Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,957
- 13,717
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuwasilisha hoja akilitaka Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) kuwasaidia wahitimu kwa kuwapatia Leseni mapema kwa kuwa wanapitwa na fursa nyingi Mtaani, ufafanuzi umetolewa na Baraza hilo.
Kusoma hoja ya awali, bofya hapa ~ Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) mtusaidie tupate Leseni mapema, fursa zinatupita Mtaani
Uhusiano na Mawasiliano wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), Ezekiel Nyalusi amezungumza na JamiiForums na kuelezea kinachoendelea kwa kusema hivi:
“Kwanza ifahamike Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni mamlaka ambayo inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Kinga ya Mwaka 2010 na kanuni zake.
"Kwa mujibu wa Sheria hiyo, moja ya jukumu ni kuorodhesha Wauguzi na Wakunga wote baada ya kuhitimu kwenye vyuo vyao, wanakuja kufanya mtihani wa Usajili na leseni kwetu.
“Usajili huo unafanya kwa mujibu wa Kifungu cha 21 ambapo Msajili atatoa Leseni kwa Muuguzi na Mkunga, leseni na vyeti vyote vinaweza kuuishwa kadiri itakavyotakiwa.
Utaratibu wa Utoaji Leseni
“Muuguzi akifaulu, ataitwa kwa ajili ya kula kiapo, akiapishwa ndio anakabidhiwa Leseni na Cheti kutoka Baraza.
“Huyo mtoa mada (Mdau wa JamiiForums.com) anataka kwenye akaunti yake isomeke kuwa anaruhusiwa kufanya kazi licha ya kuwa hajasajiliwa wala kuorodheshwa na kwa maana hiyo bado hajaapishwa.
“Takribani zilizopo ni kuwa Wauguzi 3,500 walifaulu na wapo kwenye orodha yetu, hadi jana kati yao takribani 2,000 walikuwa wapo kwenye mchakato wa kuhakikiwa kuhakikisha wanaingia kwenye daftari.
“Kinachofanyika kwa sasa ni maandalizi ya mahafali, hivyo Mwanafunzi hataweza kuona Leseni yake hadi ale kiapo siku ya mahafali.
“Inawezekana hali ya kisoko kwa sasa inachangia Mwanafunzi kuona anahitaji Leseni haraka kwa kuwa anaona amehitimu, pia inawezekana wanaosisitiza hivyo wana presha ya kupata kazi.
“Itabulike kuwa kutangaza majibu ya ufaulu wao mapema haimaanishi ndio kuwahi kutoa leseni, kuna mchakato unaendelea, na kawaida zoezi hilo huwa linachukua Siku 60 – 67, hivyo mpaka sasa bado tupo ndani ya muda.
“Kuhusu mahafali bado tupo kwenye taratibu za kuandaa, kawaida huwa inategemea na mchakato wa Leseni kukamilika, hakuna tarehe maalum ambayo imeshapangwa, tunatoa wito wawe watulivu kipindi hiki mambo yapo katika mchakato.”