benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,186
Agosti 20, mwaka huu, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), lillibua miadala baada ya kuitaka Serikali kusitisha mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), kwa sababu ya hoja kadhaa, ikiwamo wananchi walio wengi hawakubaliani nao.
Kwamba Watanzania na baraza hilo, hawakubaliani na IGA. Kwamba, hata kuwe na mazuri kiasi gani, maaskofu wamesema kwa ajili ya umoja na amani ni vema wana nchi kusikilizwa chini ya mamlaka waliyonayo katika ibara ya 8 ya Katiba.
Wakisema huo ni moja ya mikataba mibovu na ya hovyo kuwahi kutokea Tanzania. Kwamba ni bora kupata matokeo hasi kwa kuendesha bandari wenvewe tukiwa huru badala ya matokeo chanya utumwani chini ya uwekezaji wa DP-World. Katika hoja 10 za baraza hilo ni pamoia na kampuni moja ya DP-World kutawala kazi ndogo za ndani na kukosekana muda wa ukomo.
TEC inatoa hoja hiyo ikiwa ni taasisi yenye nguvu na msaada mkubwa wa maendeleo ya kiroho, kijamii na kiuchumi katika Taifa chini ya jumuiya ndogo 67,000 na parokia 1,300.
Ni taasisi iliyoweka msingi wa matumaini kupitia misimamo inavolinda na kutetea masilahi ya Taifa. Imewahi kufanya hivyo na Watanzania wengi tumekuwa tukibarikiwa sana.
Ni kweli kwamba, mjadala huu umetawaliwa na makundi kadhaa, likiwamo la Watanzania wasiokuwa na uelewa kabisa wanaoweza kuathiriwa na ushawishi wa kundi linalopinga au kuunga mkono.
Binafsi nimeuelewa mkataba huu na asili yake kitaalamu bila kuvumbishwa na kundi lolote kwa sababu nawajibika pia kama Mtanzania kuhoji na kuchochea uwajibikaji wa Serikali.
Lakini kwa kuwa TEC ni taasisi yenye ushawishi, nasukumwa kuhoji maeneo manne yanayoweza kutusaidia Taifa kupata suluhu ya miadala huu wa sakata la bandari wakati Serikali ikiendelea kupokea maoni na kuyafanyia kazi.
Mtazamo wa kwanza ni kuhusu hoja 10 ilizowasilisha ambazo ni msingi wa kupinga mkataba huo wa IGA.
Kuhusu hoja hizi sijaelewa kwamba, ufafanuzi wa kitaalamu wa wataalamu wa Serikali hauaminiki? Nasema hivyo kwa sababu hoja hizi zote zilishajibiwa kitaalamu tena kwa ufasaha.
Hii kauli ya kwamba ni bora kupata matokeo hasi kwa kuendesha bandari wenyewe tukiwa huru badala ya matokeo chanya utumwani chini ya uwekezaii wa DP-World inatoka kwa wananchi gani? Nauliza hivyo kwa sababu Tanzania sio ya kwanza kuingia mikataba ya IGA inayohusisha huduma za kibandari.
Je, uchunguzi wa TEC unaeleza nini kuhusu uingiaji wa mikataba ya aina hiyo? Kwamba mataifa mengine yaliingia mizuri kuliko Tanzania au mikataba ya aina hiyo ina asili ya kufanana?
Mtazamo wa pili ni kuhusu uzalendo
Hivi ni kweli Serikali na timu nzima ilivohusika katika kuandaa na kusaini mkataba huo sio wazalendo au hawana uwezo wa kitaalamu?
Sawa, ngoja nijaribu kuamini hivyo, lakini vipi kuhusu Bunge, ni kweli pia halina uzalendo pamoja na uwezo wa kuchambua IGA kabla ya kuridhia au waliridhia kwa maslahi yao binafsi?
Sawa ngoja pia nijaribu kuamini pia hilo, lakini vipi kuhusu Mahakama iliyotafsiri hoja za vifungu vya IGA na kuna hakuna shida?
Je, ni kweli pia majaji hawakuwa na uwezo wa kutambua udhaifu kama wazalendo?
Mtazamo wa tatu unajengwa na hoja ya kimazingira.
Sijaelewa kwa nini TEC imeibuka na waraka huo kwa sasa ukiwa umesharidhiwa na Bunge, huku mahakama ikitoa baraka zake.
Katika muktadha huo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo siku chache zilizopita kupitia hotuba va dakika 40 alivoitoa alitu-kumbusha kumbe viongozi wa dini walishawasilisha maoni yao kwa pamoja.
Nikajiuliza vipi kuhusu huu waraka? Ni kwamba TEC imeamua kuleta maoni yake kwa umma nje ya maoni ya pamoja ya viongozi wa dini au mantiki yake ilikuwa ni kuishirikisha jamii kuhusu msimamo wake katika IGA?
Kama ndivyo ili iweje?
Mtazamo wa nne umejengwa katika hoja ya kukubalika kwa Watanzania Kwamba, hata kuwe na mazuri kiasi gani, maaskofu wamesema kwa ajili ya umoja na amani ni vema wananchi kusikilizwa chini ya mamlaka waliyonayo katika ibara ya 8 ya Katiba. Hoja hi ilikuwa na utafiti wa kutosha au ni kuteleza?
Nimeuliza hivyo kwa kuakisi ufafanuzi wa hoja tano za shemasi kuhusu uhalali wa mfumo wa vyama vingi ulitokana pia na ushawishi wa makundi mbalimbali, iki-wamo viongozi wa kanisa kabla ya Seri-kali kuridhia, licha ya asilimia ndogo sana kupendekeza hilo.
Hii inamaanisha nini katika uongozi? Tutafakari pamoja huku maslahi ya umoja na amani yetu ikiwa kipaumbele zaidi.
Imeandikwa kwenye gazeti la Mwananchi