ujumla na kukuza demokrasia ya Tanzania Bara na visiwani bila kuleta machafuko
 
Huku zanzibar bora msije watu nyie mtamwagiwa tindi kali bure,ni hivi kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya tanzania ameshindwa kuutatua mgogoro huu wa zanzibar nyie mnakuja kufanya nn?
 
Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Peter Kuga Mziray amesema wanajipanga kukutana na kuitisha baraza la mashauriano baina ya vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC wakati wowote visiwani Zanzibar kwa ajili ya majadiliano.

Hilo baraza kama ni la nchi huru ya Zanzibar na wajumbe wa hivyo vyama ni wazanzibari watupu wenye vitambulisho vya mzanzibari wana Haki kisheria kukutana na ZEC kuongelea uchaguzi wa Zanzibar.Lakini kama viongozi wenyewe ni hawa akina Kuga Mziray wa nchi ya tanganyika kwenda kuongelea Zanzibar mambo ya uchaguzi wa Zanzibar ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya muungano na ile ya Zanzibar sababu uchaguzi wa Zanzibar si jambo la muungano.

Wanachofanya akina Kuga Mziray ni uvunjaji katiba na uingiliaji mambo ya ndani ya Zanzibar kutoka kwa raia wa nchi nyingine ya Tanganyika.
ZEC iwapuuze na isikutane nao hadi iwe na uhakika kuwa inakutana na wazanzibari tu sio watu wa nchi zingine za nje ikiwemo Tanganyika.
 
Kiukweli baraza la vyama vya siasa halina faida yeyote.kuna wakati fulani ilikubaliwa kuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 katiba iliyopo ilipaswa kufanyiwa marekebisho hili kukidhi mahitaji ya sasa lkn haikufanyika na baraza halikufanya chochote ma kubaliano yao na aliyekuwa rahisi wakati huo 2014
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…