DOKEZO Barabara ya Ntyuka Dodoma kutelekezwa, kodi za wananchi kutumika vibaya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hapa Dodoma mjini kuna ujenzi wa barabara ya Lami kutoka mjini kati kwenda Ntyuka [Dampo] kama kilometres 9, barabara ilifika hatua ya kumwaga changarawe, barabara imesimama toka mwezi wa tano [Mei 2024 ] wananchi wanapita kwenye barabara ya muda ambayo ni mbovu sana

Serikali mpaka Leo haijatuambia wananchi kwanini ujenzi umesimama muda mrefu na ni haki ya kikatiba kuambiwa au kupewa taarifa wananchi, tujue changamoto ni kweli Serikali haina hela kama mtaani wanavyosema, maana barabara imeanza kuharibika hata kabla ya ujenzi haujakamilika

JF ni sauti ya wananchi, naamini mkipaza sauti Serikali itakuja na majibu na kukamilisha ujenzi
 
Ni jambo la hatari sana, mwisho wa siku utasikia mkandarasi alilipwa kwa riba kwa sababu ucheleweshaji wa malipo ..kumbe ten percent..
 
Back
Top Bottom