Barabara ya lami ya Musoma-Makojo-Busekera kuanza kujengwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,337
1,113
Wizara ya Ujenzi inasema yafuatayo:

1. Matayarisho ya Manunuzi (kumpata Mkandarasi) yanakamilishwa. Barabara litajengwa kwa awamu mbili, kwa kuanza na km 40.

2. Randama (Kitabu cha Bajeti) kinasomeka hivi;
(2a) Ukurasa wa 116 unaorodhesha barabara hilo kwenye Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025
(2b) Ukurasa wa 129 unaorodhesha daraja la Suguti kuwa moja ya madaraja makubwa yatakayojengwa Mwaka wa Fedha 2024/25

Hadi leo hii, ni kilomita 5 tu zimejengwa kwa kiwango cha lami kwenye barabara letu la Musoma-Makojo-Busekera. Serikali inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kujenga barabara lote kwa kiwango cha lami.

Leo Bungeni, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameongelea ujenzi wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera, na ametoa ushauri wa Wizara ya Ujenzi kuongezewa Bajeti ya Mwaka 2024/25

CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa: tafadhali sikiliza ushauri alioutoa Prof Sospeter Muhongo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 30.5.2024

 
Back
Top Bottom